Kushambuliwa MBUNGE Arusha, Nahodha Jiuzulu mara moja!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kushambuliwa MBUNGE Arusha, Nahodha Jiuzulu mara moja!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Uwezo Tunao, Dec 21, 2010.

 1. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #1
  Dec 21, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  KAMA HATA MHE MBUNGE HAYUKO SALAMA WANANCHI TUKIMBILIE WAPI???

  Kwa kitendo hiki cha ajabu (Askari Polisi Kumpiga Mh Mbunge) sana kuwahi kufanywa nchini mwetu, WAZIRI WA MAMBO YA NDANI PAMOJA NA SAID MWEMA WOTE WAJIUZULU mara moja kwa kuzingatia MSINGI WA UWAJIBIKAJI katika dhana zima ya Utawala bora na huyo askari awajibishwe kwa Maslahi ya Umma!!

  Hili la askari kumpiga mbele ya hadhara Mhe Mbunge mbele ya wananchi anaowaongoza kamwe HAIKUBALIKI na wala HAIVUMILIKI hata kidogo. Katika hili hakuna kiwango chochote cha MAELEZO WALA VISINGIZIO vitakavyoweza kutolewa kuhalalisha CHOMBO CHOCOTE KUMDHALILISHA KIONGOZI kiasi hicho.

  Chombo chetu cha jeshi la polisi KIKATIBA ni chombo USALAMA NA UTULIVU kumshambuliwa kiongozi yeyote bila kujali itikadi yake ya kisiasa nchini. Kitendo hiki hakina tofauti sana na kitendo cha KUMPIGA BABA AU MAMA MZAZI mbele ya watoto wake.

  Msononeko kwa watoto hautokaa ufutike kiurahisi kwenye kumbukumbu zao na hata kusadikiwa jambo kama hili kusababisha madhara makubwa kisaikolojia katika jamii. Ni kutokana na ukweli huu ndio MAANA SHERIA KOKOTE DUNIANI HUTOA ADHABU KALI MNO kwa wadhalilishaji wa aina ya askari polisi huyu wa Arusha.

  Siku zote watoto pale nyumbani huamini kwama ama BABA AU MAMA NDIO WATU WENYE NGUVU KULIKO WOTE DUNIANI kiasi kwamba wanapoona mashujaa wao hawa wakipigwa hadharani basi ujue moja kwa moja kwamba mpaka hapo Ulimwengu wao unakua umefunikwa juu kutazama chini.

  Kitendo cha KUSHAMBULIWA KWA MANENO NA KIWILI NA KUJERUHIWA kwa mwakilishi halali wa raia bungeni akiwa katika eneo lake ya kazi jimboni kwake Arusha ni kitendo UDHALILISHAJI MKUBWA mbele ya macho ya umma wa Tanzania.

  Kama hilo halitoshi na tunaiomba Bunge letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kamati zake za (i) Kamati ya Maadili na (ii) Kamati ya Ulinzi na Usalama kukutana mara moja na KUSHUGHULIKIA KWA NAMNA ITAKAVYOTURIDHISHA WANANCHI JUU YA HUU UTOVU MKUBWA WA NIDHAMU uliofanywa na askari wetu kwa kiongozi wa ngazi ya juu wa ngazi ya ubunge kama alivyofanyiwa Mhe Lema.

  Hili ni jambo zito lisilohitaji hiyana hata kidogo. Nani analo jibu atakayepigwa kesho au kesho kutwa kati ya viongozi wetu. Huwezi kujua kesho huenda akapigwa Waziri, Waziri Mkuu au hata Raisi wetu. Japo Rais katukashirisha sana alilolifanyia taifa kwenye uchaguzi mkuu lisilokubalika lakini mtu kumpiga hatuwezi kukubali hata kidogo.
   
 2. Mbaha

  Mbaha JF-Expert Member

  #2
  Dec 21, 2010
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 697
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hivi Godbless angekuwa wa CCM angefanyiwa hivyo kweli????!!!
   
 3. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #3
  Dec 21, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180

  Umesahau OCD wa Maswa alivyotandikwa Makofi na Mateke na mgombea wa CCM Robert Kisena?
  Polisi ni taasisi inayomilikiwa na CCM kwa hiyo hawawezi kumpiga au kumdhalilisha mbunge wa kupitia CCM.
  Nakumbuka kuna wakati Mkuu wa mkoa wa Manyara alimwamuru Ole Sendeka kutoka nje ya mkutano, alipogoma kutoka akamwamuru OCD kumtoa nje Sendeka, lkn alishindwa kufanya hivyo kwa kuwa ni wa CCM.

  Umaskini unaleta shida sana nchi hii.

   
 4. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #4
  Dec 21, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  MWANASHERIA MKUU WEREMA TUFAFANULIE KAMA KUWEPO UPINZANI KUNAMPUNGUZIA MTU HADHI NA HAKI YA URAIA WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  Mwanasheria Mkuu, Ndugu Werema nawe UNALO WAJIBU USIOKWEPEKA SAFARI HII wa kutuelewesha sisi Wa-Tanzania wenzako endapo mtu kuingia Chama Cha Upinzani au hata kuwa kiongozi wake kunampunguzia kiasi fulani cha haki zake za uraia wa taifa hili kiasi cha kudhalilishwa na vyombo vya dola kiasi hiki.

