Kupotelewa na nyaraka mbalimbali!..

Kupotelewa na nyaraka mbalimbali!..

Liwengi

Member
Joined
May 15, 2011
Posts
29
Reaction score
7
Watanzania wenzangu.

Mimi kwa jina halisi naitwa Bernard Bruno Mwenda

Ninapenda kuwajulisha Watanzania wenzangu kuwa, siku ya tarehe 9/11/2013 majira ya saa 12:30 jioni, nikiwa na usafiri wa pikipiki nikitokea Uwanja wa Ndege kuja Mwenge, nilidondosha begi. Begi hilo nilidondoshea kati ya Ubungo na Mlimani City. Katika begi hilo kulikuwa na vitu vingi sana ikiwa pamoja na nyaraka zangu mbalimbali.

Miongoni mwa nyaraka zilizokuwemo katika begi hilo ni:-


  1. Cheti cha Sekondari 1996
  2. Cheti cha JKT operation Kagera
  3. Cheti cha Polisi [Auxiliary Police] 2002
  4. Kadi ya Pikipiki T513 BZL na Road Licence pamoja na Kadi ya Bima.
  5. Kitambulisho cha Kazi
  6. Kitambulisho cha Uraia
  7. Kitambulisho cha Chuo TPSC
  8. Cheti cha shule ya msingi cha mototo wangu Melinda Mwenda
  9. Kitabu cha Biblia ndani yake kuna namba za simu za mke wangu
  10. Fedha Taslimu Laki moja na tisini elfu
  11. Modem mbili na Flash mbili
  12. Saa aina ya SEICO AUTOMATIC
  13. Na nyaraka nyingine mbalimbali na yote hivyo vina majina ya Bernard B. Mwenda au Mwenda B B

Tafadhali, anayeweza kuwa na taarifa ya vitu hivyo anipigie namba za simu 0714093091 au 0758227414. Tutaelewana baada ya kupata taarifa hizo.

Pia kwa mtu aliyeokota vifaa hivyo, tafadhali asiwe na shaka yoyote, anaweza kuchukua vyoye anavyovipenda katika begi hili ikiwa ni pamoja na pesa, isipokuwa aniachie document na vyeti vyangu. Mimi kwa sasa nimekwama sina ujanja kabisa.

Vifaa hivyo anaweza kuvipeleka kituo chochote cha Polisi au anipigie simu nilizoandika hapo juu.


Mtanzania mwenzenu, Bernard Bruno Mwenda
 
Dah pole sana Mwenda. Hope utavipata..
 
Asante sana Baba V, nasubiri tu muujiza wa Mungu!
 
Pole sana, najua umuhimu wa ivyo vitu kwako, kwanza next time jifunze uwe una scan copy ya vyeti vyako vyoote muhimu , plili hilo bag ulikuwa umefunga nyuma kwenye pikipik!? umebeba likadondoka usijue au ilkuwajekuwaje...?? eleza vizuri ili tupate mwanga wa kukushauri na kujaribu kuimagine jinsi tukio lilivyotokea ili tujue tunavipata vipi vitu vyako na maeneo gani!

ushauri cha kufanya kumbuka mara ya mwisho uliliona begi lako wapi, from there anza taratibu kutembelea majirani na barabara hasa masela wa vijiwe wanakuwaga wanadata sana wale,...shirikiana na jamaa yako yoyote akusaidie zoezi mmoja upande wa kulia wa barbara mmoja upande wa kushoto hata kama itakuwa wiki

Pia chapisha vitangazo vidogo vidog vyenye namba yako ya simu uwe unacha kwenye maduka na kwa watu wa vijiwe.

Kama kweli unahitaji ukitumia njia hii hakika utavipata...bag kubwa bwana!!
 
Pole sana. I hope alie kuokotea atampigia mke wako sim na kupanga nae namna ya kurudisha vyeti hivyo muhimu
 
Asante sana bwana syruss kwa ushauri wako mzuri. Nitalifanyia kazi wazo lako.
 
Niligundua kuwa begi sina baada ya kufika maeneo ya Mlimani City. Ubungo nilikuwa nalo ndiyo maana nimeandika kuwa lilidondoka kati ya Ubungo na Mlimani City.
 
Back
Top Bottom