Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,553
- 4,013
Wakuu
Mambo yanaonekana kuwa si shwari huko ndani ya Chama Cha Mapinduzi kama tunavyoaminishwa
Siku ya leo wanakijiji wa Mtaa wa Viwandani, Kata ya Unga Limited, wameonyesha kutoridhishwa na uamuzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa kumpitisha Rasuli Mshana kwenye kura za maoni
WanaCCM hao wamesema kwamba hawatakubaliana na kumpa kura za Ndio Rasuli Mshana, aliyeshinda kura za maoni, ikiwa jina lake halitatolewa kama mgombea katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024.
Soma pia: Kigamboni: CCM wararuana wenyewe kwa wenyewe. Vurugu zapamba moto kwenye Uchaguzi wa ndani ya chama
Makada hao walisema kuwa mgombea aliyepitishwa sio chaguo lao kwa kuwa hawamfahamu badala yake walikuwa wanamtaka mgombea anayeitwa Richard Mbwambo ambaye ndio walikuwa wanamtaka.
Katika kueleza hisia zao, makada hao walifanya maandamano kuelekea ofisi za CCM Arusha Mjini.
Kwa hiyo kumbe wanaCCM wanaruhusiwa kuandamana kama hawajapenda matokeo ya uchaguzi lakini upinzani wametishiwa kutokuandamana iwapo hawatakubaliana na matokeo ya Uchaguzi wa Serikali za mitaa kama alivyosema Albert Chalamila?
Soma pia: Chalamila aliagiza Jeshi La Polisi kuwashughulikia wananchi watakaopinga matokeo ya Uchaguzi ujao wa Serikali Za Mitaa
Nini kinaendelea huko CCM?