POTOSHI Kupitia kikao cha mtandaoni CHADEMA, Joseph Mbilinyi asema wanaikataa No reforms, No election

POTOSHI Kupitia kikao cha mtandaoni CHADEMA, Joseph Mbilinyi asema wanaikataa No reforms, No election

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha


1757921429958.png
 
Tunachokijua
Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu ni mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Nyasa lakini pia amewahi kuwa mbunge wa bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa vipindi tofauti kupitia jimbo la Mbeya Mjini.

Madai

Ipo video inayosambazwa mtandaoni ikidaiwa kuwa ni kikao cha CHADEMA kilichofanyika kwanjia ya mtandao ikisikika sauti ya Joseph Mbilinyi akisema "CHADEMA Kanda ya nyasa na nchi nzima hatutaki na tunakataa kwa nguvu kabisa No reforms, No election"

Uhalisia

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck umejiridhisha kuwa video hiyo inapotosha uhalisia kwani sauti hiyo ya Sugu hakuwa katika kikao cha mtandaoni cha CHADEMA. Vilevile sauti hiyo imehaririwa kwa kuondoa baadhi ya maneno jambo lililopotosha ujumbe halisi.

Kupitia utafutaji wa maneno muhimu (Key words search) imebainika kuwa sauti hiyo imetolewa katika video halisi ambayo Mnamo tarehe 20 Agosti, 2025 Sugu alifanya mkutano na waandishi wa habari, ambapo pamoja na mambo mengine alibainisha kuwa hakuna hatua zozote zilizochukuliwa licha ya watu kupotea akiwemo Deus Soka na wenzake.

Katika sehemu ya sauti inayosika kwenye video iliyopotoshwa, uhalisia ni kwamba Sugu alisema wana CHADEMA kanda ya nyasa wanasimama na msimamo wa 'No reforms, No election' pamoja na kukataa sheria za hovyo za uchaguzi zinazoleta kadhia kwa wagombea na wapiga kura na kudai mabadiliko ya sheria hizo.


View: https://www.youtube.com/live/uKYw8JinUVc?si=l-_jh5PlNprohw_c&t=731
Back
Top Bottom