Kusaini Petition ina maana gani Tanzania??!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Nieleavyo mimi petition ni kusainiwa kwenye karatasi kuhusu jambo filani ambalo watu au kundi la watu wanapenda kulifikisha kwenye vyombo husika ili kuleta mabadiliko fulani kuhusu hilo wanalolipigania!

Lkn ili hili liwezekane ni lazima nchi husika pia iwe na utaratibu wa kisheria wa kuweza kulifanikisha hili kwa mfano labda sheria ya nchi husika inasema baada ya idadi ya watu kadhaa kusaini khs jambo fulani basi kisheria labda hilo jambo linapaswa kushughulikiwa lkn siyo kila nchi ina huu utaratibu na Je vipi kuhusu nchi yetu?

Kwa maana kila siku nasikia wimbo wa petition, petition mara sijui saini petition dhidi ya jambo fulani sasa je sheria zetu zinatambua petition? na kama inatambua ni idadi gani ya watu inayoilazimu sheria yetu kulishughulikia jambo?

Isije kuwa kama mambo mengine ambayo tunaiga tu bila ya kuelewa tunachokifanya, sasa ningependa kufahamu nchi yetu inatambua mambo ya petition? Kwa maana kama haitambui hii kusainishana petition kuliko shika kasi hakutakuwa na maana yoyote ile zaidi ya kupotezeana muda na kupotoshana tu!
 
Back
Top Bottom