Kusafiri bure walimu: Lengo zuri ila plan haijakaa vizuri

Nyanya mbichi

JF-Expert Member
Nov 10, 2011
3,716
2,215
Kama kichwa cha habari hapo juu, mh Makonda na serikali kwa ujumla wamekua na wazo zuri sana kama namna mzuri ya ku motivate walimu ila wamekosea kufanya wawe wanasafiri free off charge,hofu yangu ipo namna vile kondakta wanavyokejeli wanafunzi kwa kulipa 200 na pale raia anapogundua wakati wa kutaka amepungukiwa na 100 au 50 inakuwa kesi utatukanwa na kila mtu atajua umetoa pesa pungufu.

Kosa jingine kwanini iwe DSM tu isiwe Tanzania Yote? Sasa yale maneno ya rais kuwa DAR es salam ndio Tanzania yatakua YANATIMIA na watu badala ya kushawishiwa kuondoka/kupungua DAR watakua wanataka kuja Dar kusudi ya kupata priority kama ya kusafiri bure.

Askari wana unafuu kutokana na field yao.

Wazo langu kwanini serikali wasiwawekee fare allowances hao walimu?
 
Kidding

Konda : cheke cheke! abilia nauli

abiria: mi mwalimi

konda: onyesha kitambulisho

mwalimu: (anashika mfukoni) hiki hapa

konda (anakichukua kile kitambulisho na kukikodolea macho pande zote mbili)....

konda: (anarudisha kitambulisho) sasa mbona umekalia siti

mwalimu : kwan kuna tatizo?

konda: hebu wapishe waliolipa nauli wakae

mwalimu: (kwa hasira) hebu acha kunizaliliasha kijana

konda: (akimuangalia mwalimu usoni) hivi we unaona ni haki kukaa wakati alielipa nauli amesimama?

mwalimu (kimya)

konda: kwanza nyie walimu nina hasira na nyie sana

mwalimu (kwa ghadhabu) hasira?

konda: eeh kwanza mlinichapa sana bado nifeli.... na leo unapanda gari yangu huna nauli..

abiria wengine: hahahahahaha

konda: dah yani sipendi kupakia hizi chenga kubwa

mwalimu: nani chenga?

konda : yan wewe ni chenga kuliko huyo mwanafunzi unaemfundisha

mwalimu: (kwa tabasamu la aibu) kivipi?

konda : we umekalia siti hujalipa hata mia lakin dogo kasimama na amelipa 200..

konda (kwa kejeli) sasa sema wewe na dogo nan chenga?

mwalimu (kwa hasira anafungua pochi na kutoa sh 5000 ) kata mia nne yako mbwa wewe. WAZO NI GUMU KUTEKELEZEKA LABDA MWALIMU AWE NA ROHO YA JIWE
 
Mimi nadhani ni wazo zuri la kupunguza makali ya maisha kwa waalimu. Ila angewapa allowance za nauli kwenye mishahara yao. Vile vile je waalimu wa mikoa mingine vipi? Kwani wao hawapandi vyombo vya usafiri? Huo si ubaguzi?
 
hakika ni kuwadhalilisha walimu...ingekuwa me.mwalimu najilipia tu nauli yangu sitaki bugudha ya konda
 
Hahahaha kila siku tutajionea ngumi kati ya konda na walimu asee sipat picha mwalimu amekunjwa sharti na kondakta
 
Mimi nadhani ni wazo zuri la kupunguza makali ya maisha kwa waalimu. Ila angewapa allowance za nauli kwenye mishahara yao. Vile vile je waalimu wa mikoa mingine vipi? Kwani wao hawapandi vyombo vya usafiri? Huo si ubaguzi?
Umenena
 
Uko ni kukurupuka kama wana nia ya dhati kwenye moja ya mapato ya halmashauri wasitoe %flani wakawapa walim as transport allowance na ikawepo kisheria co tamko ambalo halina uharali wa sheria
 
Ni kwanini wengi wa wanasiasa hasa hawa wa kuteuliwa siyo wabunifu na wakibuni jambo linakuwa halina tija? Ni nini kilichomo kwenye bongo zao?
Huyu dc aliyesema walimu wa dar easafiri bure ni mbaguzi mno kwani walimu hawapo dar tu. Nini hatima ya walimu wa mikoa mingine? Na ni kwanini ni walimu tu? Kada nyingine hawahitaji kusafiri au kuwahi kazini?
Nikisema pesa za miradi ya ujenzi wa nyumba za watumishi wa umma mmezipiga na sasa mnataka kuwawekea pipi mdomoni ili wasipaze sauti zao nakosea? Kama kweli ana ndoto ya kumaliza tatizo aanzishe harambee za kujenga nyumba za walimu maeneo ya kazi na siyo vinginevyo.
Makonda tuache hatuhitaji kusafiri bure. Na cwt acheni kujifungia tokeni hadharani kupinga kudhalilishwa kwa wanachama wenu.
 
Kwa kuwa wameteuliwa hawajapata kazi kwa kutegema skill wanakosa ubunifu
 
Back
Top Bottom