Kusipokuwa na Katiba Mpya, Siyo tu Vyama vya Upinzani Visishiriki Uchaguzi Bali Hata Uchaguzi Wenyewe Usifanyike

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,219
40,450
Kwa miaka mingi tumekuwa na demokrasia, haki na uhuru wa hadaa, na watawala badala ya kufanya yale wanayoyataka wananchi, wao wanataka wananchi wafanye yale wanayoyataka wao watawala.

Tangu mwaka 2014, wananchi wote waliotoa maoni kupitia Tume ya Jaji Warioba, walisema wanataka katiba mpya. Na tume ile ya Warioba ndiyo Tume iliyotambulika kisheria, na ilitungiwa sheria na Bunge la JMT.

Licha ya wananchi wote, (kwa kupitia sampuli za waliotoa maoni), kusema wanataka katiba mpya, watawala wakapuuza matakwa ya wananchi. Watawala wakaamua kuhangaika na ya kwao, ambayo siyo kipaumbele cha wananchi. Hii ni dharau kubwa ya watawala kwa wananchi.

Hata Tume bandia ya kukusanya maoni kuhusu katiba mpya, iliyoundwa na Rais Samia, waliotoa maoni wote, hakuna hata mmoja aliyesema hataki katiba mpya. Wote walisema wanataka katiba mpya, wakatofautiana tu juu ya muda wa kuipata, na nini kiwemo. Bado watawala wamepuuza, hatuoni jitihada na harakati za watawala za kutekeleza takwa hili kuu la wananchi. Tena, inayoonekana ni dharau kwa wananchi, Mh. Rais Samia akathubutu kutamka kuwa yale yalikuwa ni maoni tu, wao ndio watakaoangalia nini kifanyike. Hii ni dharau kubwa kwa umma wa Watanzania. Namheshimu sana Rais Samia, na natambua jitihada zake kwenye baadhi ya mambo, lakini niseme wazi, kauli ile ilikuwa ni dharau kubwa kwa umma, na hakika alipotoka. Kauli ile ilimaanisha wao watawala wanaweza kuyakubali baadhi ya maoni ya wananchi, au wakayatupilia mbali yote, na kiyaweka ya kwao.

Kwa sasa, Serikali, na hasa Rais, atamke kama ana uwezo wa kusimamia mchakato wa kupata katiba mpya kwa wakati unaotakiwa au hapana. Na kama hana uwezo, wananchi tutafute namna nyingine ya kupatikana katiba mpya bila ya ushiriki wa Serikali. Serikali ibakie tu kwenye utekelezaji na siyo kutoa maoni au mwongozo.

Kwa sasa, Serikali, na hasa Rais, atamke, je, nchi yetu itaingia kwenye kipindi cha uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2024 ikiwa na katiba mpya? Je, tutaingia kwenye kipindi cha uchaguzi mkuu mwaka 2025 na katiba mpya? Kama jibu litakuwa hapana, SERIKALI ITAKUWA HAINA UHALALI WA KUENDELEA KUONGOZA KWA MAANA IMESHINDWA KUSIMAMIA JAMBO AMBALO NI KIPAUMBELE CHA UMMA.

Kauli yetu wananchi iwe, HAKUNA KATIBA MPYA, HAKUNA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITA, HAKUNA KATIBA MPYA HAKUNA UCHAGUZI MKUU.

Watanzania tutaamka lini? Mbona watawala wanachezea matakwa ya wananchi kwa namna ambayo wao wanataka? Msimamo wetu wananchi uwe, KIONGOZI ATEKELEZE MATAKWA YA UMMA, ASIYETEKELEZA MATAKWA YA UMMA NI ADUI WA UMMA.

Katika kupata katiba mpya iliyo nzuri, unahitajika ushiriki mkamilifu wa wananchi wote, vyama vya siasa vyote, viongozi wote, taasisi za kidini zote, taasisi za kiraia zote, n.k. Wananchi wote, walio ndani ya vyama vya siasa na nje ya vyama vya siasa, tupiganie kupata katiba mpya ambayo inalinda haki, uhuru, demokrasia na ustawi wa kila mtu, uwe mwananchi mwanachama wa chama cha siasa au hapana, uwe na dini au huna dini, uwe na elimu ndogo au kubwa, au namna nyingine yoyote iwayo.

