Kuporomoka kwa Uchumi: Wabunge waisingizia TRA!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuporomoka kwa Uchumi: Wabunge waisingizia TRA!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mr. Zero, Mar 16, 2011.

 1. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,509
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280
  Wabunge waikaanga TRA kuporomoka kwa uchumi Send to a friend Tuesday, 15 March 2011 20:54 0diggsdigg


  [​IMG]
  Leon Bahati
  MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imesema matatizo ya mgawo wa umeme nchini imesababisha kupoteza Sh295 bilioni katika makadirio ya makusanyo ya Sh3,686 bilioni kwenye kipindi cha miezi minane iliyopita.

  Akizungumza kwenye semina ya wabunge inayoendelea jijini Dar es Salaam jana, Naibu Kamishna Mkuu wa TRA, Placidus Luoga, miongoni mwa sababu zilizopelekea kushuka kwa mapato ni mgawo wa umeme.Semina hiyo ina lengo la kushauri serikali jinsi ya kukabiliana na kupanda kwa gharama za maisha, uhaba wa nishati ya umeme na njia za kubuni vyanzo vingine vya mapato.

  "Katika kipindi cha Julai 2010 hadi Februari mwaka huu, makusanyo yalikuwa ni Sh3,391 bilioni wakati matarajio yalikuwa Sh3,686 bilioni. Hayo ni mafanikio ya asilimia 64 ya matarajio ya kukusanya Sh5,652.6 bilioni kwa mwaka huu wa fedha 2010/11," alisema Luoga.

  Luoga alisema TRA imeweka mikakati kuhakikisha katika miezi minne iliyobaki mwaka huu wa fedha unaoishia Julai, kiwango cha makusanyo ya Sh5,652 kinafikiwa. Hata hivyo, wabunge waliishambulia TRA kwa uzembe wa masuala mbalimbali, ikiwamo kushindwa kukusanya kodi ipasavyo kwenye sekta ya madini, misamaha ya kodi na rushwa miongoni mwa wafanyakazi wake.Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Kabwe Zitto, alisema mwaka wa fedha uliopita 2009/10, serikali ilipoteza Sh630 bilioni kutokana na misamaha ya kodi.

  Zitto alilalamika kuwa, hasara hiyo ilichangiwa na misamaha ya kodi kwa wawekezaji sekta ya madini.
  Mbunge wa Viti Maalumu (CUF), Magdalena Sakaya, alisema ukwepaji mkubwa wa kodi unafanywa na wawekezaji kwa kubadilisha majina kila baada ya miaka mitatu, unafanywa kutokana na udhaifu wa sheria.

  Matatizo mengine yaliyolalamikiwa na wabunge ni urasimu unaofanywa na watumishi wa TRA na kusababisha wafanyabiashara kukwepa Bandari ya Dar es Salaam, tofauti ya kodi Zanzibar na Tanzania Bara, kodi kubwa kwenye mishahara ya wafanyakazi na kushindwa kukusanya kodi kwa Wamachinga.

  Lakini, Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tindu Lisu, alitofautiana na wenzake akisema, lawama hizo hazipaswi kutupiwa TRA bali ni wabunge waliotunga sheria dhaifu za ukusanyaji kodi mwaka 1997.
  "Kuwapo na kiwango kikubwa cha msamaha wa kodi wanaopaswa kulaumiwa ni wabunge sio TRA," alisema Lisu na kuongeza:"Kwa mfano mwaka jana sekta ya madini iliingiza Sh7.2 trilioni, lakini makusanyo ya kodi yalikuwa ni Sh283 milioni. Ukiangalia hapa utaona asilimia 94 ya utajiri wa Tanzania ulienda nje kutokana na tatizo la Bunge hili."
  Mwenyekiti wa semina hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi, Dk Abdallah Kigoda, alisema msamaha wa kodi Kenya na Uganda ni asilimia moja wakati Tanzania inafikia asilimia mbili.


  Source: Mwananchi

  My take: Huwa nashangaa ninaposikia kuwa mashirika yanatumia ujanja kukwepa kodi kwa kutumia sheria dhaifu iliyopo. Sasa kama washalijuwa hilo kwa nini wasibadilishe sheria??? Hizo pesa wanazopoteza kutokana na mgao wa umeme zingeweza kununua magenarator mangapi???

  Cha kushangaza, wabunge wote hawalioni hilo (pamoja na our own Brilliant Zitto) except Lissu!! Sheria na poor policy, lawama kwa TRA!!
   
 2. T

  Tata JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,743
  Likes Received: 661
  Trophy Points: 280
  Mimi nadhani kimsingi Zitto na Tundu wameongea kitu kimoja. Kwa nionavyo mimi Zitto ameongeleo matokeo wakati Tundu Lissu ameongelea chanzo cha matokeo hayo. Zitto ameongelea misamaha ya kodi ambayo inatolewa na TRA kwa mujibu wa sheria zilizopo za kodi. Tundu Lissu ameweka lawama pale inapotakiwa kwani wanaotunga sheria sio TRA bali ni Bunge kwa kusaidiana na Wizara ya Fedha inayoandaa miswada. Najua TRA huwa wana mchango wao katika kuandaa miswaada husika na ndio washauri wakuu wa waziri kwa masuala ya kodi.

  Lakini tatizo kubwa hapa ni kuwa TRA hawana maamuzi ya mwisho juu ya yaliyomo kwenye mswada wa kodi unaopelekwa bungeni. Pia hawawezi kulizuia bunge kupitisha muswada kuwa sheria hata kama imejaa utumbo. Ni wajibu wa wabunge kusoma kwa uangalifu miswada yote inayofikishwa bungeni na kujua madhara yake kabla ya kupitisha kuwa sheria. Lakini kwa kiwango cha hili bunge letu lililojaa ushabiki usio na tija sidhani kama wanaweza kupitia miswada ya sheria kwa uangalifu na UADILIFU. Big Up Zitto na Tundu Lissu.
   
Loading...