Dr. P.W. Slaa na Mr. Zito Z. Kabwe ni wanasiasa mashuhuri hapa nchini.
Pamoja na kuwa Zito ana kasoro zake nyingi tu, bado ni kijana anayeuzika sana kwenye siasa za Tanzania. Ameshajijenga vizuri sana. Kuna siku alimbeza mwenzake Tundu Lissu bungeni, nikaona kuwa huyu jamaa kumbe kweli anatakiwa aekue kidogo. Sometimes busara zinaongezeka kulingana na muda.
Kama Zito kabwe atampisha Dr. W.P. Slaa agombee uraisi uchaguzi wa mwaka 2015 na kumfanyia kampeni ya dhati, CHADEMA itafanya vizuri sana kwenye uchaguzi. Lakini kukiwa na kutofautiana kati ya Zito na Slaa, basi CHADEMA inaweza ikakosa mafanikio kwenye uchaguzi wa mwaka 2015. Matokeo ya mwaka 2015 yatachangia sana matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2020.
Napendekeza, Dr. Slaa aachiwe agombee mwaka 2015 na baada ya hapo akiwa raisi aongoze kwa miaka mitano tu, amuachie Zito, akikosa astaafu siasa, ataheshimika sana kisiasa hapa Tanzania kuliko wale ambao wanasema wamestaafu alafu baada ya muda mfupi wanarudi. Zito pia anatakiwa amrudishe David Kafulila CHADEMA ili washirikiane kuhakikisha Kigoma inakuwa ngome muhimu ya CHADEMA.

Slaa akiwa rais sidhani kama atakubali kuongoza miaka 5 tu! ninavyo mjua na anavyopenda Uongozi huenda akataka kubadili hata na katiba ili aendelee kukaa madarakani! haya tumeyaona huko Senegal pale Wade alipotaka kubadilisha katiba na hata Zambia mpinzani Chiluba alipoukwaa Urais nae alitaka kubadili katiba!
zitto atapata kura nyingi akigombea urais kuliko slaa,Slaa ni mzee kwa sasa.
Ujana wake nayo ni sifa? kwani ukiwa mzee huwezi kuwa rais?
sababu za kuto mchagua Zitto Kabwe
1. hana sifa ya kugombea urais coz hajatimiza umri unaotakiwa na sheria
2. hana sifa ya kugombea coz ana uchu wa madaraka
3. hana sifa ya kugombea urais coz hana Busara na hekima
4. hana sifa ya kugombea coz anatumiwa na ccm
Tuache kelele nyingi, kama ungepewa mamlaka ya kumteua kati ya Zitto Zuberi Kabwe ama Wilbroad Peter Slaa kugombea nafasi ya urais mwaka 2015. Ni nani ungemteua? Na Kwa Nini? Toa sababu kuu nne TU.