multmandalin
JF-Expert Member
- Sep 8, 2012
- 2,030
- 576
CCM wanazidi kupoteza kura. Kwa bahati mbaya wanazitafuta CDM. Wanatumia polisi wenye bunduki na mabomu, wanapekua kila ofisi ya CDM na kwenye nyumba za viongozi wa CDM wakizitafuta kura zao. Masikini CCM!!! Laiti wangejua kuwa kura zao hazipo CDM...
Zifuatazo ni baadhi ya sehemu ambako kura za CCM zimepotelea, nawashauri waende huko wakazitafute...
1. Maelfu ya kura za CCM yamepotelea kwa wafugaji wa kimasai na kibarbeig, ambao wamenyang'anywa ardhi yao kule Loliondo akapewa mwarabu, na walipojitahidi kujihifadhi sehemu nyingine kama wakimbizi tunashuhudia wakiondolewa bila huruma kule Korogwe, Ihefu na Rufiji...
2. Maelfu ya kura za CCM yamepotelea Mtwara, ambapo wakazi wake wanalilia raslimali ya gesi iwafaidishe, lakini wameishia kuvuliwa nguo, kuchapwa viboko na kuuawa...
3. Kura za CCM zimepotea kwa maelfu mikononi mwa wakulima wa korosho, ambao walilaghaiwa kuuza kwa stakabadhi ghalani, wakaishia kuliwa...
4. Maelfu na maelfu ya kuza za CCM yamepotelea mikononi mwa wakulima wa pamba, ambao bei ya zao lao inazidi kuporomoka kutokana na CCM kubinafsisha kiholela na kuua viwanda vya nguo nchini na kisha kushindwa kuwatafutia bei nzuri kwingineko...
5. Makumi na mamia elfu ya kura za CCM yamepotelea mikononi mwa wanafunzi waliomaliza form 4, wazazi wao na jamaa zao ambao pamoja na kupoteza fedha na muda mwingi kugharamia elimu, wameishia kufeli kutokana na mazingira mabaya ya elimu...
6. Maelfu ya kura za CCM yamepotelea mikononi mwa wamachinga, ambao wanatumia nguvu na uwezo wao kujtafutia rizki, lakini kila siku wananyanyaswa na mgambo...
7. Kura za CCM maelfu zimepotelea mikononi mwa wananchi wa kule Songea, kule Ifakara na kule Ngara ambao walishuhudia maisha ya wenzao yakikatizwa bila hatia na polisi wa CCM...
8. Kura za CCM zimepotelea mikononi mwa walimu ambao ambao wanadhulumiwa jasho lao, na walipojitahidi kuzidai hadharani wakaishia kukatazwa mahakamani na kutishiwa kufukuzwa kazi...
9. Maelfu ya kura CCM yamepotelea mikononi mwa madaktari ambai wanafanya kazi katika mazingira magumu na mishahara duni, na pale walipojaribu kudai, wakashuhudia mwenzao aking'olewa kucha na meno bila ganzi...
10. Kura za CCM zimepotelea mifukoni mwa wakulima, ambao hawana pembejeo, na pale wanapojitahidi na kupata mavuno kidogo mashamba yao hayafikiki kutokana na ubovu na kukosekana kwa barabara...
11. Kura za CCM zinazidi kipotelea mikononi mwa wanaotumia simu za mikononi, ambao pamoja na kulipa ghali kununua na kutumia simu, bado wanakamuliwa sh 12,000 kila mwaka kuchangia ununuzi wa mashangingi ya viongozi wa CCM, kugharamia matumizi kwenye nyumba ndogo zao na kusomesha watoto wao wavivu Ulaya...
Nawashashauri CCM waje huku nilikowatajia wakazitafute kura zao, tena hawana haja ya kuja na polisi wala mabomu. Zipo tu. Wajue kwamba hata wapekue kwa miaka 10, hawataikuta kura yao hata moja kwenye ofisi za CDM wala nyumbani kwa viongozi wao, kwani hazipo kule. Tunazo sisi humu mtaanii....
I hear the voice saying talk to them talk to them, This is the voice people must listen to.
In that thinking it is real nyinyiem don't get onto JF! But if they get onto it hawana king'amuzi.
These are Da Vinci codes.