Kura za Maoni UKAWA tayari imeshinda

Kura za Maoni UKAWA tayari imeshinda

Mwiba

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
7,607
Reaction score
1,764
Huhitaji REDET au sijui akina nani wanaotutangazia mshindi ni nani ,kwa kadiri nilivyozunguuka Tanzania nzima katika kipindi kifupi cha mwezi uliopita ,uchunguzi binafsi tena wa kienyeji kabisa ,kama UKAWA watampata Lowasa basi njia ya IKULU ni nyeupe ,hayo ni maneno niliyokuwa nayasikia kila penye kijiwe iwe cha wazee au vijana.

Kuna niliowasikia wakisema chama chetu kimepata jembe na kama hili jembe hawakulipitisha basi tumefungwa bao la kisigino ,wakati huo Lowasa anaitafuta njia ya IKULU kupitia CCM na matarajio ya wana CCM wengi walikuwa wameshamchagua Lowasa wanasubiri siku ya kupiga kura tu ,ila chaguo lao limepigwa na chini ,upigwaji chini kwa Mheshimiwa Lowassa ulitarajiwa na walio ndani ya siasa za CCM kwani si mara zote CCM humchagua yule ambae watu wanamuhitaji,tarehe zinaonyesha hivyo na hata vurugu zimewahi kuzuka kwa wanachama wa ccm kupelekewa mtu ambae si chaguo lao kwani NEC ya CCM si mtu wao ,mara hii CCM wamecheza mchezo ambao utawagharimu katika ngazi ya Uraisi kumpeleka Pombe wakati sio chaguo la ccm walio wengi.

Sasa chunguza huko mitaani katika vijiwe na vigenge bila ya kutegemea mashirika ya udaku utaona Lowasa aka UKAWA wanaongoza kwa kilomita nyingi dhidi ya Pombe aka CCM.
 
Ni Dar tu au nchi nzima?

Nchi nzima nzima kwenye miji mikuu ndio usiseme ,utamzikia mwanachama wa CCM akisema NEC wamenitibua na kunivuluga kabisa sijui niludishe kadi au nitoke chama....yaani huelewi anasema nini.Mambo kwa chama cha CCM ni magumu zaidi ya unavyofikiria.
 
sidhani kama kuna kijana yeyote kama mimi hatampa kura lowasa. Lowasa Ashashinda.
 
Back
Top Bottom