Kurekebisha fomu ya mkopo 2016/2017

Felix Aweda

JF-Expert Member
Jun 23, 2012
504
143
Habari za mda huu wanajamii
Naombeni msaada Wataalamu wa IT walioko humu. Jana nilijaza fomu ya bodi ya mikopo sasa kuna sehemu ya wilaya nilikosea kujaza. Badala ya kuandika wilaya ya Ngorongoro nilijikuta nimeandika wilaya ya Arusha.

Tofauti na mwaka jana, mwaka huu hakuna sehemu ya kufanya marekebisho. Nilihangaika sana lakini sioni. HESLB mwaka huu wanachofanya ni kuwa utafanya marekebisho tu kabla haujaprint. Ukisha print hakuna sehemu ya kuedit. Maana hapa ninapo ongea fomu nisha print.

Kwa Unyenyekevu mkubwa naombeni msaada kama kuna mtu alishakutana na mambo kama haya.

Mchango wa kilamoja utaheshimiwa.
 
Hiyo form huwezi kuedit isipokuwa mtu au mfanyakazi wa HELSB anayeshughulikia matatizo. Kwa wewe mwombaji baada ya kusevu system haiwezi kukuruhusu kufanya changes zozote na hiyo ni kwa sababu za kiusalama.
Chakufanya nenda HELSB watakutatulia tatizo hilo.
 
Ahsante mkuu. Nipo Ngorongoro na HESLB wapo Dar ndo tatizo kufika Dar.
 
Hiyo hujakosea Sana,haina effect Sana ila pia lazima ifanyiwe mabadiliko.

Kuna Jamaa aliwapigia wakamwambia kuwa kama endapo utakuwa umekosea sehemu basi andika barua na uambatanishe siku unatuma hayo maombi yako ukionyesha haswa mahali ambapo kosa limefanyika. Kila kitu kitaenda vema.

Huwezi kufanya corrections zozote. Kila la kheri!

Kwa maelezo zaidi fatilia Uzi huu
HESLB yatangaza kupokea maombi 2016/2017
 
Hiyo hujakosea Sana,haina effect Sana ila pia lazima ifanyiwe mabadiliko.

Kuna Jamaa aliwapigia wakamwambia kuwa kama endapo utakuwa umekosea sehemu basi andika barua na uambatanishe siku unatuma hayo mamombi yako ukionyesha haswa mahali ambapo kosa limefanyika. Kila kitu kitaenda vema.

Huwezi kufanya corrections zozote. Kila la kheri!

Kwa maelezo zaidi fatilia Uzi huu
HESLB yatangaza kupokea maombi 2016/2017
Ahsante mkuu. Nitaandika barua tu.
 
Mimi form yang ktk kipengele cha shule uliyo soma o_level imeniandikia new school ila namba niliyo fanyiga mtihani imekuja kama kawaida sasa nilipo mwambia aliye ni Downloadia hiyo form kaniambia Eti labda shule hiyo wanaitambua hivo na akasema kama ingekuwa imekosewa basi nomber isinge kuja wala jina. Wana jf hivi hili tatizo nifanyeje? Msaada
 
Hvi wadau no city gani vya kua navyo wakati WA kujaza fomu online bodi ya mikopo na namba ya fomu six ya mtihani mwaka huu inahitajika
 
Back
Top Bottom