Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Nimekuwa nikifuatilia taarifa zinazotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu, na kuona mara nyingi sana watoa taarifa ambazo kwa kweli zinapaswa tu kuripotiwa na magazeti ya kila siku badala ya kuzitoa kama taarifa rasmi kwenye headed paper ya kurugenzi.
Je, Kurugenzi ya Mawasiliano wameamua kuwa kuwa chombo cha propaganda za kisiasa za Raisi Magufuli badala ya kuwa chombo ambacho kinatoa taarifa muhimu na rasmi kwa wananchi?
Kwa mfano hili la Rais kufanya mazoezi na kutoa mchango wa milioni 20 kwa ajili ya wavuvi. Kweli hivi vitu ni vya kutolea taarifa rasmi kwenye headed paper ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu?
Kuna vitu vidogo vidogo vingi tu ambavyo Kurugenzi ya Mawasiliano huwa inaamua kuvitolea taarifa rasmi ambavyo kwa kweli wala havistahili kupewa hadhi ya taarifa rasmi kutoka Ikulu. Hii inashusha hadhi ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu na kufanya waonekane kama ni gazeti la mtaani au chombo cha Propaganda cha Rais. Tafadhali jirekebisheni.
Kwa nchi zetu sio jambo LA kushangaza hata kama ingekuwa wew lazima upalambelambeHuyo Greyson Msigwa na kundi lake wanajikomba sana kwa mkulu hadi wanatia aibu
Wataweka utaratibu wa kujisajili,hapo anuani ya makazi yako ya kudumu,kazi unayofannya,majina matatu unayotumia na kama ukihitajika kwa haraka ni wapi waweza patikana!Nashauri kwenye tovuti ya Ikulu kuwe na ka-option ka ku-comment ili tujue naniliu anaungwa mkono
Tatizo ni kwamba ili tupate hiyo taarifa siyo lazima Kurugenzi ya Mawasiliano iitoe kama taarifa rasmi. La sivyo siku moja Magufuli atatembelewa na mjomba wake pale Ikulu na Kurugenzi ya Mwasialo watatupa taarifa rasmi, "Leo Raisi Magufuli ametembelewa Ikulu na mjomba wake toka Chato"Milioni 20 aliyoitoa ni sehemu ya kodi tunazolipa hivyo sio vibaya tukipewa taarifa. Kama sijakosea bwana mkubwa analo fungu la mengineyo ambalo kwa mwezi linafika shilingi milioni 100.
Siku zote duniani kunakuwa na watu wa aina mbili - mashabiki wasiojua lolote na wanaokwenda upande wowote kwa kusukumwa, na wale walio na uwezo wa kufikiri, wanaowasukuma mashabiki. Ni rahisi kuona uko wapi kati ya haya makundi mawili.Kama umeshindwa kumfundisha kazi Mbowe ili aachie madaraka baada ya kuichakaza saccos , utaweza kuifundisha kazi kurugenzi ya ikulu??
Hahahaha, nimependa msisitizo wa hoja yako.Tatizo ni kwamba ili tupate hiyo taarifa siyo lazima Kurugenzi ya Mawasiliano iitoe kama taarifa rasmi. La sivyo siku moja Magufuli atatembelewa na mjomba wake pale Ikulu na Kurugenzi ya Mwasialo watatupa taarifa rasmi, "Leo Raisi Magufuli ametembelewa Ikulu na mjomba wake toka Chato"
Unawaonea ndugu unajua aliewaweka anataka kusikia nini,?Nimekuwa nikifuatilia taarifa zinazotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu, na kuona mara nyingi sana watoa taarifa ambazo kwa kweli zinapaswa tu kuripotiwa na magazeti ya kila siku badala ya kuzitoa kama taarifa rasmi kwenye headed paper ya kurugenzi.
Je, Kurugenzi ya Mawasiliano wameamua kuwa kuwa chombo cha propaganda za kisiasa za Raisi Magufuli badala ya kuwa chombo ambacho kinatoa taarifa muhimu na rasmi kwa wananchi?
Kwa mfano hili la Rais kufanya mazoezi na kutoa mchango wa milioni 20 kwa ajili ya wavuvi. Kweli hivi vitu ni vya kutolea taarifa rasmi kwenye headed paper ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu?
Kuna vitu vidogo vidogo vingi tu ambavyo Kurugenzi ya Mawasiliano huwa inaamua kuvitolea taarifa rasmi ambavyo kwa kweli wala havistahili kupewa hadhi ya taarifa rasmi kutoka Ikulu. Hii inashusha hadhi ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu na kufanya waonekane kama ni gazeti la mtaani au chombo cha Propaganda cha Rais. Tafadhali jirekebisheni.
Linaitwa zawadi za raisMilioni 20 aliyoitoa ni sehemu ya kodi tunazolipa hivyo sio vibaya tukipewa taarifa. Kama sijakosea bwana mkubwa analo fungu la mengineyo ambalo kwa mwezi linafika shilingi milioni 100.
Kwa hiyo wakifanya upupu tukae kimya kwa kuwa zama zimebadilika? Watu wote wakianza kula kinyesi cha ng'ombe bado sintakula, maana wewe unadokeza utakula.Acheni watu wafanye kazi zao
zama zinabadilika msikariri
Hehehehehe! Kazi ipo.Rais kunywa cha na Traffic !!