Kurudia mtihani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kurudia mtihani

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Wababa, Dec 24, 2011.

 1. W

  Wababa Senior Member

  #1
  Dec 24, 2011
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 159
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nisaidieni waungwana, nina D moja tuu ya form iv, na nimemaliza mwaka elfu mbili na nne, nataka nirisit masomo matano, jaman ntaweza kuyahimili kweli wkt nafanya na kazi??
   
 2. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,029
  Likes Received: 868
  Trophy Points: 280
  Mhm...!!jiangalie kwanza kichwa chako kina uwezo gan mkuu!
   
 3. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #3
  Dec 24, 2011
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 5,988
  Likes Received: 20,391
  Trophy Points: 280
  Hakuna kinachoshindikana kama hali na nafasi vinakulazimu kufanya hivyo, kikubwa hapa ni kuhakikisha unachagua masomo ambayo una hakika utaweza kuyaelewa vizuri unapofundishwa, yapo madarasa ya watu wa QT yanaweza kukusaidia sana kufanikisha malengo yako.

  Unahitaji kutenga muda na kutumia muda wako na saikolojia yako uiweke kiuanafunzi ili uweze kujisomea na kujichanganya kwa walio karibu wanaoweza kukusaidia kufuta hayo matokeo mabovu uliyopata.
  Kama umeamua unaweza, ondoa hofu
   
 4. W

  Wababa Senior Member

  #4
  Dec 24, 2011
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 159
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Thax m2 wangu obe, ubarikiwe kwa kunijaza matumaini, i hope nitakomaa na nitaweza tuu
   
 5. Kijuche

  Kijuche JF-Expert Member

  #5
  Dec 25, 2011
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 419
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Pia jaribu kufuatilia kiundani pale baraza la mitihani au kwa wadau wengine wa elimu ni masomo mangapi unatakiwa kuchukua wakati wa kureseat maana kama nilisikia kwa watu(informal source) kwamba kwa sasa inabidi urudie masomo yasiyopungua saba na uhahikishe unapata credit 3 at the same sitting sio zile za kuungaunga tena. Wadau wengine watakujuza zaidi juu ya hili..
   
 6. W

  Wababa Senior Member

  #6
  Dec 25, 2011
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 159
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Thanx kijuche ndugu yangu, naombeni wadau wengine mnijulishe naweza rudia mitihani mitatu ambayo nakuwa na uhakika nayo au mpk nirudie hiyo mitihani saba??? Nijuzeni pls.
   
 7. aikaruwa1983

  aikaruwa1983 JF-Expert Member

  #7
  Dec 25, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 1,362
  Likes Received: 1,189
  Trophy Points: 280
  kwa muda uliokaa home baraza la mitihani linakutambua wewe kama babu au bibi sasa mchakato uko hivi unatakiwa uanze mwakani 2012 form one na two yaani QT then form three and four 2013 utapiga tena pepa ya four.!!!!! utu uzima dawa komaa ndugu then neshino sevis inakusubiri sasa naamini elimu haina mwisho..................
   
 8. W

  Wababa Senior Member

  #8
  Dec 25, 2011
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 159
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  cyo ushauri niliokuwa nataka, u show how stupid you are!!
   
 9. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #9
  Dec 26, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,640
  Likes Received: 2,000
  Trophy Points: 280
  mimi ni mwenzako,niko kazini...ninafamilia ya watoto 2,nilimaliza fIV 1998 na D ya Kiswahili na D ya Siasa tu.
  2010 nilirudia necta nikapata div.III. Hapa nilipo nimeanza kujisomea masomo ya fV. & VI comb.PCB, nitafanya mtihani 2013. Nimelazimika kuandika yote haya ili nikutoe wasiwasi kuhusu kufanya mtihani kama private candidate.
  Naamini utaweza sana kama una nia. Kuna 'mitego' ambayo wengi wa watahiniwa huwanasa.....ukipenda ni PM.
   
 10. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #10
  Dec 26, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kwa kifupi ulipata daraja 0,katika kusoma ni vigumu kupata daraja la kwanza na daraja 0,mkuu mimi siwezi kukuficha na wala siwezi kuzunguka mbuyu!uwezo wako ni mdogo,kama unataka kurudi vitani ni lazima ufanye utafiti yakinifu ili kujua udhaifi wako ili uweze kukabiliana na changamoto za sasa!kwa kifupi una kazi nzito na unapaswa ujitahidi sana!
   
