Kupoa kwa ndoa kuna sababishwa na nini??

QEEN ADEMU1

Senior Member
Joined
Dec 24, 2019
Posts
134
Reaction score
324
[emoji2771]Leo naomba kuuliza Wanandoa waliopo humu, hata wale ambao bado mabaharia mnakaribishwa Sana maana nyie ndio wahanga wakubwa wa hili suala. Mwanzoni munakuwa na mapenzi makubwa kwa wenza wenu lakini baadaye mambo yanaharibika.

[emoji2771]Kwanini wakati wa mwanzo wa mahusiano mnakua very romantic mpaka mnapelekea Ndoa, na baada ya Ndoa wengine hata mwaka hujaisha wameshaanza mipango ya kando na wanabadilika kabisaaa, mapenzi hakuna -- yaani "wanabakana" kwenye Ndoa zao.

[emoji2771]Hao hao Wanandoa kila mmoja akipata mchepuko nje anafanya vizuri lakini akija kwa Mume wake au Mke wake wanaishi kama wazee.

[emoji2771]Hakuna mahaba, hata jumbe tamu za maneno tu. Huwezi kuta Wanandoa wanaongea mambo ya Mapenzi, sana sana ni mambo ya Karo za shule za Watoto , Kodi ya nyumba nakadhalika. Hakuna hata Nakupenda Mpenzi, hakuna mashamsham , yalishaisha kitambo.

[emoji2771]Ndio maana Wanawake japo sio wote wanajitahidi kutafuta Makungwi na kujiunga kwenye magroup ya WhatsApp wanafundishwa namna na kumshika Mwanaume akupende, na Mwanaume naye japo sio wote yuko busy kushinda kwenye mitandao ya kijamii kutafuta company na Marafiki wa Kike.

[emoji2771]Yaani upendo umepoa kabisaa. Yale malovee hakuna kabisa kwenye Ndoa zetu. Kabla hamjaoana mlikuwa mnapeana raha mnaridhishana lakini baada ya mwaka mnabaniana unyumba au unapewa kwa masharti huku mkishindwa kuridhishana. Shida nini hapo Wanandoa[emoji780]

Wanandoa , najua wengi wapo humu na wahanga wa hili tatizo. Je, shida ni nini[emoji780]

Tunaomba Mwanaume mfunguke kero zenu na Wanawake wenzangu mfunguke kero zenu ili 2020 tujenge familia bora.

Ndoa bila usaliti, inawezekana. Karibuni[emoji779]

[emoji3590]Ndoa na IHESHIMIWE NA WATU WOTE [emoji120] NA MALAZI YAWE SAFI [emoji120] MAANA WAASHERATI NA WAZINZI MUNGU [emoji120] ATAWAHUKUMIA adhabu (Waebrania 13: 4)

Sent using i phone x
 
"Waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu"

Popcorn please! Nipo kujifunza hapa
 
1.kuchokana
2.kuchokana
3.kuchokana
4....
5...
Cc: chakula hata kiwe kitamu vepe Kula hiko hiko Kila siku inaboa...so you gat to seek another taste somewhere else

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tukumbuke ndoa ni kama biashara tu, inahitaji muda, rasilimali na uongozaji ili ipige hatua. Wanandoa wengi baada ya kuingia kwenye ndoa hujisahau na kuoana kwa kuwa tumeshaoana basi yote yamekwisha. Hawajui kwamba ndoa yenyewe ni namna gani wataishi maisha ya kila siku kwa lengo la kuiboresha na kuipa uhai zaidi ndoa, hakika ndoa ya kweli ni pale tu baada ya wanandoa hao kuanza kutambua ni kipi kinawaweka pamoja na kipi kinawatofautisha, watakapojifunza ni namna gani kuboresha kinachowaweka pamoja na kupunguza athari ya vinavyowatofautisha basi hapo ndoa hunawiri kila uchwao mpaka watakapozeeka au kutenganishwa na kifo, hakika ndoa ni maridhiano ya hiari na hakika hakuna mahala binadamu aliyekamilika anapaswa kujitolea kama kwenye ndoa. Kinyume chake ndo tunaona ongezeko la washauri wa ndoa na ongezeko la michepuko pia huku wanandoa wenye ndoa changa tu wakitamalaki kwa ugomvi na kila mmoja kutafuta mpango wa kando au kuzidisha uadui zaidi baina yao. Hakuna mganga wa ndoa ila wanandoa wenyewe, wanandoa wasiwe wagumu kuzungumzia yanayowaleta pamoja na yanayowatofautisha na kama wanaweza kuboresha yanayowaleta pamoja ili wawe karibu zaidi. Wazungumze kirafiki kama walivyokutana kirafiki kabla ya kuoana.
[emoji2771]Leo naomba kuuliza Wanandoa waliopo humu, hata wale ambao bado mabaharia mnakaribishwa Sana maana nyie ndio wahanga wakubwa wa hili suala. Mwanzoni munakuwa na mapenzi makubwa kwa wenza wenu lakini baadaye mambo yanaharibika.

[emoji2771]Kwanini wakati wa mwanzo wa mahusiano mnakua very romantic mpaka mnapelekea Ndoa, na baada ya Ndoa wengine hata mwaka hujaisha wameshaanza mipango ya kando na wanabadilika kabisaaa, mapenzi hakuna -- yaani "wanabakana" kwenye Ndoa zao.

[emoji2771]Hao hao Wanandoa kila mmoja akipata mchepuko nje anafanya vizuri lakini akija kwa Mume wake au Mke wake wanaishi kama wazee.

[emoji2771]Hakuna mahaba, hata jumbe tamu za maneno tu. Huwezi kuta Wanandoa wanaongea mambo ya Mapenzi, sana sana ni mambo ya Karo za shule za Watoto , Kodi ya nyumba nakadhalika. Hakuna hata Nakupenda Mpenzi, hakuna mashamsham , yalishaisha kitambo.

[emoji2771]Ndio maana Wanawake japo sio wote wanajitahidi kutafuta Makungwi na kujiunga kwenye magroup ya WhatsApp wanafundishwa namna na kumshika Mwanaume akupende, na Mwanaume naye japo sio wote yuko busy kushinda kwenye mitandao ya kijamii kutafuta company na Marafiki wa Kike.

[emoji2771]Yaani upendo umepoa kabisaa. Yale malovee hakuna kabisa kwenye Ndoa zetu. Kabla hamjaoana mlikuwa mnapeana raha mnaridhishana lakini baada ya mwaka mnabaniana unyumba au unapewa kwa masharti huku mkishindwa kuridhishana. Shida nini hapo Wanandoa[emoji780]

Wanandoa , najua wengi wapo humu na wahanga wa hili tatizo. Je, shida ni nini[emoji780]

Tunaomba Mwanaume mfunguke kero zenu na Wanawake wenzangu mfunguke kero zenu ili 2020 tujenge familia bora.

Ndoa bila usaliti, inawezekana. Karibuni[emoji779]

[emoji3590]Ndoa na IHESHIMIWE NA WATU WOTE [emoji120] NA MALAZI YAWE SAFI [emoji120] MAANA WAASHERATI NA WAZINZI MUNGU [emoji120] ATAWAHUKUMIA adhabu (Waebrania 13: 4)

Sent using i phone x

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna kitu binadamu akaridhika nacho milele hasa wanawake. Mathalani, cheusi mangala anajichubua awe cheupe dawa, mwenye flati skrini anatafuta wapi mchina ili awe afungashie. Wanandoa wengi wanaishi kwa kuvumiliana tu ila upendo ulisha expire kitambo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom