kuporomoka maadili Vs maisha ya ndoa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kuporomoka maadili Vs maisha ya ndoa.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mbu, Aug 14, 2009.

 1. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #1
  Aug 14, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...Neno kuporomoka kwa maadili si neno geni masikioni mwa wengi.
  Ndoa nyingi za kisasa zimekuwa zinakumbwa na matatizo kiasi kuhatarisha maisha ya kizazi husika.

  Nani alaumiwe?

  Ni kosa la Wazazi, ambao ni taswira ya watoto?

  .... au ni maendeleo ya kisayansi na tekinolojia inayohusisha matumizi ya sinema, Interneti na simu za mkononi?

  ...au ni mapungufu ya imani, mila na desturi?

  ...huenda ni serikali na matokeo ya utandawazi pamoja na 'upofu' wa mila za kigeni?

  ...Jadili!
   
 2. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #2
  Aug 14, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  1.KULAUMU WAZAZI NI KUWAONEA.kumbuka kwa maisha ya sasa watu wengi wanapata influence ya maisha kutoka kwa watu wengine zaidi -hutumia muda mchache sana kuishi na wazazi.
  2.maendeleo ya kisayansi na tekinolojia - Huenda.Kwa maana kila kitu chema na kibaya vimerahisishwa.
  3.mapungufu ya imani, mila na desturi- haswa!watu hawana woga wa matokeo ya ubaya wafanyao.Hawaamini tena dini wala mila na desturi
   
 3. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #3
  Aug 14, 2009
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  life has changed for the worst-culpit ni WOMAN LIB-sasa hivi akina mama na haki zao wanacheza nje openly matokeo sparks fly and nothing is safe kuanzia ndoa hadi watoto
   
 4. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #4
  Aug 14, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  wazazi;
  Katika jamii nyingi za kileo, 'upofu' wa wazazi katika malezi unapelekea vijana kuamua kuishi kadri wazazi wao ama wanaowazunguka wanavyokubaliana nao. Kama mzazi anaona sawa bintiye kutoka na vivazi vya kudhalilisha, unadhani binti huyo atakubaliana na masharti ya mumewe kuhusu mavazi?

  mfano; Kama binti/kijana haulizwi wala kudhibitiwa kwao uhusianio wake na mpenzi/wapenzi wake (wengi) katika umri wao mdogo, unadhani itakuwaje kesho/keshokutwa atapofumaniwa na mwenza wake na kesi hiyo kupelekwa kwa hao wazazi?

  Sayansi, na teknolojia;
  Pamoja na mazuri ya sayansi na teknolojia, zamani kulikuwa na restrictions nini kinachofaa kuangaliwa na watu wa umri gani au jamii gani. Mnaokumbuka enzi zile Drive inn Cinema, Avalon, Empress, Newchox, Empire, Tivoli na Sapna (morogoro), Metropole Arsuha... sinema zilikuwa classified na huingii kama umri haukuruhusu! Urahisi wa upatikanaji tekinolojia kwa njia ya simu, internet, umepelekea vijana wengiu kujifunza mambo ambayo hapo awali yalikuwa mwiko kujifunza achilia mbali kutaka kuyajua. Hata sinema za kibongo siku hizi aaaaaah, mambo nje nje!

  Imani;
  wengi tunazaliwa either wakristo/waislamu/baniani, au singasinga.
  Ama kwa kukosa nafasi kutokana na msongo wa maisha au kukosa msisitizo toka kwa wazazi na jamii inayotuzunguka, Imekuwa ni nadra kusoma mafundisho ya vitabu na kufuata miongozo ya dini zetu jinsi ya kuishi kwa heri, heshima na taadhima. Kama una imani, na unaamini 'hukumu' basi utaogopa, na kujirudi. Kinyume na hapo, unakuta mtu anaponda mali tu kwa kudhani siku ya siku akishaungama yote yataisha,...usipoipata hiyo nafasi je? una miadi na 'minister of Justice' aliyepo mbinguni?

  mila na desturi;
  tunazijua mila na desturi zetu? au mila hukumbushwa pale binti anapotaka kuolewa tu kwenye utoaji wa mahari?

