Kurasa za Mark Zuckerberg zimedukuliwa

Francis Mawere

JF-Expert Member
Nov 17, 2015
958
830
Kurasa za mitandao za kijamii za bwenyenye mwanzilishi wa Facebook Mark Zuckerberg zimedukuliwa.

Kurasa za mtandao wa Instagram, Twitter, LinkedIn na ule wa Pinterest zilidukuliwa na kutekwa kwa muda siku ya jumapili kabla ya wataalamu wa usalama wa mitandao kumudu kuzidhibiti saa chache baadaye.

Kundi la wadukuzi la Ourmine limedai kudukua akaunti za Zuckerberg.

Kundi hilo lilijidai kwenye ujumbe waliochapisha kwenye mtandao wa Twitter kuwa ndio waliodukua kurasa hizo na wakamtaka

Zuckerberg awatumie ujumbe wa moja kwa moja iwapo alikuwa anataka umiliki wa akaunti hizo.

"Vipi @finkd tumedukua kurasa zako za Twitter , Instagram, Pinterest, tupigie iwapo unataka tukurudishie''
160606095910_mark-zuckerberg-twitter-hack.jpg

Ujumbe huo hata hivyo umefutwa kwa sasa.

Japo anaimiliki ukurasa huo Zuckerberg hajachapisha ujumbe wowote tangu mwaka wa 2012.

Mbunifu Ben Hall alichapisha picha ya ukurasa wa bwana Zuckerberg wa Pinterest uliodukuliwa.

BBC inafahamu kuwa muundo wa usalama wa kampuni ya Facebook ndiyo iliyowazuia wadukuzi hao kuteka ukurasa wake wa Instagram.

Mtandao huo wa kijamii unaotumika kuchapisha picha unamilikiwa na Facebook.

Wandani wa maswala ya usalama wa mitandao ya Intaneti wanadai kuwa huenda udukuzi wa mwaka wa 2012 wa ukurasa wake wa LinkedIn ndio uliochangia tukio hilo la jana.

BBC imeripoti.
 
Hawa BBC nao na Kiswahili chao cha Google translate wanajishushia hadhi sana. Hivi hakuna waandishi wanaojua vizuri Kiswahili hapo BBC Swahili hadi mhangaike kubadili habari kutoka Kiingereza?
 
Hawa BBC nao na Kiswahili chao cha Google translate wanajishushia hadhi sana. Hivi hakuna waandishi wanaojua vizuri Kiswahili hapo BBC Swahili hadi mhangaike kubadili habari kutoka Kiingereza?
haswaa hili ni jambo la mbolea!
 
Hawa BBC nao na Kiswahili chao cha Google translate wanajishushia hadhi sana. Hivi hakuna waandishi wanaojua vizuri Kiswahili hapo BBC Swahili hadi mhangaike kubadili habari kutoka Kiingereza?
hata mimi nililiona hilo siku nyingi nikawa najua inawezekana mm ndio sijui lugha ya kiswahili au wanaoandika sio wazungumzaji wa kiswahili.
Hawa jamaa habari zao hazielewekii.
 
Kumbe inawezekana ngoja ni hack a/c zake za banks..hebu nikumbushen tena hiv anatumia bank gan crdb au mkombozi?
 
hata mimi nililiona hilo siku nyingi nikawa najua inawezekana mm ndio sijui lugha ya kiswahili au wanaoandika sio wazungumzaji wa kiswahili.
Hawa jamaa habari zao hazielewekii.
Unajua Kiswahili kilichotokana na kubadilisha
lugha kinajulikana tu. Hakieleweki kabisa. Sasa nashangaa sijui kuna umuhimu gani wa kuajiri waandishi kutoka Tanzania halafu habari hawatumiki kuziandika. Wazungu watu wa ajabu sana.
 
Back
Top Bottom