Kura ya kutokuwa na imani na serikali

Kura ya kutokuwa na imani na serikali

MWANA WA UFALME

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2010
Posts
578
Reaction score
144
Kwa mlolongo wa matukio yanayoendelea kwenye taifa la sasa ni dhahiri kuna udhaifu mkubwa kwenye serikali maana chochote wanachosema hawaaminiki tena,

Raisi haonekani kuonyesha msimamo thabiti juu ya kukemea maovu yanayoendelea kwenye taifa. Wanaofanya maasi dhidi ya upinzani (ambao serikali ndio mtuhumiwa wa kwanza) wanaachwa huru,

Waziri mkuu ametamka wazi wamechoka kazi, na wanachokifanya sasa ni kutoa kipigo tu kwa wananchi. Hii ni kauli inayotolewa na kiongozi mkuu kabisa wa serikali.

Taasisi nyeti kama jeshi la polic havionekani kuonyesha weledi wowote wa kazi zao na wamekuwa hatari kwa wanachi,

Taasisi za kimahakama hazioneshi kutenda tena haki, na rushwa ndio habari ya siku,

Kama serikali ni hatari kwa maisha ya wananchi na kuna hisia kwa asilimia kubwa inaendekeza sera kandamizi za mauaji yasiyo na sababu huku ikipambana kila kukicha kuingia mikataba kandamizi ya rasilimali za nchi,

Je ni wakati wa kufikiria uwezekano wa kura ya kutokuwa na imani na hii serikali?
Je utaratibu huu unaweza kuanza nje ya bunge?
 
hapa utaratibu wa uongozaji wananchi unapotoshwa mimi nadahani tufanye uchaguzi utakao weka mtu makini sio kiongozi anashindwa kutoa msimamo wa uongozi
 
Hata mama mzazi hakuwa na Imani na baba yake mwana wa ufalme
 
CCM vichwa vyao viko kama mabox matupu,kazi ya vichwa vyao ni kubebea nywele tu.
 
Bado miezi 16 cha kueleweka kitaeleweka. Mimi binafsi sina imani hata chembe na serikali hii. Naishi kwa masononeko makubwa. 2015, watanzania wanayo haki toshelevu ya kuikataa CCM na serikali yake kupitia sanduku la kura. Kinyume cha hapo sidhani kama fursa hiyo ipo. Sana sana, tutaendelea kupigwa na kuuwawa kama wanavyofanya.
 
Mbona hamjibu swali? Tunaweza kupiga kura ya maoni tukianzia nje ya Bunge? Wa nje tukiwa wengi inamaanisha na bunge watafuata.
 
Usiogope maana mungu ameshawakataa ufalme wa ccm umefitinika ni swala la damu tu.
 
Hili kwenye katiba hii iliyojaa viraka halimo, lakini kuna umuhimu mkubwa wa kuliweka hili katika katiba mpya. Kama lingekuwemo katika katiba ya sasa si ajabu DHAIFU angeshatoswa tangu 2007 pale alipoonyesha hana uwezo wa kuongoza nchi.
 
Tatizo wale wabunge wa CCM wakitishiwa nyau tu wote wanaunga mkono utawala uliopo. KURA upande wa CCM ni moja tu nayo ni ya DEO FILIKUNJOMBE.
 
Vipi kwani zile njia za Misri au Libya haziwezekani?
 