  'Upofu' wa mila za kigeni;
  Kwenye miaka ya sitini, serikali iliyapiga marufuku mashindano ya urembo (Ms Tanzania), ...wajanja (dada'ngu kina Farida fashion, Khadija mwanamboka, nk) wakatumia 'mianya' kuanzisha maonyesho ya urembo na mavazi mpaka serikali ilipoyaruhusu tena mashindano haya. Leo hii tuna Ms Utalii, Ms vyuo vikuu, Ms Universe, Ms Tanzania, Ms Redds, mpaka majuzi tumeshuhudia Ms 'Totoz'...

  Kwa serikali kuachia wazi maeneo kunakopelekea mabinti wengi kuwa na muono mfupi wa maisha, yaani sex sells. No wonder, tunashuhudia mabinti kati ya miaka 16-23 kwa wingi sasa waporadhi watumike kama bidhaa (na bidhaa haichagui mnunuzi) badala ya ku pursue higher education, na maisha bora ya kifamilia.

  ...nitarudi na 'blah blah' nyingine...
   
 5. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #5
  Aug 14, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...ndio maana wakasema, 'ukimfunda (vyema) mtoto wa kike, umeifunda jamii nzima,....ukikosea, jamii nzima itaangamia!'
   
 6. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #6
  Aug 14, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  1-hatuwezi kuwalaumu wazazi,kwa kusimamia msemo wa WE ARE THE IMAGES OF OUR PARENTS!NO WAY!kwasababu maisha ya sasa social interactions zimekua kwa kasi ya ajabu na ni nyingi!

  2-maendeleo ya kisayansi na technologia yamechangia kiasi.ingawa tatizo kubwa sana lipo kwa huyu mpokeaji wa huu utandawazi na namna anavyoutumia/apply practically kwenye maisha.dada zetu huku bongo wanalewa na mapenzi ya kwenye tamthilia,akiangalia maria-clara anavyoish anaamini ndio maisha halisi ya wazungu!WHICH IS WRONG!kuna mabinti wanapata hisia za tamthilia hadi wanasahau kwamba ni maigizo tu.

  4-Imani,mila na desturi VIMESHUKA SANA!wenzetu huko mbele mnaita MORAL DECAY!kwavyovyote vina mchango mkubwa sana.nisisitize tu hili linachangiwa na hoja tajwa hapo juu(no.3)

  5-kwatika hili serikali inaonewa
   
 7. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #7
  Aug 14, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...ngoja nikwambie wazazi tunavyohusika.

  kina mama wengi wanatizama hizo tamthilia kwenye luninga na watoto wao, hususan wa kike. Unakubaliana nami au? sio ajabu kabinti ka 8-11yrs leo hii kakakuhadithia series nzima za hizo tamthilia...

  Iwapo kabinti hako kataona mamie yake anavyobubujikwa na machozi, na haswa alivyo hooked kwenye hizo series, naye kidogo kidogo kataanza kujifunza 'maisha ndivyo yalivyo!'

  Enzi zetu ilikuwa sana sana tumewaangalia Charlie Chaplin, Laurel and Hardy, au Snow White na seven dwarfs.. utajifunza nini pale kama sio kucheka tu? Sana sana sinema ya 'mlevi' ilitufunda ubaya wa pombe!

  Wazazi tunachangia malezi ya watoto wao, hasa 'kuharibu' malezi ya mabinti wa kileo, aka wazazi wa kesho.
   
 8. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #8
  Aug 14, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  I would say it is the inevitability of the social version of the second law of thermodynamics and it's inherent increasing entropy that is bound with all closed systems.
   
 9. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #9
  Aug 14, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  state the law bana!unadhani kila mtu ni sayansist?
   
 10. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #10
  Aug 14, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mbu mi naona ni vyote hapo juu!
   
 11. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #11
  Aug 14, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  GIYF.