  Je, hatuna haki yetu humo kwenye katiba ya taifa tena?? Hili la SELECTIVE TREATMENT AND ADMINISTRATION OF LAW AND ORDER kama ilivyotokea kwenye mikasa ya kule Shinyanga na sasa kule Arusha, ndivyo sheria zetu zinavyoelekeza??? You have a duty to speak without any further delay on this.

  Kule Kigoma Mjini tumeona CCM kuandika na kuanika hadharani bango kubwa linalotoa MAELEKEZO WANAYOAMINI KUWA NI SAHIHI kwamba ili mwananchi aweze kupata HUDUMA ZOZOTE ZA KISERIKALI ni sharti kwanza awe na kadi ya chama hicho.

  Maana yake ni kwamba walioko upinzani wao walie tu hawana chao LICHA YA WAO PIA KUWA WALIPAKODI wa nchi hii kama wengine. Ndio kusema mfumo wa Vyama Vyingi tulivyoridhia katika katiba yetu ndivyo unavyotakiwa kuendeshwa???

  Hili nalo ni msingi wa watu kupata au kukosa mikopo benki, mikopo bodi ya mikopo kwa wanafunzi, huduma za maji na umeme. Ndivyo sheria inavyoelekeza??

  Kwingineko serikali inadiriki hata kutupotezea ajira kwa kumshambulia mfanyabiashara kwa kumtwisha mizigo viinimacho ya kodi toka TRA kwa sababu tu ni mpinzani na biashara yake ife - ndio kusimamia uchumi huku kwa mtindo huu kwa mujibu wa maelekezo ya katiba yetu tukufu???
   
 5. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #5
  Dec 21, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180


  Ameteuliwa na CCM hawezi kukupa jibu huyo unajisumbua bura brother.

   
 6. n

  nyantella JF-Expert Member

  #6
  Dec 21, 2010
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 890
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Lema mwenyewe anajua kiherehere chake ndicho kimemfanya apewe mkong'ote na bado!
   
 7. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #7
  Dec 21, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mbunge, sehemu yake rasmi ya kazi ni Jimboni kwake na kule bungeni anaenda tu kawakilisha waliomtuma mara moja na kurudi kwake. Sasa iweje Mbunge apigwe tena mbele ya macho ya watu wake anaowaongoza huku akiwa kazini kutekeleza wajibu wake wa kazi???

  Kwa nini kule Shinyanga mgombea tu ambaye wala hakubahatika kuwa Mbunge aweze kuingia kituo cha polisi na kupiga polisi ngala mpaka chini kisha kujipukuta vumbi na kujiondokea zake mpaka leo hii hajachukuliwa hatua kwa sababu tu ni mwana-CCM?? Inamaana SHERIA ZETU SASA HIVI NI ZA KIBAGUZI kwa ajili ya kuwatawala akina wale sio!!!
   
 8. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #8
  Dec 21, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  sioni sababu ya nahodha kujiuzulu wakati andengenye anaweza kuwajibishwa hata kwa sms na IGP wake

  kumuingiza waziri kwenye hili ni kuleta siasa... yawezekana huyu bwana alikua anatekeleza order ya mkuu wake wa kazi tu
   
 9. t

  truth Member

  #9
  Dec 21, 2010
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Can the police take courage to beat an MP just like that!!!? No one speaks of the wrong side of the MP that lead to the beating why? Ooh! I think I now know the answer most of us don't want to be accountable for our actions! Right?
   
 10. E

  Eberhard JF-Expert Member

  #10
  Dec 21, 2010
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 1,024
  Likes Received: 283
  Trophy Points: 180
  Kimsingi Hawa polisi wamefanya jambo baya. Mimi pia naamini kuwa kulikuwa na order kutoka juu.Hata hivyo hii inashiria ukosefu wa demokrasia safi nchini. kimsingi hii ni kama kuwapiga wananchi kwa sababu Lema anakalia kiti kwa ridhaa ya wananchi.Jamani Lema hayupo kenye kampeni tene, yeye ni mbunge(mheshimiwa) inapaswa aheshimiwe. Naamini kitendo hicho akijafanywa na CCM bali ni mtu mmoja anayefikilia kupandishwa cheo au kuonekana mchapa kazi akifikila anatetea CCM au anaogopa kuhamishiwa SIMIYU.
  From Eberhard
   
 11. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #11
  Dec 21, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Nachagua kuheshimu maoni haya lakini msimamo haujabadilika. Pindi tunapogawa majukumu ya kazi kitaifa kwa maana ya wizara mbali mbali, anayejulikana na kukabidhiwa hayo majukumu ya kipolisi ni Waziri wa Mambo ya Ndani.

