Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,553
- 41,060
Kwa miaka mingi tumekuwa na demokrasia, haki na uhuru wa hadaa, na watawala badala ya kufanya yale wanayoyataka wananchi, wao wanataka wananchi wafanye yale wanayoyataka wao watawala.
Tangu mwaka 2014, wananchi wote waliotoa maoni kupitia Tume ya Jaji Warioba, walisema wanataka katiba mpya. Na tume ile ya Warioba ndiyo Tume iliyotambulika kisheria, na ilitungiwa sheria na Bunge la JMT.
Licha ya wananchi wote, (kwa kupitia sampuli za waliotoa maoni), kusema wanataka katiba mpya, watawala wakapuuza matakwa ya wananchi. Watawala wakaamua kuhangaika na ya kwao, ambayo siyo kipaumbele cha wananchi. Hii ni dharau kubwa ya watawala kwa wananchi.
Hata Tume bandia ya kukusanya maoni kuhusu katiba mpya, iliyoundwa na Rais Samia, waliotoa maoni wote, hakuna hata mmoja aliyesema hataki katiba mpya. Wote walisema wanataka katiba mpya, wakatofautiana tu juu ya muda wa kuipata, na nini kiwemo. Bado watawala wamepuuza, hatuoni jitihada na harakati za watawala za kutekeleza takwa hili kuu la wananchi. Tena, inayoonekana ni dharau kwa wananchi, Mh. Rais Samia akathubutu kutamka kuwa yale yalikuwa ni maoni tu, wao ndio watakaoangalia nini kifanyike. Hii ni dharau kubwa kwa umma wa Watanzania. Namheshimu sana Rais Samia, na natambua jitihada zake kwenye baadhi ya mambo, lakini niseme wazi, kauli ile ilikuwa ni dharau kubwa kwa umma, na hakika alipotoka. Kauli ile ilimaanisha wao watawala wanaweza kuyakubali baadhi ya maoni ya wananchi, au wakayatupilia mbali yote, na kiyaweka ya kwao.
Kwa sasa, Serikali, na hasa Rais, atamke kama ana uwezo wa kusimamia mchakato wa kupata katiba mpya kwa wakati unaotakiwa au hapana. Na kama hana uwezo, wananchi tutafute namna nyingine ya kupatikana katiba mpya bila ya ushiriki wa Serikali. Serikali ibakie tu kwenye utekelezaji na siyo kutoa maoni au mwongozo.
Kwa sasa, Serikali, na hasa Rais, atamke, je, nchi yetu itaingia kwenye kipindi cha uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2024 ikiwa na katiba mpya? Je, tutaingia kwenye kipindi cha uchaguzi mkuu mwaka 2025 na katiba mpya? Kama jibu litakuwa hapana, SERIKALI ITAKUWA HAINA UHALALI WA KUENDELEA KUONGOZA KWA MAANA IMESHINDWA KUSIMAMIA JAMBO AMBALO NI KIPAUMBELE CHA UMMA.
Kauli yetu wananchi iwe, HAKUNA KATIBA MPYA, HAKUNA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITA, HAKUNA KATIBA MPYA HAKUNA UCHAGUZI MKUU.
Watanzania tutaamka lini? Mbona watawala wanachezea matakwa ya wananchi kwa namna ambayo wao wanataka? Msimamo wetu wananchi uwe, KIONGOZI ATEKELEZE MATAKWA YA UMMA, ASIYETEKELEZA MATAKWA YA UMMA NI ADUI WA UMMA.
Katika kupata katiba mpya iliyo nzuri, unahitajika ushiriki mkamilifu wa wananchi wote, vyama vya siasa vyote, viongozi wote, taasisi za kidini zote, taasisi za kiraia zote, n.k. Wananchi wote, walio ndani ya vyama vya siasa na nje ya vyama vya siasa, tupiganie kupata katiba mpya ambayo inalinda haki, uhuru, demokrasia na ustawi wa kila mtu, uwe mwananchi mwanachama wa chama cha siasa au hapana, uwe na dini au huna dini, uwe na elimu ndogo au kubwa, au namna nyingine yoyote iwayo.
Hata kwenye mataifa yenye katiba nzuri, sheria nzuri, viongozi wanatii sheria na katiba, viongozi wanaheshimu umma, huwa siyo kwa sababu watawala ni waungwana sana, bali wananchi wa mataifa hayo, wamesimama imara kulinda mamlaka yao, na kuwafanya viongozi kuwa waoga kutotimiza matakwa ya umma, kwa sababu wasipotekeleza matakwa ya umma, umma unawawajibisha viongozi mara moja.