Hata kwenye mataifa yenye katiba nzuri, sheria nzuri, viongozi wanatii sheria na katiba, viongozi wanaheshimu umma, huwa siyo kwa sababu watawala ni waungwana sana, bali wananchi wa mataifa hayo, wamesimama imara kulinda mamlaka yao, na kuwafanya viongozi kuwa waoga kutotimiza matakwa ya umma, kwa sababu wasipotekeleza matakwa ya umma, umma unawawajibisha viongozi mara moja.
 
Binafsi mpaka sasa sijajua wananchi tunashindwa wapi kuwawajibisha hawa watawala wababe na jeuri kwetu! Eti mpaka wanawake wa Iran wameweza! Sisi bado tu tumelala.

Inahuzunisha sana. Yaani mtu anafikia hatua ya kuwakejeli na kuwatukana! Lakini bado tunaifyata tu mikia yetu.
 
Haya maneno ungeongea wakati wa jiwe ungeonekana jasir sana!
 
Uamsho wa kudai katiba mpya lazima uwepo na uchochewe mpaka moto wa mabadiliko uchome nafsi za watawala.

Wachochezi kamwe wasiwe wanasiasa ambao wengi wao hujali matumbo yao tu.

Katiba mpya iwe ajenda endelevu, wanasiasa na watawala ambao hawawezi kusimamia hoja ya utekelezaji wa katiba mpya wakae pembeni.

Ikiwezekana tuwakatae sio kwenye sanduku la kura tu bali hata kitaa wakipita tuwaonyeshe vidole vinavyostahili kutokana na matendo yao.

Kama tunashindwa kuongea, kupaza sauti na kukemea basi kila mwananchi atumie kidole chake au vidole vyake kuonyesha hisia zake hapa namaanisha lugha ya mwili itumike.
 
Umetulia na tekno boom yako unaongea kama una nguvu vile
Hii freedom ya social platform watu mnajiona wakubwa sana
 
Kwa miaka mingi tumekuwa na demokrasia, haki na uhuru wa hadaa, na watawala badala ya kufanya yale wanayoyataka wananchi, wao wanataka wananchi wafanye yale wanayoyataka wao watawala.

Tangu mwaka 2014, wananchi wote waliotoa maoni kupitia Tume ya Jaji Warioba, walisema wanataka katiba mpya. Na tume ile ya Warioba ndiyo Tume iliyotambulika kisheria, na ilitungiwa sheria na Bunge la JMT.

Licha ya wananchi wote, (kwa kupitia sampuli za waliotoa maoni), kusema wanataka katiba mpya, watawala wakapuuza matakwa ya wananchi. Watawala wakaamua kuhangaika na ya kwao, ambayo siyo kipaumbele cha wananchi. Hii ni dharau kubwa ya watawala kwa wananchi.

Hata Tume bandia ya kukusanya maoni kuhusu katiba mpya, iliyoundwa na Rais Samia, waliotoa maoni wote, hakuna hata mmoja aliyesema hataki katiba mpya. Wote walisema wanataka katiba mpya, wakatofautiana tu juu ya muda wa kuipata, na nini kiwemo. Bado watawala wamepuuza, hatuoni jitihada na harakati za watawala za kutekeleza takwa hili kuu la wananchi. Tena, inayoonekana ni dharau kwa wananchi, Mh. Rais Samia akathubutu kutamka kuwa yale yalikuwa ni maoni tu, wao ndio watakaoangalia nini kifanyike. Hii ni dharau kubwa kwa umma wa Watanzania. Namheshimu sana Rais Samia, na natambua jitihada zake kwenye baadhi ya mambo, lakini niseme wazi, kauli ile ilikuwa ni dharau kubwa kwa umma, na hakika alipotoka. Kauli ile ilimaanisha wao watawala wanaweza kuyakubali baadhi ya maoni ya wananchi, au wakayatupilia mbali yote, na kiyaweka ya kwao.

