Uchaguzi mkuu tunawapigia kura madiwani, wabunge na raisi. Baada ya kupiga kura zinahesabiwa na matokeo ya kura za udiwani, ubunge na uraisi yanabandikwa kwenye kituo husika, Yale ya udiwani yanajumlishwa kwa ngazi ya kata na mshindi hutangazwa papo hapo kuwa diwani. Ya ngazi ya ubunge yanajumlishwa kwa ngazi ya Jimbo na mshindi hutangazwa papo hapo kuwa mbunge wa Jimbo husika, ni za raisi tu ndio hutangazwa tume makao makuu.
Sasa najiuliza juu ya muundo ya huo mfumo wa wizi kwa ngazi ya Jimbo na kata upoje kupitia hiyo combination ya NEC+NIDA+CCM? Au hapo wahuni hawana interest kabisa kwa ngazi ya madiwani na wabunge?
Sasa najiuliza juu ya muundo ya huo mfumo wa wizi kwa ngazi ya Jimbo na kata upoje kupitia hiyo combination ya NEC+NIDA+CCM? Au hapo wahuni hawana interest kabisa kwa ngazi ya madiwani na wabunge?