Kura zenu ni muhimu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kura zenu ni muhimu

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Ngambo Ngali, Sep 24, 2010.

 1. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Hodi Hodi Jamvini, Malenga na wasomaji,
  Tafadhali tambueni, tumeupata mtaji,
  Tunakuja uwanjani, jengo tunalihitaji,
  Kura zenu ni muhimu, ili kuwa wapangaji.

  Timu imekamilika, kila idara yatosha,
  Slaa tumemsimika, kamwe hatotuangusha
  Sera amezitamka, Mtanzania kuneemesha,
  Kura zenu ni Muhimu, ili kuwa wapangaji

  Kazunguka mikoani, sera kuelezea,
  Watoto madarasani, vyuoni na chekechea
  Kulipia asilani, shule bure kupatia
  Kura zenu ni Muhimu, ili kuwa wapangaji

  Wafanyakazi kakumbuka, kilio chao cha kale
  Mishahara kufutuka, kuwafanya watoto wale
  Chochote wakikumbuka, mifukoni ziko hela
  Kura zenu ni Muhimu, ili kuwa wapangaji

  Timu haijatimia,jengoni kumsindikiza
  Baregu anafuatia, uzushi kuudamaza,
  Mabere afuatilia, sheria kuwaeleza
  Kura zenu ni Muhimu, ili kuwa wapangaji

  Zitto pia Ndesamburo, wote wanaunguruma,.
  Halima pia Mbogoro, kidete wamesimama,
  CCM wana Kihoro, wamuonapo Lema,
  Kura zenu ni Muhimu, ili kuwa wapangaji.

  Nimtaje naye Mbowe, Mbilinyi jimbo la Mbeya,
  Na anatamba Shamwee, kule Vijijini Mbeya,
  Waonekanapo mayowe, Nisemacho si umbea,
  Kura zenu ni Muhimu, ili kuwa wapangaji.

  Swali sasa ni lako, wewe unisomaye,
  Ulanga na Makambako, Hassani, Pili, Simbeye,
  Muhimu ni kura yako, wa CHADEMA umpendaye,
  Kura zenu ni Muhimu, ili kuwa wapangaji.

  Kura peke haitoshi, Kuzilinda ni lazima,
  Bukoba Lindi na Moshi, kura kuzitazama,
  Itamaliza ubishi, itasimama CHADEMA,
  Kura zenu ni Muhimu, ili kuwa wapangaji.

  Kwa wingi tujitokeze, Pasi kudai ujira,
  Watoto wajane wazee, kuzilinda zetu kura,
  Mtatufanya tuweze, kupata kilicho bora,
  Kura zenu ni Muhimu, ili kuwa wapangaji.
   
Loading...