Kupuliza perfume/refreshner kwenye ndege

socialife

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
206
85
Hebu nisaidieni wenzangu, ukiwa unatoka mfano Africa kusini na ndege yao kuja Tz, wanapuliza kama perfume/air refreshner kwenye ndege wanadai according to international blah blah. Mie nafkiri wanatuona sie wachafu na vitu kama hivyo. Kuna mwenye maoni tofauti anijuze why only way back Tz?
 
Hilo mbona kawaida??mi nilisafiri kutoka london kwenda Istanbul na Turkish airline nao walipuliza...ni kuweka mazingira ya hewa nzuri mara baada ya abiria kupanda.
 
Hilo mbona kawaida??mi nilisafiri kutoka london kwenda Istanbul na Turkish airline nao walipuliza...ni kuweka mazingira ya hewa nzuri mara baada ya abiria kupanda.
Mi nimewahi safiri moscow kwenda instubul hiyo hiyo Turkish sijawahi ona,hata Qatar na fly emirates sijawahi ona
 
hiyo siyo perfume wala airfresher ni madawa maalum yanayopulizwa kwenye ndege ili kuua vijidudu hasa unaposafiri kutoka huku kwetu kwenda kwenye nchi za wenzetu ambazo hasa hazina Malaria.
 
hiyo siyo perfume wala airfresher ni madawa maalum yanayopulizwa kwenye ndege ili kuua vijidudu hasa unaposafiri kutoka huku kwetu kwenda kwenye nchi za wenzetu ambazo hasa hazina Malaria.

Mkuu hzo dawa zinawekwa kabla abiria hawajaingia au?
 
Mkuu hzo dawa zinawekwa kabla abiria hawajaingia au?

zinawekwa wakati abiria wote tayari wapo ndsni ya ndege hii ni kwa sababu hata wakiweka kabla abiria bado anaweza kuingi na mbu hata kwenye koti lake and something like that
 
hiyo siyo perfume wala airfresher ni madawa maalum yanayopulizwa kwenye ndege ili kuua vijidudu hasa unaposafiri kutoka huku kwetu kwenda kwenye nchi za wenzetu ambazo hasa hazina Malaria.

kwa hiyo wakipuliza ndio vimelea vya malaria vinakwisha au??unawafaham au unawasikia falciparam spp.....
 
Huku Yaeda tunapuliza hata bila kusafiri.......kusafiri kitu gani bana.......freshner walawala........
Hebu nipe uelekeo wa namna ya kufika huko Yaenda, hivi unapanda meli ziwa Tanganyika ndo inakufikisha huko?.
 
Mbona ni jambo la kawaida kabisa hilo....

Emirates wanapulizia....hali kadhalika British Airways, KLM, Lufthansa, na Delta.
 
Tunazo hata kwenye baiskeli zetu sembuse ndege.
Hilo si jambo la ajabu mkuu.

Wanataka abiria wote mnukie sawa msidolishiane harufu zenu.
 
Back
Top Bottom