Kupitia kipindi cha Ajenda 2020 Star Tv nitazungumza na Watanzania kwanini nimehamia CCM

Mar 3, 2018
75
799
Nilianza siasa za kugombea katika nchi yangu August 2015.

Ni kweli kwamba nilichaguliwa kuwa Diwani wa Kata ya Gwarama nikiwa Mwaka wa 2 Chuo Kikuu cha Dar es salaam kama alivyoandika kaka yangu @malisa_gj na @charles_william2 .

Nilipewa heshima kubwa sana na ya pekee kama Kijana aliyeamua kupeleka maarifa yake kusaidia jamii yake na kweli nilipokelewa vizuri na Watanzania wenzangu Waishio Gwarama ya Tanzania kwa kupata kura 4,500 dhidi ya zile 1,500 za Mgombea wa CCM na NCCR-Alipata kura 84.

Hapa ndipo nilianza kupata hoja za kupinga usemi wa kwamba Nabii hakubaliki kwao kwani Mimi ( "Nabii Elia" kwa kutumia maneno ya Baba yangu @freemanmbowetz nilikubalika kweli kweli) na hata niliposhinda Wananchi walinieleza kuwa nirudi kuhitimisha Shule kwani wao nitawakuta,nilirudi na nikahitimisha Shahada ya kwanza na kisha nikapata Bahati ya kuendelea kusoma Shahada ya pili hapo hapo Mlimani japo nilikuwa huru kuishi na kufanya Kazi za Wananchi.

Nilipendwa nyumbani na nikapendwa na nje ya nyumbani hata wewe unaesoma ujumbe huu ukawa umenifahamu.
Wakati huo nilikuwa Mgeni kwenye masikio ya Viongozi wa CHADEMA Taifa.

Mwaka 2017 nilifahamika zaidi kwenye chama na ikapelekea kupewa heshima ya kugombea ubunge katika uchaguzi mdogo 2018.

Kama ambavyo CHADEMA ilimlea kaka yangu @zittokabwe na dada yangu @halima_james_mdee na mimi nilipata malezi pia baada ya CHADEMA kugundua kuwa nina kitu ambacho kinahitaji malezi.

Heshima yote hiyo nimeipata kutokana na nguvu iliyoko ndani ya moyo wangu,nguvu inayonisukuma kufanya siasa. Niliamua kutoka ndani ya roho yangu kufanya siasa ambazo mpaka nazipenda kweli.

Moja ya mambo yaliyonisukuma kufanya siasa ilikuwa ni kubadilisha kwanza eneo ninalozaliwa kwani ujambazi ulikuwa umekithiri na wananchi walikuwa hawawezi kufanya maendeleo maana wenye jitihada za maendeleo walikuwa wanauliwa. Huku ni mpakani mwa Tanzania na Burundi kuna mambo mengi.

Babu yangu alipotaka kufariki 2013 aliniita akanishika mkono na akaniambia "umebarikiwa na Mungu" nikiwa nimesimama mbele yake na pembeni yangu alikuwepo baba yangu ambae ni Mchungaji akaniambia nipige magoti aniombee na nilifanya hivyo nikakutana na upako huo wa maombi.

Nguvu ya kufanya maamuzi binafsi ikanifanya nifahamike kwa Watanzania. Hata nilipopata heshima ya kugombea Ubunge mwaka 2018 kwa mara ya kwanza Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilinitangaza kuwa nimepata kura 19,600 dhidi ya zile 24,000 za aliyetangazwa kuwa mshindi.

Ikumbukwe kuwa niliambiwa nimepata kura hizo bila kuwa na Wakala wa majumuisho,kwa hiyo kazi ya kuhesabu kura ilifanywa na Mkurugenzi pamoja na Mawakala wa vyama vingine 8 kwani Wagombea tulikuwa 10 ila yule wa ACT Wazalendo aliniunga mkono.

Kupitia Uchaguzi huo Watanzania wengi zaidi walinifahamu na wengi wakanitia moyo wakasema wewe bado ni Kijana utafika mbali.Nawashukuru kwasababu hawakusema nitafika mbali nikiwa CHADEMA tu. Kwa tafsiri nyingine waliniona Mimi zaidi kuliko chama Nilichokuwa napitia.

Nina umri wa Miaka 29,toka zamani nilipanga kuwa nitakapofikisha miaka 30 nitaanza Kazi rasmi ya kuvuka nje ya mipaka niliyozaliwa na kueneza kile nilicho nacho mahali pengine. Msimamo huu ulikolezwa na maandiko matakatifu yaliyopo kwenye Biblia kuwa Yesu alianza kazi Rasmi akiwa na Umri wa miaka 30 umri ambao ninaufikisha Mwaka kesho 2020.

Nimeamua kuhama chama,nimeona pia kupitia Kipindi cha AGENDA 2020 chini ya Kaka yangu @alloyce_nyanda pale StarTV Dec 02 Saa tatu na nusu usiku niongee na Taifa juu ya hatma yangu Kisiasa.

Naomba niangaliwe na nisikilizwe maana ni haki yangu kusikilizwa kisha Maisha yaendelee.

Ninakuomba @alloyce_nyanda uniandalie maji makubwa ya Jambo yaliyoandikwa "JAMUKAYA" maana wewe nae umeamua.

Elia F Michael.
Aliyekuwa Diwani na Mgombea Ubunge Jimbo la Buyungu 2018.

IMG-20191124-WA0093.jpeg
 
Kumbuka bila CHADEMA kukupa fursa usingefikia hapo ulipo.

Ni ngumu kumwamini mtu wa Kigoma au Arusha kumpa cheo kikubwa katika chama maana nyie ni vigeugeu sana mnafika bei kirahisi.Ilianzia Walid Kabouru

2020 usitegemee CCM kukupitisha kugombea cheo chochote maana wenye chama wana bifu na nyie wahamiaji kina mtatiro.

Hakuna chama chenye mapungufu ila huko CCM ni kwa mafisadi juzi mkapa kakiri waliiba pesa za EPA
 
Dah!! Ila pesa haijawahi kushindwa kitu, labda kurudisha uhai tu, mkuu kwahiyo uliona ukiwa CHADEMA ambayo unakiri imekulea, ukifikisha miaka 30 hutoweza kuvuka mipaka ya ulipozaliwa? Kwamba CHADEMA ambayo unasema ilikupa heshima kubwa mpaka nafasi ya kugombea ubunge ilikuwa inakubania wewe kuvuka mipaka?

Unadhani ungekuwa CCM ungepewa nafasi ya kugombea udiwani ukiwa na miaka 25 tena ukiwa upo chuo unatumia boom kuishi na huna pesa za kuhonga?

Sawa bwana Elia, siasa ni fursa na wewe ifuate fursa ilipo
 
Elia F Michael,
Mtoto mpuuzi sana wewe, umeuza moyo wako kwa shetani halafu unatuletea ngonjera zako hapa. Leo umeungana na waliomuua Mawazo, waliompiga risasi Lissu na wakandamizaji wa demokrasia, eti unataka kufanya siasa zinazovuka mipaka, hiyo akili hata huna ulikua unabebwa na uchadema tu.
 
Back
Top Bottom