Kushuka kwa thamani ya shilingi dhidi ya dola si kigezo cha kuporomoka kwa shilingi

Lubebenamawe

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
1,952
2,194
Wadau,

Mimi si mtalaamu katika maswala ya uchumi ila elimu niliyonayo na uzoefu wa kibiashara vinanipa maarifa ya kuchangia kuhusu kushuka kwa thamani ya Tsh dhidi ya USD.

Kwa uzoefu na maarifa niliyonayo sikubaliana na hoja kwamba uchumi wetu unaporomoka kutokana na thamani ya TSH kushuka dhidi ya USD.

Watanzani tunapaswa kufahamu kuwa kuporomoka kwa thamani ya Tsh hakuwezi kuwezi kuthibitishwa kwa kulinganishwa na fedha ya nchi moja tu. Hii inawezekana kwamba fedha inayolinganishwa nayo inaweza kuwa imeimarika wakati Tsh iko pale pale.

Kwa hiyo itakuwa ni makosa kusema kuwa TSh imeporomoka kwa kuilinganisha na USD. Hali kadhalika itakuwa ni makosa kusema kuwa TSh imepanda thamani kwa kuilinganisha na USD pekee.

Kwa hiyo uthibitisho wa kwamba thamani ya Tsh imeporomoka unapaswa kufanyika kwa kuilinganisha Tsh dhidi ya fedha za kigeni zaidi ya tatu.

Kwa maana hiyo basi tunakujiridhisha kwamba thamani ya Tsh imeporomoka kwa kuilinganisha fedha za kigeni za nchi zaidi ya tatu mfano Dhidi ya Ksh, dhidi ya GBP, dhidi ya USD na pengine dhidi ya Rand(SA).
 
Ushasema wewe sio mtaalamu fumba domo lako!! Na ungoje wataalam waje na wewe usiye mtaalam ujifunze na sio kujaza nyuzi jf!
Sio kila jambo linaweza kufafanuliwa na wataalamu. Watu wenye uzoefu pia wanaweza kufafanua uchumi. Mi sina sijasomea uchumi, ila nafanya biashara, wakati mwingine navuka mipaka ya nchi kwa sababu ya biashara hivyo nina uzoefu katika ubadilishaji wa fedha za kigeni.
 
Umeandika mengi muhimu mkuu

ongezea na hili

Andika kwa tarakimu..imeshuka kutoka

1 usd ......nasasa ni 1usd........

shukrani.
 
Mkuu usikurupuke kuandika mambo usiyoyajua uchumi Ni taaluma kama huna taaluma husika omba msaada Au soma majarida mbalimbali utaelewa tu
 
Mkuu usikurupuke kuandika mambo usiyoyajua uchumi Ni taaluma kama huna taaluma husika omba msaada Au soma majarida mbalimbali utaelewa tu
Sija conclude kwamba Tsh imeporomoka thamani au la bali nimetoa angalizo tu kuwa si sahihi kuthibitisha kushuka kwa thamani ya Tsh kwa kuilinganisha na fedha moja tu ya kigeni. Jambo hilo la kutoa angalizo siyo lazima uwe mtaalam/ mbobezi ndiyo unaweza kufanya. Sasa kosa langu li wapi??? Au kwa sababu nimewashika pabaya wapotoshaji???
 
Sio kila jambo linaweza kufafanuliwa na wataalamu. Watu wenye uzoefu pia wanaweza kufafanua uchumi. Mi sina sijasomea uchumi, ila nafanya biashara, wakati mwingine navuka mipaka ya nchi kwa sababu ya biashara hivyo nina uzoefu katika ubadilishaji wa fedha za kigeni.
hata pogba wetu ana hulka kama wewe, anajidai anajua kila kitu kuanzia uchumi, uhandisi, utabibu wakati yeye ni mwalimu wa kemia! nadhani yanayotokea unayaona mwenyewe.
 
Mkuu kama sio mtaalam wa uchumi alaf unaandika Uzi wa ku-address uma si shaka kua unaupotosha umma. Better listen to professionals
 
Wadau,

Mimi si mtalaamu katika maswala ya uchumi ila elimu niliyonayo na uzoefu wa kibiashara vinanipa maarifa ya kuchangia kuhusu kushuka kwa thamani ya Tsh dhidi ya USD.

Kwa uzoefu na maarifa niliyonayo sikubaliana na hoja kwamba uchumi wetu unaporomoka kutokana na thamani ya TSH kushuka dhidi ya USD.

Watanzani tunapaswa kufahamu kuwa kuporomoka kwa thamani ya Tsh hakuwezi kuwezi kuthibitishwa kwa kulinganishwa na fedha ya nchi moja tu. Hii inawezekana kwamba fedha inayolinganishwa nayo inaweza kuwa imeimarika wakati Tsh iko pale pale.

