Anaandika Green Osward
_
Uchaguzi mkuu nchini Ghana unaendelea muda huu. Rais aliyepo madarakani bwana "Nana Kufo Ado" kushoto aachuana vikali na hasimu wake wa siku zote bwana "John Mahama" kulia.
View attachment 1644596
Ikumbukwe hawa watu wamekutana kwenye kinyang'anyiro cha Urais wa Ghana mara mbili, hii ya leo mi mara ya tatu. Na katika vipindi walivyokutana kila mmoja kashinda mara moja. Yaani kwa kifupi hawa wote walishawahi kuwa ma Rais wa Ghana wakiachiana ofisi.
Mwaka 2012 walichuana kwa mara ya kwanza na John Mahama akashinda kwa kupata 50% na Nana Akufo-Ado akapata 47%. Mwaka 2016 wakachuana kwa mara ya pili ambapo John Mahama akaangushwa kwa kupata 44% na mpinzani wake Nana Akufo-Ado akapata 53%. Sasa wanachuana tena kwa mara ya tatu.
Linapokuja swala la utawala bora na demokrasia, Ghana ni mama wa demokrasia barani Afrima. Tume yao ya uchaguzi haifungamani na chama chochote cha siasa. Dola huwa haifanyi kazi ya kumbeba aliye madarakani. Kwanza sidhani kama dola ina muda huo mchafu.
Matokeo ya urais yatatangazwa saa 72 baada ya kumalizika zoezi la upigaji kura. Wapiga kura wanaruhusiwa kubaki vituoni (umbali wa mita 50) wakisubiri matokeo. Ikumbukwe Ghana, Rais huwa anatawala kwa miaka minne.
Kipindi chote cha kampeni, hakuna aliyezuiwa kufanya kampeni wala kupigwa mabomu ya machozi. Hakukuwa vitisho vya polisi wala usalama wa taifa. Waliotaka kuandamana waliandamana kwa amani na kulindwa na polisi. Hakuna media zilizofungiwa kwa kuwapa airtime wapinzani. Kwa kifupi kmpeni zilikuwa safi zaidi ya "skin tight" za wadada wa salon.
Nchi nyingi za Afrika zina mengi ya kujifunza kutoka Ghana, hasa kuhusu utawala bora na demokrasia. Ikumbukwe mpaka sasa hakuna mtu mwenye uhakika wa kushinda kati ya Rais aliyemaliza muda wake bwana "Nana Akufo-Ado au John Mahama. Hatima yao itaamuliwa na wananchi kupitia masanduku ya kura, na sio vyombo vya dola.
Mwitikio wa watu kwenye kupiga kura ni mkubwa sana. Mungu awavushe salama watu wa Ghana wanapotekeleza haki yao kikatiba.!
Follow @greenosward @greenosward @greenosward