Kwa sasa, Serikali, na hasa Rais, atamke kama ana uwezo wa kusimamia mchakato wa kupata katiba mpya kwa wakati unaotakiwa au hapana. Na kama hana uwezo, wananchi tutafute namna nyingine ya kupatikana katiba mpya bila ya ushiriki wa Serikali. Serikali ibakie tu kwenye utekelezaji na siyo kutoa maoni au mwongozo.

Kwa sasa, Serikali, na hasa Rais, atamke, je, nchi yetu itaingia kwenye kipindi cha uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2024 ikiwa na katiba mpya? Je, tutaingia kwenye kipindi cha uchaguzi mkuu mwaka 2025 na katiba mpya? Kama jibu litakuwa hapana, SERIKALI ITAKUWA HAINA UHALALI WA KUENDELEA KUONGOZA KWA MAANA IMESHINDWA KUSIMAMIA JAMBO AMBALO NI KIPAUMBELE CHA UMMA.

Kauli yetu wananchi iwe, HAKUNA KATIBA MPYA, HAKUNA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITA, HAKUNA KATIBA MPYA HAKUNA UCHAGUZI MKUU.

Watanzania tutaamka lini? Mbona watawala wanachezea matakwa ya wananchi kwa namna ambayo wao wanataka? Msimamo wetu wananchi uwe, KIONGOZI ATEKELEZE MATAKWA YA UMMA, ASIYETEKELEZA MATAKWA YA UMMA NI ADUI WA UMMA.

Katika kupata katiba mpya iliyo nzuri, unahitajika ushiriki mkamilifu wa wananchi wote, vyama vya siasa vyote, viongozi wote, taasisi za kidini zote, taasisi za kiraia zote, n.k. Wananchi wote, walio ndani ya vyama vya siasa na nje ya vyama vya siasa, tupiganie kupata katiba mpya ambayo inalinda haki, uhuru, demokrasia na ustawi wa kila mtu, uwe mwananchi mwanachama wa chama cha siasa au hapana, uwe na dini au huna dini, uwe na elimu ndogo au kubwa, au namna nyingine yoyote iwayo.

Hata kwenye mataifa yenye katiba nzyri, sheria nzuri, viongozi wanatii sheria na katiba, viongozi wananheshimu umma, huwa siyo hisani ya watawala bali wananchi wamesimama imara kulinda mamlaka yao, na kuwafanya viongozi kuwa waoga kutotimiza matakwa ya umma, kwa sababu wasipotekeleza matakwa ya umma, umma unawawajibisha viongozi mara moja.
Nchi hii ina mambo mengi ya kufanya serikali haiwezi kukaa kila siku iwasikilize watu wasio na hoja ikaacha kuhudumia wananchi wao wakae pembeni maisha yataendelea sio lazima kila tuongelee siasa Kuna maendeleo pia.
 
Unaelewa maana ya maendeleo?

Kuwa na mifumo bora ambayo msingi wake mkuu ni katiba, ndiyo hatua ya kwanza ya maendeleo. Ukosefu wa maendeleo ya mifumo mbalimbali ya kusimamia utawala, haki, demokrasia, uzalishaji, sheria, tekinolojia, elimu, tafiti, vyote kwa pamoja husababisha uduni wa maendeleo ya kiuchumi.

Ndiyo maana hata makampuni makubwa yanapotaka kwenda kuwekeza katika Taifa fulani huangalia mambo mbalimbali ikiwemo sheria za hilo Taifa, utawala, mifumo ya kodi, n.k. Hivyo vyote vina mchango mkubwa katika kukupa usalama na mafanikio ya wa uwekezaji wako.
 
Umetulia na tekno boom yako unaongea kama una nguvu vile
Hii freedom ya social platform watu mnajiona wakubwa sana
Umechangia nini kqenye mada iliyopo? Iwe tekno, iphone, laptop, havina uhusiano na mada iliyopo.