Kwa hiyo itakuwa ni makosa kusema kuwa TSh imeporomoka kwa kuilinganisha na USD. Hali kadhalika itakuwa ni makosa kusema kuwa TSh imepanda thamani kwa kuilinganisha na USD pekee.

Kwa hiyo uthibitisho wa kwamba thamani ya Tsh imeporomoka unapaswa kufanyika kwa kuilinganisha Tsh dhidi ya fedha za kigeni zaidi ya tatu.

Kwa maana hiyo basi tunakujiridhisha kwamba thamani ya Tsh imeporomoka kwa kuilinganisha fedha za kigeni za nchi zaidi ya tatu mfano Dhidi ya Ksh, dhidi ya GBP, dhidi ya USD na pengine dhidi ya Rand(SA).

Mbona brah brah tu, mimi nadhani ungekuja na hoja ya kutueleza kwanza nini kinasababisha thamani ya hela kuporomoka, kuliko kusema unalinganisha fedha za kigeni za nchi zaidi ya tatu, alafu unatwambia elimu uliyo na uzoefu wa biashara, vinakupa mandate ya kuja hapa jukwaani kufafanua kwa nini shilingi ya Tanzania imeendelea kuporomoka kulinganisha na dola ya marekani. Si bora ungenyamaza tu, unaabisha hiyo bendera
 
Sija conclude kwamba Tsh imeporomoka thamani au la bali nimetoa angalizo tu kuwa si sahihi kuthibitisha kushuka kwa thamani ya Tsh kwa kuilinganisha na fedha moja tu ya kigeni. Jambo hilo la kutoa angalizo siyo lazima uwe mtaalam/ mbobezi ndiyo unaweza kufanya. Sasa kosa langu li wapi??? Au kwa sababu nimewashika pabaya wapotoshaji???
Unajua wewe ndo mpotoshaji namba moja! Hujui unatetea usichojua na hata hivyo mamraka ya kutangaza kuporomoka au kupanda niya mkuu wa nchi, sasa wewe sijui umetangulizwa kusafisha njia au vp tuambie tuelewe?
 
Kama vitu vingine hufahamu jaribu kuuliza sio kujifanya unajua kitu ambacho huna utaalamu nacho.
 
Mkuu China wanaidai USA maana kuna kipindi USA walikopa fedha China kuanzia 2010 USA wakawa wanaiomba China washushe thamani ya yuan ili USA watumie usd chache kulipia deni lao China waligoma kata kata 2014 mwishoni uchumi wa China ukaanza kuyumba na kupelekea fedha yao kushuka thamani against Usd huku usd ikiimarika mpaka 2016 march uchumi wa China umeanza kukua tena kwa 6.7% kwa 2016...hata Nchi chache Afrika zenye fedha imara kwa usd kama Botswana na SA uchumi wa hizo Nchi ni tofauti na Nchi ambazo unatumia fedha nyingi kupata 100 usd...
 
Mleta mada labda asaidiwe tu badala ya kupinga mada au uwezo wake wa kuelewa uchumi. Amefanya vizuri kukiri kwamba yeye sio mchumi, ila baadaye akajichanganya kwa kutoa hitimisho la kichumi kana kwamba yeye ni mchumi.

Labda nikuambie kwamba reference ya fedha nyingi duniani ni dollar ya marekani hata kama ela nyingine zipo kama British pound, Euro nk. Dollar ya marekani hata kama inapitwa kwa thamani na dola au sarafu nyingine ndio base au referral currency ya biashara karibu zote kati ya nchi na nchi. Unapoongelea kushuka kwa thamani ya fedha manake unaongelea biashara ya kimataifa ambayo mbabe au baba ni dollar ya marekani. Volume ya international trade duniani inapimwa kwa dollar ya marekani.

Lakini pia kumbuka na tilia manani point ifuatayo: Shilingi ikiteremka thamani dhidi ya US$, ndani ya muda mfupi zaidi ya muda unaotumia kupiga chafya, shilingi pia itateremka dhidi ya Bpound au fedha nyingine kuu za biashara ya dunia. Hii inatokana na kile wachumi wanaita triangular currency arbitrage, kwamba kama shilingi imeteremka dhidi ya dollar lakini ikapanda dhidi ya pound ya Uingereza kwa mfano, basi wenye dollar watanunua shilingi ili wanunulie pound kwa faida. Hili likitokea pound itajirekebisha kwa nayo kuishusha shilingi. Kwa msingi huu ushauri wako kwamba kupima kushuka kwa shilingi lazima kipimwe kwa kutumia sarafu nyingine zaidi ya tatu haitaleta utofauti wowote maana ela nyingine kubwa zitajirekebisha automatically.
 
Back
Top Bottom