Selwa
JF-Expert Member
- Dec 17, 2010
- 671
- 707
Kuna rafiki yangu mmoja najaribu kumpa mawazo ya hapa na pale ila inakuwa ngumu. Hadithi yake inaenda hivi, alikuwa na mwanamke mzuri sana ila akateleza kidogo na kujifurahisha nafsi na mwingine, mwanamke huyu baada ya kugundua akamvumilia ila shetani akamptia akarudia tena, ndipo mwanamke huyu akaondoka na kwenda kusikojulikana. (walikuwa wakiishi wote) basi wakapoteana na familia yake yule binti haikutaka kumwambia yupo wapi yule binti na alipotea kabisa kwa ramani. majuzi katika pita pita zetu tukamwona na akenda kumsalimia, alipata kazi Kenya akakaa huko kama mwaka na nusu ila mkataba ukaisha ndio karudi. Ila shida jamaa bado kamzimika sana yule mwanamke ila hajui hata aaenze wapi. Je mwanamke, unaweza kumrudia mwanaume aliekucheat zaidi ya mara moja akikuonesha anakupenda kweli.
Na pia, jamaa alishatoa mahari kwa mwanamke mwingine alipokataa tamaa kumtafuta yule binti ila roho yake inakataaa baada ya kuonana tena na huyo ex wake. Afanyaje?
Na pia, jamaa alishatoa mahari kwa mwanamke mwingine alipokataa tamaa kumtafuta yule binti ila roho yake inakataaa baada ya kuonana tena na huyo ex wake. Afanyaje?