mwibi
Senior Member
- Jul 28, 2016
- 131
- 79
Serial killer Gary Leon Ridgway alimaarufu kama Green River Killer, mtu alieua wanawake wasiopungua 49 katika mji Wa Washington kabla hajakamatwa mwaka 2001
MAISHA YAKE
Gary Leon Ridgway alizaliwa 18/01//1949 katika mji Wa Salt Lake huko Utah, Marekani alikuwa anafanya kazi kwenye gari ya kusambaza rangi takiribani miaka 30 na ameona Mara tatu. Alianza mauaji ya Wanawake mwaka 1982 na kukamatwa 2001. Baada ya vipimo vya DNA kumtambua. Ridgway aliwambia Wapelelezi kuwa ameua Wanawake kama 75-80 au zaidi katika barabara ya 99 iliyoko South King huko Washington. Alitubu na kupata kifungo cha maisha mara nne.
MAUAJI YA GREEN RIVER
Ridgway alianza mauaji mwaka 1982, baada ya vijana wa kike waliokimbia makazi yao na Malaya kuanza kupotea kwenye barabara ya 99 iliyopo South King huko Washington. Alipeka wengi wao nyumbani kwake baada ya kuwasulubu na kisha kuwabaka kisha kuwapeleka kwenye msitu na kuwaacha. Alikamatwa baada ya kuanza kutumika teknojia ya vinasaba yaani DNA.
HUKUMU YA MAISHA MARA NNE
Ridgway alitakiwa kunyongwa lakini alifanya makubaliano na wapelelezi ili awambie ni wapi alipowaficha miili mingine ambayo bado ilikuwa haijawahi kuonekana na pia alikubali kuhusishwa na kesi zitakazotokea na kumhusisha au kuendana na mauaji yake. Na alifungwa mwaka 2003. Pia akawa ndie mtu aliyeuwa watu wengi kwa makusudi (serial killer) kuliko watu wote katika historia ya Marekani.
Na mwili mwingine ulipatikana mwaka 2013 na kuhusishwa na Ridgway na kufanya serikali imuongezee tena kifungo kingine cha maisha jela.