  Kuna concept fulani basic katika maisha kila mtu anatakiwa kuzijua, hata kama si mhasibu unatakiwa ujue tofauti ya debit na credit, this law is that basic.
   
 12. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #12
  Aug 14, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...si ndio hapo bana.

  sisi ndio wazazi wenyewe wa taifa la kesho, na sisi wenyewe tuishaanza kuonyesha dalili za kushindwa kuliendesha jahazi, unadhani hawa wazawa wetu itakuwaje na kizazi chao?

  angalia mfano wa vituko hivi;
  ...Wema Binti Sepetu, mnh mie wala sisemi wallahi...
   
 13. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #13
  Aug 14, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...kuna wenzetu hawajui size za viatu, suruali hata mashati yao wanayovaa, na hata ukimuuliza urefu wake au uzito wake yeye mwenyewe haujui.

  Unataka kutuadhibu bure na hizo terminologies na basic laws za 'kidhungu'
   
 14. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #14
  Aug 14, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  ..state the law please!
   
 15. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #15
  Aug 14, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Your request hinges on the extremes of laziness.

  GIYF= Google Is Your Friend

  [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Second_law_of_thermodynamics"]http://en.wikipedia.org/wiki/Second_law_of_thermodynamics[/ame]
   
 16. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #16
  Aug 14, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Mbu..nataka kubadili msimamo wangu wa awali kuwa wazazi wasilaumiwe.
  Kama tunazungumzia ndoa..kwenye ndoa si kuna kiongozi? Tena kiongozi huyu hapigiwi kura wala nini.Uongozi wake ukiwa bora basi tunatarajia familia/ndoa yake itakuwa na mafanikio na hata matatizo yatakuwa yale ya kawaida kabisa ya kibinadamu.

  Tatizo ni kuwa wengi wa hawa viongozi wamekithiri kwa uongozi mbovu, ufisadi, ubabe, kukosa mwelekeo, kutokuwajibika, kutokuwa na uwazi, kutokuwa na ukweli na uadilifu.Matokeo yake ni kukosa mwelekeo familia nzima.MAADILI YAKIKOSEKANA KATIKA FAMILIA ambapo watoto wanaona wazazi wanavyoishi kwa ubabe, visa,ukatili,utovu wa adabu na nidhamu, vitendo vya ukengeufu wa maadili usitarajie nao wakikuwa watakuwa wanandoa bora.

  Kibaya zaidi unakuta mwanamke na mwanaume wanakutana ukubwani kila mtu na background tofauti kwa maana ya kwamba mwingine kalelewa kwa maadili na upendo wa hali ya juu wa wazazi na hakujua kabisa tabia chafu za kukosa maadili.Anakutana na mwenzake aliyelelewa kwenye malezi mabovu ambapo wazazi hawana maadili.Sasa niambie hiyo ndoa itakuwa ya namna gani? Most likely yule aliyetoka kwenye background mbovu atakuja na vitabia vyake vibaya kwenye ndoa na kumkwaza yule aliyekuja na maadili mema- uchafuzi tu!
   
 17. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #17
  Aug 14, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...:D ayiiiii, kuuliza si ujinga... majibu mengine jamani yanaweza sababisha TIA (Transcient Ischaemic Attack) bureee!
   
 18. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #18
  Aug 14, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Huyu alikuwa haulizi, alikuwa anaomba maji ya kunywa wakati yupo kwenye mtumbwi katika Delta ya mto Amazon hapo Cabo Do Norte.
   
 19. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #19
  Aug 14, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145

  the entropy of an [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Isolated_system"]isolated system[/ame] which is not in [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Thermodynamic_equilibrium"]equilibrium[/ame] will tend to increase over time, approaching a maximum value at equilibrium.


  what are you tryng to explain here bana?
  .........that african moral ethics are not in equilibrium?
   
 20. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #20
  Aug 14, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  mwache mdogo wangu mwanasayansi anieleweshe!tulikimbia umande.tuna kingereza cha twisheni
   
Loading...