LadyRed
JF-Expert Member
- Mar 19, 2016
- 9,636
- 11,449
Mkuu assumption za kiuchumi zilizofanywa awamu ya 4 zinagoma kabisa awamu hiiNa nilishangaa sana Kuona Ujenzi wake hasa Kipindi hiki wakati hali ya Kiuchumi Tanzania ( hasa Kibiashara ) si nzuri. Na ukitaka ulione vyema hilo Jengo pita wakati wa Usiku utaliona linapendeza lakini ndani yake hakuna Wapangaji kabisa. Ninachojua Wafanyabiashara Wakubwa na Wasomi huwa kabla ya Kuanzisha Biashara yoyote / Mradi wowote ule huwa wanatakiwa pia kufanya anticipation hasa ya Business Environment kwa wakati / kipindi husika na hata kwa baadae ili usiingie Hasara isiyokuwaa ya lazima.
Na wala tusifiche hapa hali ya Uchumi kwa Tanzania kwa sasa ni mbaya na Watanzania wengi wapo ICU hasa Kimaisha na kama Mheshimiwa Rais asipoambiwa ukweli na Wasaidizi wake ambao wao Wachache wanafaidika nae huku wakiwa wanamsifia na kumdanganya kuwa hali ni Shwari kuna Siku hawa hawa Watanzania waliopo ICU Kimaisha wanaweza Kuamua kufanya Jambo ambalo pengine linaweza Kuifanya Tanzania irejee ule mfano wa French Revolution ya 1789.
Rais apunguze Miradi mingi ambayo inachukua Pesa nyingi na Kuharibu Mzunguko wa Pesa kwa Wananchi, ahakikishe Watu wa TRA wanakuwa ni Chachu ya Kuboresha Biashara za Watu kwa kuwatoza Kodi Rafiki, Benki nazo ziweze Kutoa Mikopo ya Riba nafuu kwa Wananchi ili basi Watanzania baadhi wakianzisha Miradi yao zile Pesa ziweze Kuzunguka vyema miongoni mwao ila mkazo mkubwa pia uwekwe katika Sekta ya Kilimo hasa kwa kuwapa Nafuu Wakulima katika Bei za Mbolea na hata Vifaa vya Kilimo na kama haitoshi hata Masoko yao yawe wazi na Kasi ya Uwekezaji nchini iwe ya haraka ili hili Kundi Kubwa la Wasomi wasio na Ajira ( Kazi ) sasa waweze angalau Kuajirika huko.
Wakimaliza hilo warudi tena katika Mfumo mzima wa Elimu yetu Tanzania na yenyewe ibadilishwe na kuwa ya Research Based na siyo ile ya Kikoloni ya Content Based ambayo imezalisha Wasomi wengi wenye Uwezo wa Vyeti tu ( Theory ) ila 85% yao ukija katika Practical ni Watupu kabisa kiasi cha kuwafanya wengi wao wasiwe Competent na kuwa mojawapo ya sababu ya wengi wao / wetu kutoajirika. Masomo ya Biashara, Matangazo, Ubunifu, Sayansi, Utafiti na Ujasiriamali ndiyo yanatakiwa yapewe mno Kipaumbele kwa sasa nchini Tanzania na zile Fani zingine nazo hasa za Masomo ya Sanaa ( Arts ) nao Mitaala yao inatakiwa iboreshwe zaidi ili kuweze Kuendana na Mazingira ya sasa ya Kidunia ambayo yametaliwa na Teknolojia na Ubunifu zaidi.
Rais aambiwe huu Ukweli tafadhali na aupokee kwa mikono miwili na siyo aununie kwa kutuona tunaomwambia labda tunamchukia wakati kumbe yawezekana Sisi tulio mbali nae na ambao 24/7 tupo Mitaani na katika Jamii husika na huenda wengine tukawa ni Wahanga wa haya Maisha magumu ya sasa ndiyo tunampenda na ndiyo maana tunachukua muda wetu huu kumuandikia mambo kama haya ambayo kamwe kwa aina wa Viongozi wake wengi Wanafiki aliowateua na anaowaamini hawawezi Kumuambia ng'o.
Mfano kwenye real estate