fimboyaukwaju
JF-Expert Member
- Aug 3, 2020
- 5,608
- 7,166
Mimi ni mwislamu na ni mkimya sana,nasali na sijioneshi kabisa na mara nyingi navaa vizuri sana napoenda kusali,mara chache sana huwa navaa kanzu,nashiriki mikutano ya waislamu wenzangu lakini sio muongeaji sana,ila michango natoa.
Sasa marehemu mama yangu ndio alikuwa muislamu lakini alinifundisha kushiriki mikutano ya dini zingine na pia kuchangia. Basi huwa naenda RC,Sabato,KKKT na madhehebu mengine ya Kikristu,mikutano ya mabaniani napo kama kuna kazi nashiriki zote na michango natoa.
Nachofurahi makanisa yote ya kikristu wananijua na wananikubali na huja kwangu mara kwa mara ama kupata ushauri au kijia michango na nafurahia kabisa,na mahusiano mazuri mno na wachungaji,mapadri,masista,na hata viongozi wa dini za wahindi.
Namshukuru sana marehemu mama ambae alikuwa kila mahali yupo.Na Mungu ananitunza sana