Kusindikiza milipuko kwa kampuni za uchimbaji madini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kusindikiza milipuko kwa kampuni za uchimbaji madini

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by ntamaholo, May 24, 2012.

 1. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #1
  May 24, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,142
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  Wakuu'

  salamu mbele siku zote.

  Nina jamaa yangu ni askari, na huwa anachukuliwa kwenda kusindikiza milipuko kwa ajili ya hawa wezi wanaoharibu mazingira yetu wakitafuta dhahabu sehem mbalimbali za nchi yetu.

  Kwa mjibu wa sheria ya milipuko, hairuhusu milipuko hiyo kusafirishwa bila kuwa na kibali cha afisa madini wa eneo husika, lakini pia bila kuwa na police escort.

  Kinachonisikitisha, ni malipo wanayopewa baada wakati wakisindikiza. ikumbukwe kuwa, askari wetu hawa, wanalazimika kusindikiza milipuko hiyo kisheria, lakini pia kwao inakuwa ni sherehe kwani akisafiri kwa siku wanapewa 50,000/tsh.

  Mimi naamini inawezekana kiwango kinachotambuliwa kimataifa ni kikubwa kuliko wanacholipwa hawa askari wetu, kusindikiza milipuko, ni sawa na kutembea na kifo mkononi.

  Mwenye kujua kiasi hasa anachotakiwa kulipwa askari wetu anijulishe niwataarifu hawa masoja wetu wanaohangaika kulisaka tonge, kwani mishahara yao hailingani na majukum waliyopewa na sheria zetu.

  nawasilisha
   
 2. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,142
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  mwenye taarifa sahihi anijuze tafdhali
   
 3. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #3
  Jul 12, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,142
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  Milipuko, milipuko, je tanzania hatuna elimu sahihi ya milipuko? Naombeni majibu nikawaelimishe wapiganaji wetu wajue namna ya kudai haki zao
   
 4. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #4
  Jul 12, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mkuu ni kweli askari wanafanya kazi hiyo na wanatakiwa kulipwa per diem kwa mujibu ya waraka wa serikali wa mwaka 2004. ambao kwa rank an file nadhani ni humohumo elfu 50 ama 60,,kwa ofisa huwa ni 80 elfu. So hakuna kupunjwa hapo.
   
 5. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #5
  Jul 13, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,142
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  Thamk U mmbangifingi. huo waraka waweza patikana tukauchungulia? kuna jamaa alitoa wa BOT alitoa namna wanavyosindikiza pesa, akasema, kuna pesa ya escort kwanza, halafu per diem iko pale pale. hii nayo ikoje, au inahusika pale BoT tu, hawa wezi wa madini wenyewe hawahusiki na utaratibu huo?
   
 6. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #6
  Jul 13, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Hawa "wezi" wa madini kwa utaratibu uliopo pale polisi ni kwamba wao ndo wanagharamia malipo hayo kwa askari.kuhusu waraka ni ule ambao watumishi wote wa umma wanaposafiri nje ya vtuo vyao vya kazi wanalipwa,,pamoja na yote haiyumkini kuna madudu kwenye inshu nzima hii
   
 7. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #7
  Jul 13, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,142
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  kwa watanzania, wizi ni sehemu ya maisha yao, na hii imetokana na serikali ya CCM kuwa dhaifu tangu kuwepo kwake. ukichukua kiwango cha wizi na rushwa kwa tanzani na Rwanda, utashangaa sana. Wakati rwanda wako mil. nane, bajeti yao iko trilion 16 za kitanzania na ni cash money, sisi iko 15trilion kwa watu milion 45 halafu mali kauli, inayotegemewa kukusanywa katika mchakato wa maisha. hivyo wizi upo kwa kuwa na mishahara isiyokidhi hali ya maisha

  anyway....

  kuna hii kitu inaitwa risk allowance, imeainishwa katika vitu gani wakati wa kusindikiza? na je usalama wa TAIFA ambao naamini wamesha acha kazi yao ya kulinda Taifa, na kujiingiza kulinda CCM wanahuskaje katika isue nzima za usindikizaji hasa wa milipuko?
   
Loading...