Kurusha Matangazo ya Vipindi vya Bunge - Faida na Hazara zake zatajwa

josam

JF-Expert Member
Nov 22, 2011
2,241
1,031
Taarifa za kutokurusha moja kwa moja (LIVE) kwa matangazo ya vikao vya Bunge zimepokelewa kwa hisia tofauti tofauti mioni mwa Wananchi Tanzania.
Sababu zilizowahi kutolewa na Serikali zinakinzana kwa kiasi fulani na zile zilizotolewa na Bunge hivi karibuni ingawa sababu hizo zilizotolewa na Bunge zimeonekana kuungwa mkono na serikali kufuatilia kauli iliyotolewa waziri mwenye dhamana na habari, michezo na utamaduni ndg Nape Nnauye.

Kwa maoni yangu kama mtu huru siungi mkono sababu ama zilizotolewa na serikali ya awamu ya nne katika bunge lililo pita ama sababu zilizotolewa na ofisi ya Bunge na waziri Nape hivi karibuni. Watanzania wanayo haki na uhuru wa kuamua mambo yao kama wanavyo ona inawafaa. Waingereza waliitawala Tanzania lakini siyo kigezo cha kukopi na kupesti kila walifanyalo. Wawe Wafaransa, Waingereza ama Wamarekani ama mabunge ya Jumuiya ya Madola yapo tunayoweza kujifunza kutoka kwao na kuyatekeleza nchini kwetu lakini si kila jambo na hata hilo la kuchukua lazima lijadiliwe na watanzania kama wanaafiki hicho tunachotaka kuiga kutoka nje hususani kama kinagusa maisha na maslahi ya watanzania.

Utu na uhuru wetu uko wapi? Nani ana haki ya kuamua hatima ya Watanzania? Ni Mawaziri au Wabunge?
Bunge lionyeshwe live, visingio vya watu kuwa kazini siyo hoja. Mwanzo serikali ilisema kuonyesha vipindi vya bunge live vinasbabisha hasara. Leo hii kuja na hoja watu kutokupata muda wa kuangalia bunge muda wa kazi ni kioja kingine. Nini maana ya muda wa kazi? Kama sababu ndiyo hiyo kwa nini msizime luninga zote zisirushe matangazo yao kwa sababu hakuna watazamaji!!??? Hapa kazi tu, itaonekana inafanya kazi bala bala kama itajipambanua hata katika bunge. Serikali inalenga kuficha nini?

Hasara Vs Faida za kurusha matangazo live

1. Kupoteza muda watu wapo kazini- Watu wafika saa ngapi kutoka kazini? Nani atakuwa na muda wa kuangalia vipindi vilivyo rekodiwa wakati amechoka kwa kazi na usafiri, mfn wakazi wanao jishughulisha na shughuli zao Dsm wengi wao huamuka kuanzia saa kumi na hufika nyumbani hadi saa nne. Hivyo kujikuta amebakisha masaa yasiyo zidi mane kuamuka kwenda kazini!

2. Gharama kuendesha vikao vya bunge - .......kama ni suala la gharama mbona hamfuti uchaguzi mkuu na chaguzi nynginezo ndogondogo?? Huwa zinatumika shiling ngap kufanya chaguzi hizo? Mbona bunge ama Serikali haifuti gharama za kukimbiza mwenge ambao faida ni kidogo ukilinganisha na madhara ya kuratibu zoezi hilo HASA kiafya na kiuchumi? Kupanga ni kuchagua, kama taifa tunashindwa kubeba gharama za kurusha matangazo ya bunge live?

3. Wabunge wanatumia jukwaa hilo kujionyesha na kujikweza kisiasa. Ndiyo, lakini wananchi watutajuaje kwamba mbunge amesema na kutetea hoja za wananchi wake waliomchagua na kumtuma kuwakilisha?

4. Kunyima uhuru wananchi - Kurusha matangazo ya bunge ni jambo linalo leta faraja kwa wananchi. Hili ni jambo kubwa kuliko yote na Demokrasia ni gharama, uhuru ni gharama.

5. Kuonyesha wabunge wasiowajibika (mfn kusinzia katika ukumbi wa bunge, kutokuunga mkono mambo mazuri yenye manufaa kwa nchi) - kutorusha matangazo ni faida kwa wabunge wenyewe kwa sababu wavivu na wazembe hawataonekana lakini ni hasara kwa wale waliowaajili. Umahili na umakini wa wabunge utapungua kama vipindi vya bunge havitarusha live.

6. Kutorusha matangazo kuna faida kwa serikali na watendaji wake. Kuficha maovu ya watendaji wa serikali wanao shindwa kutekeleza majukumu yao hawataonekana wakati wakishindwa kujibu au kutoa ufafanuzi sahihi kuhusu mambo yanayo wahusu ndani ya vikao vya bunge. Hili ni hasara kwa WAAJILI (wananchi) wa wabunge na viongozi wa serikali.

Hitimisho:

Kama serikali na bunge wataendelea na msimamo wao wa kutorusha vipindi vya majadiliano ya bunge, vyombo hivyo viwatendee haki watanzania kwa kuwauliza wanataka nini kati ya hayo mawili. Namaanisha Serikali iitishe kura ya maoni kuhusu kurusha vipindi vya Bunge ama kutorusha! Watanzania waamue wenyewe kama serikali na bunge wameshindwa kuamua kwa maslahi zaidi ya watu walio waweka hapo au katika nafasi hizo wanazo lingia kuamua lolote wanalopendezwa nalo hata kama halina masilahi kwa watanzania wengi.
 
