Kusitishwa kwa matokeo ya utabibu

BroBrain25

New Member
Jul 16, 2021
4
2
Naamin sasa ifike wakati kila mtu aamue kuvaa uhusika wake na kuchukua majukumu aliyonayo kama msimamizi au kama anaesimamiwa

(UMRI HAUFICHI DHAMBI)
Kauli hii itufanye tujichanganue kutokana na taarifa zinazoendelea kuwa wanafunzi wa utabibu wa LEVEL 5 Kufutiwa matokeo yao ya mitihani iliyofanyika Agosti mpaka September

Kama kweli Mitihani ilivuja hadi wanapewa hadi mwongozo wa usahishaji Je Hatuoni Hapo kuna Wale waliotunga Mitihani kabisa ndio Wahusika wakuu (Je Hilo ni kosa la wanafunzi au watunzi wa mitihani hiyo)!!? Hii inadhihirisha Ubovu wa sekta husika kuwa haina Uimara katika kusimamia mipango yake na michakato ya uendeshaj wa shughuli zake kwa kukosa kuwa na uaminifu JE WATU HAWA HUCHAGULIWA NA NANI NA WANATAKIWA KUWA NA VIGEZO GANI? Endapo umakini ungetumika na kuzingatia kila Hatua Leo hii tusingesikia Taarifa hizi za Taaruki Hivyo KOSA HILI NAWAPA SEKTA HUSIKA NA SIO VYUO KWA NAFASI YA KWANZA.

SWALI NI JE NANI HASWA ATAAMUA KUCHUKUA MAJUKUMU YA KUSIMAMIA MITIHANI HIYO NA KULIPA GHARAMA ZA UENDESHAJI MAANA KUNA CHANZO KINAELEZA MZAZI NA WANAFUNZI WAKITAHARUKI KUHUSU FEDHA ZA MITIHANI ZINAZOCHANGIWA KUFANIKISHA ZOEZI HILO je? Wizara itarusha mpira tena kulipisha wanafunzi hao na wazazi KWA KOSA LAO?

Au Wizara itatumia tena budget yake yenyewe kukamilisha zoezi hili Tukitambua kabisa hali ya uchumi wetu alafu sekta hizi nyeti zinaturudisha nyuma kwa kutumia Fedha za serikali si kwa maendeleo bali kuziba matundu yaliyotobolewa na watu wenye vibali kutoka kwao.

SWALI?
Je, mitihani hiyo haikuwa na wasimamizi kutoka wizarani? Na je hawakutoa taarifa za maendeleo ya mitihani!!? Kama zilitolewa basi wizara ieleze wazi mapema. Naamini kuna muda wa masomo wa level 6 ambapo ndo vijana hao walitakiwa kufikia kusoma na muda huo bado unasonga ukingoja wizara ifanye uchunguzi wake na watoe maamuzi hivyo wizara itambue kabisa kuwa pia mwongozo wake unatakiwa kuimarishwa na kusimamiwa ipasavyo na ifanye kazi zake kwa ufanisi kuepusha adha kama hizi kuendelea kutokea.

Nashukuru kwa kusoma hii ila nna chemsha bongo kwetu sis tusio wanafunzi😊😊😊 hivi ukiambiwa huu ndio utakuwa mtihani wako ukaonyeshwa maswali je? Utaendelea kufungua kitabu chako kujisomea au utatatua maswali yale ya mtihani😄😄 jibu tunalo
 
Back
Top Bottom