 11. G

  Geka Senior Member

  #11
  Dec 26, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  @Ndebile, nikupongeze kwa jitihada ulizofanya, binafsi nilimaliza mbele yako na nikabahatika kusoma A-levo Ndanda, kutokana na hili, ningependa kutoa ushauri wangu kidogo kuhusu wewe kusoma masomo ya Adv sec, vipi kama ungejiunga na masomo ya chuo ngazi ya cheti, then mwaka unaofuata unajiunga na stashahada. Wakati mwingine (kutokana na umri) kwenda masomo ya A level ni kupoteza muda mwingi shuleni.

  Hata hivyo kupanga ni kuchagua, na nilijaribu kutoa maoni yangu kuhusu hili, Boxing day njema
   
 12. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #12
  Dec 26, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,640
  Likes Received: 2,000
  Trophy Points: 280
  nikuulize swali TUKUTUKU: ukimwambia rafiki yako kuhusu biashara unayotaka kuanzisha akajibu hivi 'biashara yako itakufa mapema sana,utafilisika na nyumba yako utaiuza na utarudi kijijini, na huko kijijini watakucheka sana...'utajisikiaje? Uzuri wa watu wanaokatisha tamaa wenzao nao pia hawawezi kuthubutu katika kila jambo...nao pia wamekata tamaa...!
   
 13. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #13
  Dec 26, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,640
  Likes Received: 2,000
  Trophy Points: 280
  nashukuru kwa ushauri wako lakini hebu fikiria,age 37 niweke diploma miaka mitatu,degree miaka mitano...nafikiria kusoma Vet.medicine....kumbuka ninabadiri profession. Nadhani njia hii ya A-level ni fupi kidogo au unasemaje.

  Nawe pia nakutakia boxing day njema.
   
 14. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #14
  Dec 26, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,029
  Likes Received: 868
  Trophy Points: 280
  mkuu,co kwamba nakukatsha tamaa bt kiukweli,umri umesonga sana,ni vzr ungesoma kozi fupi fupi kama uhasibu nk.lakn huko unakokutaka ni parefu na pagumu sana.
   
 15. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #15
  Dec 26, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,640
  Likes Received: 2,000
  Trophy Points: 280
  Naturally napenda mambo magumu sijuhi kwa nini? Kama ningekuwa nawahi ajira,nadhani hapo ningekubali lakini tayari ninayo ajira ya kudumu kilichobaki ni kutimiza ndoto yangu. Uhasibu bwana ha!kujiajiri ni ngumu....napenda wanyama.
   
 16. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #16
  Dec 26, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,029
  Likes Received: 868
  Trophy Points: 280
  anway,mafanikio mema mkuu!
   
 17. aikaruwa1983

  aikaruwa1983 JF-Expert Member

  #17
  Dec 26, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 1,362
  Likes Received: 1,189
  Trophy Points: 280
  kwa fikra hzi hata QT huchomoki.......kimtindo nenda VETA kasome mapishi..
   
 18. W

  Wababa Senior Member

  #18
  Dec 26, 2011
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 159
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  poa m2 wangu, i hope nitaweza, cause nimepania kuweza.
   
 19. W

  Wababa Senior Member

  #19
  Dec 26, 2011
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 159
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na kwa anayeweza kunifahamisha, ninaweza kurudia hata masomo ma 4, au system ilipo ni kurudia yote?? Pls nisaidieni hapo ndugu zanguni
   
 20. G

  Geka Senior Member

  #20
  Dec 26, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  @Wababa, utaratibu wa sasa wa NECTA kuresit, lazima urudie na ufanye masomo saba, na kumbuka pia, mitalaa ya O-level imebadilishwa, kwa hiyo wala usiobabaike na hii kitu, bado QT inasaidia sana, binafsi, nilikuwa nikiwafundisha wafanyakazi wa ngazi tendaji chuo fulani hapa jijini, ni watu wazima sana na wana majukumu ya kifamilia na ndoa, hawa nilikuwa nakutana nao wakishatoka madarasa ya QT na ninakuwa nafanya brushing tu, zaidi ni kuwa na utayari na huu mwaka tunaoenda kuukaribisha unaweza kuwa ni mwaka wako wa baraka na mafanikio[​IMG]
   
Loading...