Sabayi
JF-Expert Member
- Dec 4, 2010
- 2,310
- 991
Wana-forum, nimefanikiwa kununua trector MF 565, ipo kwenye hali nzuri, ningependa niwekeze kwenye mashamba ya kukodi, na kwa vile ninazo accessories za kutosha kwa kuanzia kama, Boom Sprayer, Planter, Disc Harrow, Sub soiler, weed Cultivator na Water Pumps za nguvu, ningependa niwekeze kwenye kilimo cha mahindi, maharage, vitunguu, Karanga na ufuta. Shida kubwa niliyo nayo ni jinsi ya kupata mashamba ya kukodisha of course used, sio ya kuvunja, japo hata kama nikipata ya kuvunja kwa garama nafuu kwenye Potential areas zenye mvua za kutosha na mito ya kutosha kama vle Morogro ili niweze kuvuna maji ningefurahi sana, tatizo kubwa sijui wapi nitapata haya mashamba hata kam nikuanzia eka (70m) au Hecta (100m), 20 - 500 ekas / hectas, nitajitahidi niweze kutumia vifaa vya kilimo nilivyo navyo, na kama mnavyoona ninajitahidi sana kuondokana na kutegemea human lobour kwani kwa maisha ya leo Human labour imekuwa ya ghali sana. Jamani naombeni mawazo yenu. Natanguliza shukrani zangu za awali.
Kuna thread moja humu ina title Mwekezaji anatafuta shamba ukiipitia kwa makini utajua wapi pa kupata mashamba au mpm mtu anaitwa Doltye (sina uhakika na spelling) yumo kwenye hiyo thread atakusaidia