Siasa imeingiliwa viroboto,kila siku uzushi tu,chadema mtasubiri sana ila mtaishia patupu
 
Mimi nasikitishwa sana sana na kauli ya waziri mkuu labada atoe ufafanuzi lakini hata hivyo sitamwelewa tu kwa sababu watu wanakufa yeye anasema piga tu hivi kweli bado ana huruma kama zamani huyu au amekata tamaa na kuongoza? ok tumsamehe yeye tulie na serikali nzima yeye mungu ataangalia namna ya kumuadhibu.hii serikali ya mfano na kama kuna mahali inataka ikafanyiwe majaribio basi haifai na wala usihangaike na marekebisho haina cha kurekebisha bali kuitopa nzima nzima kama ilivyo
 
Kakiri amechoka, ila hajasema amechoshwa na kitu gani. pengine angeeleza kinachomchosa zaidi tungeweza kumshauri.
Kuchoka ni hali ya kawaida ya mtu kufanya kazi. Kama hataki kuchoka kwasababu ya kazi anaweza kuomba kupumzika maana halazimishwi
 
Tatizo wale wabunge wa CCM wakitishiwa nyau tu wote wanaunga mkono utawala uliopo. KURA upande wa CCM ni moja tu nayo ni ya DEO FILIKUNJOMBE.

Ndio maana nguvu toka nje ya bunge ni ya muhimu zaidi
 
Hili kwenye katiba hii iliyojaa viraka halimo, lakini kuna umuhimu mkubwa wa kuliweka hili katika katiba mpya. Kama lingekuwemo katika katiba ya sasa si ajabu DHAIFU angeshatoswa tangu 2007 pale alipoonyesha hana uwezo wa kuongoza nchi.

Pengine ni wakati wa kulifikiria tena
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Bado miezi 16 cha kueleweka kitaeleweka. Mimi binafsi sina imani hata chembe na serikali hii. Naishi kwa masononeko makubwa. 2015, watanzania wanayo haki toshelevu ya kuikataa CCM na serikali yake kupitia sanduku la kura. Kinyume cha hapo sidhani kama fursa hiyo ipo. Sana sana, tutaendelea kupigwa na kuuwawa kama wanavyofanya.

Mungu mkubwa, Pengine kwa neema zake anaweza kutupa mabadiliko hata kabla ya hapa, tuendelee kuomba, maana Mungu hamtupi mja wake
 
Wananchi tuiunge mkono kura hii maana serikali yetu ndio inatumaliza.
 
Kwa mlolongo wa matukio yanayoendelea kwenye taifa la sasa ni dhahiri kuna udhaifu mkubwa kwenye serikali maana chochote wanachosema hawaaminiki tena,

Raisi haonekani kuonyesha msimamo thabiti juu ya kukemea maovu yanayoendelea kwenye taifa. Wanaofanya maasi dhidi ya upinzani (ambao serikali ndio mtuhumiwa wa kwanza) wanaachwa huru,

Waziri mkuu ametamka wazi wamechoka kazi, na wanachokifanya sasa ni kutoa kipigo tu kwa wananchi. Hii ni kauli inayotolewa na kiongozi mkuu kabisa wa serikali.

Taasisi nyeti kama jeshi la polic havionekani kuonyesha weledi wowote wa kazi zao na wamekuwa hatari kwa wanachi,

Taasisi za kimahakama hazioneshi kutenda tena haki, na rushwa ndio habari ya siku,

Kama serikali ni hatari kwa maisha ya wananchi na kuna hisia kwa asilimia kubwa inaendekeza sera kandamizi za mauaji yasiyo na sababu huku ikipambana kila kukicha kuingia mikataba kandamizi ya rasilimali za nchi,

Je ni wakati wa kufikiria uwezekano wa kura ya kutokuwa na imani na hii serikali?
Je utaratibu huu unaweza kuanza nje ya bunge?
Kama wabunge wa CCM wangekuwa na mawazo ya aina hii basi wangeweza kufanya hivoy kupitia kura ya kupitisha nbajeti jioni hii. lakini sidhani kama hilo linaweza kutokea
 
Hizo pia zinawezekana lakini athari zake kwa nchi ni kubwa sana ikiwemo umwagaji wa damu na itachukua muda mrefu nchi kurudia pale ilipo kabla ya vurumai kama zile, lakini kura kama hii haina athari zozote kwa nchi zaidi ya kumwambia mhusika kazi ya kuiongoza nchi imekushinda kaa pembeni.

Back
Top Bottom