  Wale polisi wengine wote ni kwamba wanamsaidia waziri husika kutekleza majukumu yake aliyoyaapia siku ile. Na kwa dhana ya Utawala Bora, anayewajibika moja kwa moja kubeba mzigo huo wa kwanza ni waziri na naibu wake ndipo vijana wao kufuata

  Kwa misingi ya kikatiba hatujampa Nahodha kazi ili akapate mshahara wala kukidhi matakwa fulani fulani kisiasa bali ni kwamba kazi hiyo kapewa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia kwa Rais ambaye kwa wakati wa kukabidhiwa jukumu hilo alikua ni Mhe Kikwete. Lengo ilikua ni kusimamia UTULIVU NA AMANI nchini kwa mujibu wa sheria za nchi bila upendeleo wala kubaguana.

  Sasa kwakuwa kumejitokeza undumrakuwili katika kutekeleza waji huo kati ya Shinyanga na Arusha kwa watu wenye hadhi zinazofanania kuwa ni viongozi wetu, Nahodha aondoke sasa hivi. Akichelewa wananchi watamsaidia kutoka.
   
 12. igwana123

  igwana123 Senior Member

  #12
  Dec 21, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 175
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kama Mh. Lema ameonewa basi aende mahakamani ili apate haki yake. nadhani hiyo ndio njia ya haki kuliko kulumbana bure hapa.
   
 13. j

  junior2008 JF-Expert Member

  #13
  Dec 21, 2010
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 528
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Humu zinajadiliwa hoja, na ni nguvu ya hoja inayotumika sio ushabiki wala uswahili. Hayo yapeleke kijiweni kwako!! Kazi ya jeshi la polisi ni kulinda usalama wa raia na mali zao na siyo vinginevyo. Waliyoyafanya kwa Mh Lema ni ukiukaji mkubwa wa haki sio tu za raia bali za mtu mwenye dhamana ya wananchi na wamefanya hayo kwa manufaa ya Mafisadi (CCM).
   
 14. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #14
  Dec 21, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kama kaonewa na serikali inayofanya shughuli za kipolisi KIUPENDELEO katika matukio yanayoshabihiana kama kule Shinyanga na Arusha, ushauri bado tu ni kwa huyu huyu Mhe Lema aliyeonewa na serikali katika dirisha 'A' la kutolea huduma kwa umma na aendelee kuota kwamba kwa serikali hiyo hiyo inayofanya kazi kwa upendeleo sasa itamtendea haki katika dirisha 'B' kwa sababu tu imeitwa mahakamani sio???

   
 15. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #15
  Dec 21, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Vijilante wanatisha
   
 16. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #16
  Dec 21, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana kabisa na wewe mkuu, hapa ni hoja tu. Mbunge apigwe na polisi ambaye jukumu lake kikatiba tunaifahamu fika je kesho sisi wengine si ndio tutaua kabisa Ma-Uswahilini kwetu huku mtu asiseme kitu!! Kunyamazia dhuluma ndio mtaji mkubwa kwa hawa akina Rostam Azizi.
   
 17. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #17
  Dec 21, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  jambo hili limejenga chuki kuu Arusha na wanamageuzi wote. Revenge will happen one day .yes I said so
   
 18. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #18
  Dec 21, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Mtu yoyote anayejua dhana ya utawala wa sheria sidhani kama atakubaliana na hatua waliochukua polisi wa Arusha kumpiga bwana Lema ( "sio kumpiga mbuge Lema" ). Lema achukuliwe kama raia mwingine yoyote ambaye anatakiwa kulindwa na polisi na wala sio kupigwa na anatakiwa kulindwa bila kujali itikadi yake ya kichama, kidini , kijinsia etc. Mara nyingi sana nimekuwa nikisema kuwa kipimo kikuu cha ustaarabu katika nchi ni utawala wa sheria na watu tukiona utawala wa sheria unapuuzwa na/au kudharauliwa si kitu cha kuingiza ushabiki na kuchekelea ni kitu cha kukemewa sana na kama utawala wa sheria unapuuzwa basi tujue kuna tatizo kubwa ambalo linaweza kutupeleka pabaya. Kwa viongozi itakuwa udikteta na wananchi wa kawaida itakuwa anarchy. Tusimame na kudai kuwa kila chombo cha serikali kifanye kazi kwa mipaka yake, polisi waliompiga washitakiwe, viongozi wao wajiuzulu kwa kuruhusu hali hiyo itokee na /au kwa kutochukua hatua kuzuia hali hiyo kutokea, waziri naye ajiuzulu ( ministerial responsibility) na mahakama isisthubutu kusema hilo ni suala la kisiasa.
   
 19. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #19
  Dec 21, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ndugu Rasta, kwa hayo maeneo yenye wino mzito wa bluu, mimi siwezi kutoa tena mawazo bora zaidi katika hili la polisi kujichagulia kuvunja sheria na maadili yao ya kazi!!

   
 20. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #20
  Dec 21, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  mahakamani kwenyewe nako mashaka.
   
Loading...