Kusinyaa/Kuziba kwa mrija wa mkojo (Urethral stricture) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kusinyaa/Kuziba kwa mrija wa mkojo (Urethral stricture)

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Jul 1, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 1, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Mrija wa mkojo (urethra) ni kiungo muhimu kinachotoa mkojo nje ya mwili kutoka kwenye kibofu. Mrija huu unaposinyaa au kuziba hufanya utokaji wa mkojo kuwa wa mashaka na maumivu makubwa. Kusinyaa/ Kuziba kwa mrija wa mkojo huitwa pia urethral stricture.
  Visababishi na vihatarishi vya tatizo hili

  Kusinyaa kwa mrija wa mkojo husababishwa na kovu linalotokea katika sehemu ya mrija baada ya mtu kuumia, kufanyiwa upasuaji au kupona magonjwa ya zinaa. Inaweza pia kusababishwa na uvimbe karibu na eneo la kinena unaokandamiza mrija.

  Vihatarishi vya tatizo hili ni pamoja na:


  • Kuwa na historia ya kuugua magonjwa ya zinaa
  • kuwahi kuwekewa mipira ya mkojo au vifaa vya namna hiyo (catheter au cystoscope)
  • Kuvimba tezi dume (BPH) kwa wanaume
  • kuwa na historia ya kuumia au kupata majeraha maeneo ya kinena. Hii hutokea sana kwa wale wanaopata ajali wakiendesha baiskeli
  • Kupata maambukizi ya mara kwa mara ya mrija wa mkojo (urethritis)
  Ni nadra sana kwa tatizo hili kutokea kwa wanawake. Aidha ni nadra pia kwa mtoto kuzaliwa akiwa na tatizo hili (congenital urethral stricture).

  Dalili
  Mtu mwenye tatizo hili anaweza kuwa na dalili zifuatazo,


  • Kutoa shahawa zilizochanganyika na damu
  • Kukojoa mkojo mweusi au uliochanganyika na damu
  • Kupungua kwa kiasi cha mkojo kinachotolewa
  • Kukojoa kwa shida
  • kutoa uchafu katika mrija wa mkojo
  • kukojoa mara kwa mara
  • Kushindwa kumaliza mkojo wote
  • Kushindwa kuhimili kutoka kwa mkojo (mkojo kujitokea wenyewe/kujikojolea)
  • Maumivu wakati wa kukojoa
  • Maumivu chini ya tumbo
  • Maumivu ya kinena
  • Mtiririko dhaifu wa mkojo (hutokea taratibu au ghafla)
  • Mkojo kutawanyika ovyo wakati wa kukojoa
  • Kuvimba uume

  Uchunguzi


  Daktari atakufanyia uchunguzi wa mwili na namna unavyokojoa. Uchunguzi wa mwili unaweza kuonesha:


  • Kupungua kwa mkondo wa mkojo
  • Uchafu kutoka katika mrija wa mkojo
  • Kibofu kilichojaa/kuvimba
  • Kuvimba kwa mitoki ya maeneo ya kinena
  • Tezi dume iliyovimba au yenye maumivu
  • Kuhisi kitu kigumu chini ya uume
  • Uume kuvimba au kuwa mwekundu
  Hata hivyo, wakati mwingine uchunguzi unaweza usioneshe tatizo lolote lile.


  Vipimo


  Vipimo ni pamoja na:


  • Kipimo cha kuchunguza mrija pamoja na kibofu cha mkojo (cystoscopy)
  • Kuangalia kiasi cha mkojo kinachobaki katika kibofu baada ya kukojo (Post-void residual (PVR) volume)
  • X-ray ya mrija wa mkojo (Retrograde urethrogram)
  • Vipimo vya magonjwa ya zinaa
  • Uchunguzi wa mkojo (Urinalysis) pamoja na kuotesha mkojo (Urine culture)


  Matibabu


  Mrija unaweza kutanuliwa wakati wa kipimo cha cystoscopy na hiyo ikawa ndiyo mojawapo ya tiba.

  Iwapo njia ya kutanua mrija haioneshi mafanikio sana, upasuaji unaweza kuhitajika. Upasuaji unategemea eneo

  lilipo tatizo na ukubwa wa tatizo. Kama tatizo ni dogo/fupi na lipo mbali na bawabu inayotenganisha mrija na

  kibofu cha mkojo, linaweza kutatuliwa kwa kukata kasehemu kalikoziba wakati wa kufanya cystoscopy au kwa kuweka kifaa maalum cha kuzibua na kutanua mrija.

  Kama tatizo ni kubwa zaidi, upasuaji wa wazi wa eneo husika unaweza kufanyika. Upasuaji huu unajumisha kukata sehemu iliyoziba na kisha kukarabati sehemu hiyo.


  Kwa mgonjwa ambaye amepata shida ya ghafla ya kushindwa kutoa mkojo (acute retention of urine), matibabu ya dharura ya kumuwekea catheter kupitia juu ya kinena (suprapubic catherization) hufanyika. Hii husaidia kibofu kutoa mkojo nje kupitia kwenye bomba lililowekwa chini ya tumbo.

  Ifahamike kuwa mpaka sasa hakuna dawa ya tatizo hili zaidi ya njia za upasuaji na nyingine zilizoelezwa hapo juu.

  Matarajio

  Mara nyingi matibabu huleta matokeo mazuri na mgonjwa anaweza kuishi maisha yake kama kawaida. Hata hivyo wakati mwingine, mgonjwa anaweza kuhitaji matibabu ya mara kwa mara ili kuondoa sehemu ya kovu iliyopo katika mrija wa mkojo.

  Madhara ya tatizo hili

  Tatizo hili halina budi kutibiwa haraka maana kama likiachwa linaweza kusababisha kuziba kabisa kwa njia ya mkojo na kusababisha mkojo kujaa katika kibofu, hali ambayo, pamoja na kuleta maumivu makali kwa mgonjwa inaweza pia kusababisha figo kushindwa kufanya kazi (ARF).

  Kinga
  Ni muhimu kujikinga dhidi ya magonjwa ya zinaa kwa kufanya ngono salama au kuacha kabisa kufanya ngono. Aidha kuwa makini na kazi au mambo ambayo yanaweza kukusababishia kuumia maeneo ya kinena.

  Kusinyaa/Kuziba kwa mrija wa mkojo (Urethral stricture)
   
 2. Ellyson

  Ellyson JF-Expert Member

  #2
  Jul 28, 2016
  Joined: Nov 13, 2010
  Messages: 1,717
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Somo zuri sana. Kwani na mimi ni mmoja wa waathirika.
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Jul 29, 2016
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Pole sana ukihitaji tiba waweza kunitafuta nipate kukutibia upate kupona.
  Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano MziziMkavu Email barua ya pepe. fewgoodman@hotmail.com What's App na Viber +905344508169
   
Loading...