Kushindwa na kufaulu kwa Maulid Said Mtulia

wandamba

JF-Expert Member
Apr 29, 2014
510
839
Mikutano ya kampeni ya uchaguzi mdogo jimbo la Kinondoni inazidi kushika kasi kwa kila Mgombea kunadi sera zake kwa jamii kwa kutoa ahadi kedekede za atakachowafanyia endapo akishinda uchaguzi Februari 17.

Maulid Said Mtulia ni mmoja wapo wa Wagombea kupitia tiketi ya CCM anayetetea kurudisha jimbo mikononi mwake. Leo tumulike kushindwa na kufaulu kwa Mtulia.

Kushindwa kwa Mtulia

Hapo awali Mtulia alikuwa Mbunge wa jimbo la Kinondoni kupitia tiketi ya Wananchi (CUF) alifaulu kidogo kuwatumikia Wananchi lakini kwa asilimia kubwa alishindwa kabisa kutimiza vyema majukumu yake kutokana na sababu kadhaa.

Mpasuko ndani ya CUF; Kutokana na misuguano na migogoro mikali ndani ya CUF kumepelekea chama kugawanyika pande mbili kwa kuwa na Wenyeviti wawili, Makatibu wakuu wawili, pamoja na makao makuu mawili. Kwa mujibu wa kauli za Mtulia anasema ulikuwa ukiegemea upande mmoja, unapewa misukosuko na upande mwingine. Alikuwa akipewa maagizo mawili mawili moja fanya na lingine usifanye. Katika mazingira hayo aliishia kubaki njia panda hali iliyopelekea kuzorota kwa utendaji kazi wake.

Kukosekana kwa ilani; Ilani iliyopewa ridhaa mwaka 2015 na Wananchi kuweza kutumika ni ilani ya CCM, yeye Mtulia wa CUF akishindwa kabisa kutimiza majukumu yake kutokana na ilani za CUF na CCM kutofautiana. Kilichokuwa kinatokea ni yeye kujiona amekabwa na sifa nyingi za utendaji kazi zilikuwa zikienda kwa Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa wilaya na Mawaziri na yeye kupotea kabisa kutokana na kukosa ilani ya kusimamia.

Mikwaruzano na Serikali: Muda mwingi sana chama cha CUF na wapinzani kwa ujumla utumia kuikosoa, kuisusia, na kutoipa ushirikiano Serikali. Katika mazingira hayo, maendeleo yangepatikana wapi? Pasipo kushirikiana na Serikali, pesa za maendeleo angezitoa wapi?

Licha ya changamoto nyingi lakini bado Mtulia yeye kama yeye alionyesha uwezo binafsi kwa kuzuia bomoa bomoa, aliwaombea hifadhi kwenye maghorofa mapya yanayojengwa wahanga bomoabomoa wapewe makazi pamoja na kutoa pesa zake mfukoni kunyonya maji na kuchimba mifereji.

Kufaulu kwa Mtulia

Leo hii Mtulia anapogombea tena Ubunge kwa tiketi ya CCM kuna kila dalili zinazoonyesha atafaulu kutimiza majukumu yake.

Ilani ya uchaguzi; Mtulia anagombea kwenye chama chenye dola, chenye ilani ya uchaguzi inayotekelezwa na Serikali iliyopo madarakani. Huu ni ushindi wa uhakika wa kufaulu kutimiza ahadi zake anazonadi kipindi hiki.

Uimara wa CCM; Mtulia anagombea kwenye chama chenye muundo imara, sera safi, chama kilicho na umoja na mshikamano, chama kinachojali na kuheshimu katiba yake. Ndani ya CCM kuna Mwenyekiti mmoja, Katibu Mkuu mmoja. Tofauti na chama cha CUF alichojiondoa.

Uzoefu; Mtulia ni mgombea pekee kwenye uchaguzi wa Kinondoni ambaye amekuwa Mbunge kwa miaka miwili aliyepata kujifunza na kujua kazi za
FB_IMG_1517597174274.jpg
Mbunge. Haendi Bungeni kujifunza, bali anaenda kutimiza wajibu wake kutokana na kuwa na uzoefu wa kutosha kumudu majukumu.

Twende mbele, turudi nyuma Maulid Said Mtulia ndiye mgombea pekee mwenye sifa za ziada za ubora wa kuwa Mbunge wa Kinondoni. Mtulia anabebwa vilivyo na ilani ya uchaguzi ya CCM 2015 - 2020, uimara wa CCM na uzoefu kiutendaji.
 
Peleka huko ujinga wako na Mtulia wako ambae ni msaliti tu, Chama dola nenda rudi kimekuwa na wabunge wengi ambao wakienda bungeni wanapiga usingizi, ni hadi mfumo wa luwepo upinzani ndo kidogo wabunge wa chama dola ingalao wanaamka, chama dola teyari kina wabunge wengi sasa Mtulia ataenda kufanya nini, unataka turudi kule kule kwenye kupiga usingizi
 
akishinda bac awamu zake ni miaka 2 tu kufika 2020.akikosa bac namkaribisha kijiweni na siasa kwa huyu mtu zimefka mwisho.kutoijua siasa ni kitu kibaya sana...
 
Peleka huko ujinga wako na Mtulia wako ambae ni msaliti tu, Chama dola nenda rudi kimekuwa na wabunge wengi ambao wakienda bungeni wanapiga usingizi, ni hadi mfumo wa luwepo upinzani ndo kidogo wabunge wa chama dola ingalao wanaamka, chama dola teyari kina wabunge wengi sasa Mtulia ataenda kufanya nini, unataka turudi kule kule kwenye kupiga usingizi
Ww unaishi kinondoni? ndomana ww ni
ee671cd5a98ff84239366ea2547acc05.jpg
 
Mtulia hakujiuzulu ubunge sababu ya mpasuko uliotokea katika chama alichotoka yeye amempenda ngosha balaa
 
Back
Top Bottom