Nitashukuru kupata mchango wako kwenye mada iliyopo na siyo kifaa kilichotumika kufikisha hoja.
 
Uamsho wa kudai katiba mpya lazima uwepo na uchochewe mpaka moto wa mabadiliko uchome nafsi za watawala.

Wachochezi kamwe wasiwe wanasiasa ambao wengi wao hujali matumbo yao tu.

Katiba mpya iwe ajenda endelevu, wanasiasa na watawala ambao hawawezi kusimamia hoja ya utekelezaji wa katiba mpya wakae pembeni.

Ikiwezekana tuwakatae sio kwenye sanduku la kura tu bali hata kitaa wakipita tuwaonyeshe vidole vinavyostahili kutokana na matendo yao.

Kama tunashindwa kuongea, kupaza sauti na kukemea basi kila mwananchi atumie kidole chake au vidole vyake kuonyesha hisia zake hapa namaanisha lugha ya mwili itumike.
Watawala na wanasiasa, wao wanaangalia tu namna gani katiba itawawezesha kuendelea kushikilia madaraka (kwa waliopo madarakani), na namna gani katiba itawawezesha kuingia madarakani (waliopo nje ya madaraka). Sisi wananchi zaidi uwepo wa katiba mpya tunautazama katika kuleta ustawi wa Taifa letu kwenye nyanja zote:

1) kwenye siasa, katiba mpya itusaidie kuwaweka na kuwaondoa madarakani viongozi kwa mifumo ya haki na isiyochezewa

2) kwenye utawala, katiba itupatoe haki ya kuwajibisha viongozi wasiotufaa, na kuwaondoa kiurahisi

3) kiuchumi, katiba itupatie haki na uhuru wa kujenga uchumi binafsi na uchumi wa nchi bila ya kugandamizwa au kuonewa na watawala

4) kwenye kodi, katiba itujengee misingi ya kuwa na kodi rafiki, na kodi zetu zisichezewe na watawala bali ziende kwenye vipaumbele vya umma

5) kwenye haki, katiba mpya ilinde haki za watu kuishi, kupata elimu, kupata matibabu, kupata makazi, kutoa maoni, kukosoa, n.k.

6) kwenye habari, katiba mpya impe haki mwananchi kupata taarifa za kweli na siyo kudanganywa na watawala au wanaomiliki vyombo vya habari
 
Umechangia nini kqenye mada iliyopo? Iwe tekno, iphone, laptop, havina uhusiano na mada iliyopo.

Nitashukuru kupata mchango wako kwenye mada iliyopo na siyo kifaa kilichotumika kufikisha hoja.
Hakuna nguvu ya kuzuia uchaguzi hakuna

Nguvu ambayo ipo ni yakususa na kupiga makelele kwenye mitandao kama hivi

Katiba mpya haipo na haitokuja kutokea tanzania
 
Kwa miaka mingi tumekuwa na demokrasia, haki na uhuru wa hadaa, na watawala badala ya kufanya yale wanayoyataka wananchi, wao wanataka wananchi wafanye yale wanayoyataka wao watawala.

Tangu mwaka 2014, wananchi wote waliotoa maoni kupitia Tume ya Jaji Warioba, walisema wanataka katiba mpya. Na tume ile ya Warioba ndiyo Tume iliyotambulika kisheria, na ilitungiwa sheria na Bunge la JMT.

Licha ya wananchi wote, (kwa kupitia sampuli za waliotoa maoni), kusema wanataka katiba mpya, watawala wakapuuza matakwa ya wananchi. Watawala wakaamua kuhangaika na ya kwao, ambayo siyo kipaumbele cha wananchi. Hii ni dharau kubwa ya watawala kwa wananchi.