Taarifa za kutokurusha moja kwa moja (LIVE) kwa matangazo ya vikao vya Bunge zimepokelewa kwa hisia tofauti tofauti mioni mwa Wananchi Tanzania.
Sababu zilizowahi kutolewa na Serikali zinakinzana kwa kiasi fulani na zile zilizotolewa na Bunge hivi karibuni ingawa sababu hizo zilizotolewa na Bunge zimeonekana kuungwa mkono na serikali kufuatilia kauli iliyotolewa waziri mwenye dhamana na habari, michezo na utamaduni ndg Nape Nnauye.

Kwa maoni yangu kama mtu huru siungi mkono sababu ama zilizotolewa na serikali ya awamu ya nne katika bunge lililo pita ama sababu zilizotolewa na ofisi ya Bunge na waziri Nape hivi karibuni. Watanzania wanayo aki na uhuru wa kuamua mambo yao kama wanavyo ona inawafaa. Waingereza waliitawala Tanzania lakini siyo kigezo cha kukopi na kupesti kila walifanyalo. Wawe Wafaransa, Waingereza ama Wamarekani ama mabunge ya Jumuiya ya Madola yapo tunayoweza kujifunza kutoka kwao na kuyatekeleza nchini kwetu lakini si kila jambo na hata hilo la kuchukua lazima lijadiliwe na watanzania kama wanaafiki hicho tunachotaka kuiga kutoka nje hususani kama kinagusa maisha na maslahi ya watanzania.

Utu na uhuru wetu uko wapi? Nani ana haki ya kuamua hatima ya Watanzania? Ni Mawaziri au Wabunge?
Bunge lionyeshwe live, visingio vya watu kuwa kazini siyo hoja. Mwanzo serikali ilisema kuonyesha vipindi vya bunge live vinasbabisha hasara. Leo hii kuja na hoja watu kutokupata muda wa kuangalia bunge muda wa kazi ni kioja kingine. Nini maana ya muda wa kazi? Kama sababu ndiyo hiyo kwa nini msizime luninga zote zisirushe matangazo yao kwa sababu hakuna watazamaji!!??? Hapa kazi tu, itaonekana inafanya kazi bala bala kama itajipambanua hata katika bunge. Serikali inalenga kuficha nini?

Hasara Vs Faida za kurusha matangazo live

1. Kupoteza muda watu wapo kazini- Watu wafika saa ngapi kutoka kazini? Nani atakuwa na muda wa kuangalia vipindi vilivyo rekodiwa wakati amechoka kwa kazi na usafiri, mfn wakazi wanao jishughulisha na shughuli zao Dsm wengi wao huamuka kuanzia saa kumi na hufika nyumbani hadi saa nne. Hivyo kujikuta amebakisha masaa yasiyo zidi mane kuamuka kwenda kazini!

2. Gharama kuendesha vikao vya bunge - .......kama ni suala la gharama mbona hamfuti uchaguzi mkuu na chaguzi nynginezo ndogondogo?? Huwa zinatumika shiling ngap kufanya chaguzi hizo? Mbona bunge ama Serikali haifuti gharama za kukimbiza mwenge ambao faida ni kidogo ukilinganisha na madhara ya kuratibu zoezi hilo HASA kiafya na kiuchumi? Kupanga ni kuchagua, kama taifa tunashindwa kubeba gharama za kurusha matangazo ya bunge live?

3. Wabunge wanatumia jukwaa hilo kujionyesha na kujikweza kisiasa. Ndiyo, lakini wananchi watutajuaje kwamba mbunge amesema na kutetea hoja za wananchi wake waliomchagua na kumtuma kuwakilisha?

4. Kunyima uhuru wananchi - Kurusha matangazo ya bunge ni jambo linalo leta faraja kwa wananchi. Hili ni jambo kubwa kuliko yote na Demokrasia ni gharama, uhuru ni gharama.

5. Kuonyesha wabunge wasiowajibika (mfn kusinzia katika ukumbi wa bunge, kutokuunga mkono mambo mazuri yenye manufaa kwa nchi) - kutorusha matangazo ni faida kwa wabunge wenyewe kwa sababu wavivu na wazembe hawataonekana lakini ni hasara kwa wale waliowaajili. Umahili na umakini wa wabunge utapungua kama vipindi vya bunge havitarusha live.

6. Kutorusha matangazo kuna faida kwa serikali na watendaji wake. Kuficha maovu ya watendaji wa serikali wanao shindwa kutekeleza majukumu yao hawataonekana wakati wakishindwa kujibu au kutoa ufafanuzi sahihi kuhusu mambo yanayo wahusu ndani ya vikao vya bunge. Hili ni hasara kwa WAAJILI (wananchi) wa wabunge na viongozi wa serikali.

Hitimisho:

Kama serikali na bunge wataendelea na msimamo wao wa kutorusha vipindi vya majadiliano ya bunge, vyombo hivyo viwatendee haki watanzania kwa kuwauliza wanataka nini kati ya hayo mawili. Namaanisha Serikali iitishe kura ya maoni kuhusu kurusha vipindi vya Bunge ama kutorusha! Watanzania waamue wenyewe kama serikali na bunge wameshindwa kuamua kwa maslahi zaidi ya watu walio waweka hapo au katika nafasi hizo wanazo lingia kuamua lolote wanalopendezwa nalo hata kama halina masilahi kwa watanzania wengi.
ccm ccm ccm ccm ccm ccm!
 
Back
Top Bottom