Baada ya miaka hamsini ya muungano ambao una serikali mbili ya muungano na ya zanzibar basi sasa ni wakati muafaka kupitia katiba mpya kurekebisha kidogo style ya serikali, kuwepo na serikali mbili lakini ziwe ya tanganyika na ya muungano hapo ndo kero zote za muungano zitaisha.
Kumekuwa na wanaotaka serikali moja, mbili na tatu lakini hizi serikali hazitafanikiwa kama Watanzania wengi wamechoka muungano na wanataka tuwe na nchi mbili tofauti. Je leo hii tukiweka kwenye kura za maoni kama Watanzania wanataka muungano mimi naona kama Watanzania wengi watachagua muungano ufe kwani Wabara wengi wanaona wanatumiwa tu na Wanzanzibar wengi wanaona watapata faida zaidi bila muungano. Tatizo kubwa sana ni viongozi wa Zanzibar kwasababu ndiyo wanaonufaika na muungano kuliko kikundi kingine chochote na wnasingizia muungano kwa utendaji kazi wao duni.Pesa yote inaishia kuwatunza viongozi Zanzibar
Ardhi ya serikali ya muungano ni hipi kwa sasa?kumbuka Zanzibar wana Ardhi yaoSerikali 2 ndo mpango mzima! Tukiendekeza 3 Serikali ya Muungano itakuwa haina hata ardhi (ardhi si suala la Muungano) na itakuwa ombaomba kwa nchi washirika kwa kuwa haina vyanzo vya mapato vya kwake!
Na kura yenyewe iwe SIRIWAZIhakuna muafaka kwenye hili tusidanganyane. suluhisho ni wananchi wa pande 2 kupiga kura. Kwanza muungano wanautaka?
Daaah mm naona serikari mbili ndio nzuri
serkal 2 ili kuepusha kuvunja muungano siku za usoni