Hata Tume bandia ya kukusanya maoni kuhusu katiba mpya, iliyoundwa na Rais Samia, waliotoa maoni wote, hakuna hata mmoja aliyesema hataki katiba mpya. Wote walisema wanataka katiba mpya, wakatofautiana tu juu ya muda wa kuipata, na nini kiwemo. Bado watawala wamepuuza, hatuoni jitihada na harakati za watawala za kutekeleza takwa hili kuu la wananchi. Tena, inayoonekana ni dharau kwa wananchi, Mh. Rais Samia akathubutu kutamka kuwa yale yalikuwa ni maoni tu, wao ndio watakaoangalia nini kifanyike. Hii ni dharau kubwa kwa umma wa Watanzania. Namheshimu sana Rais Samia, na natambua jitihada zake kwenye baadhi ya mambo, lakini niseme wazi, kauli ile ilikuwa ni dharau kubwa kwa umma, na hakika alipotoka. Kauli ile ilimaanisha wao watawala wanaweza kuyakubali baadhi ya maoni ya wananchi, au wakayatupilia mbali yote, na kiyaweka ya kwao.

Kwa sasa, Serikali, na hasa Rais, atamke kama ana uwezo wa kusimamia mchakato wa kupata katiba mpya kwa wakati unaotakiwa au hapana. Na kama hana uwezo, wananchi tutafute namna nyingine ya kupatikana katiba mpya bila ya ushiriki wa Serikali. Serikali ibakie tu kwenye utekelezaji na siyo kutoa maoni au mwongozo.

Kwa sasa, Serikali, na hasa Rais, atamke, je, nchi yetu itaingia kwenye kipindi cha uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2024 ikiwa na katiba mpya? Je, tutaingia kwenye kipindi cha uchaguzi mkuu mwaka 2025 na katiba mpya? Kama jibu litakuwa hapana, SERIKALI ITAKUWA HAINA UHALALI WA KUENDELEA KUONGOZA KWA MAANA IMESHINDWA KUSIMAMIA JAMBO AMBALO NI KIPAUMBELE CHA UMMA.

Kauli yetu wananchi iwe, HAKUNA KATIBA MPYA, HAKUNA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITA, HAKUNA KATIBA MPYA HAKUNA UCHAGUZI MKUU.

Watanzania tutaamka lini? Mbona watawala wanachezea matakwa ya wananchi kwa namna ambayo wao wanataka? Msimamo wetu wananchi uwe, KIONGOZI ATEKELEZE MATAKWA YA UMMA, ASIYETEKELEZA MATAKWA YA UMMA NI ADUI WA UMMA.

Katika kupata katiba mpya iliyo nzuri, unahitajika ushiriki mkamilifu wa wananchi wote, vyama vya siasa vyote, viongozi wote, taasisi za kidini zote, taasisi za kiraia zote, n.k. Wananchi wote, walio ndani ya vyama vya siasa na nje ya vyama vya siasa, tupiganie kupata katiba mpya ambayo inalinda haki, uhuru, demokrasia na ustawi wa kila mtu, uwe mwananchi mwanachama wa chama cha siasa au hapana, uwe na dini au huna dini, uwe na elimu ndogo au kubwa, au namna nyingine yoyote iwayo.

Hata kwenye mataifa yenye katiba nzuri, sheria nzuri, viongozi wanatii sheria na katiba, viongozi wanaheshimu umma, huwa siyo kwa sababu watawala ni waungwana sana, bali wananchi wa mataifa hayo, wamesimama imara kulinda mamlaka yao, na kuwafanya viongozi kuwa waoga kutotimiza matakwa ya umma, kwa sababu wasipotekeleza matakwa ya umma, umma unawawajibisha viongozi mara moja.
Chadema hawatashiriki ila Vyama vingine vitashiriki
 
Kila siku nasisitiza, bila machafuko tusitegemee box la kura kuheshimiwa, au katiba bora kupatikana. Kwenda kusimama kwenye mstari wa kura eti unachagua kiongozi kwa mazingira haya ni upuuzi wa hali ya juu. Ifahamike sio kila viongozi wa nchi hupatikana kwa box la kura. Mfano halisi ni viongozi hapa Tanzania. Ni sisi wananchi kuamua kwenda kupoteza muda kwenye mstari wa kura zisizoheshimiwa, ama kufanya machafuko Kupata katiba Bora.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom