Kupinduliwa kwa Nkurunzinza

Huna unalolifahamu wewe unajiaibisha tu hapa, so unataka kutuambia Kabila aliuawa na Kagame sio? mnachekesha sana nyie watu, kiRwanda mnakioverrate mpaka mnakera.
 
Habari hii ishagaandikwa humu, umezidisha sukari kwenye chai, kwamba aliondoka Dar es salaam, kafika Bujumbura akazuiliwa kutua ikabidi aende Entebbe ambako nako akazuiliwa kutua, hapo ikabidi arejee Dar es salaam, MIZUNGUKO yote hiyo ilitumia NUSU SAA TU....!!!?? [emoji28][emoji28][emoji28]
 
Huna unalolifahamu wewe unajiaibisha tu hapa, so unataka kutuambia Kabila aliuawa na Kagame sio? mnachekesha sana nyie watu, kiRwanda mnakioverrate mpaka mnakera.
Kabila kauawa na nani?? Ama hujui operation kitona ilianzishwa kwaajili ya nini?

Nmeshakuambia Marais wa Kihutu 3 waliuawa na UPRONA/RPF alliance between 94-96 sasa kama hilo unapinga niambie facts zako sio unakosoa huku hautoi unachojua wewe.
 
Mie nadhani ,intelijensia ya Tz inahitai maboreho hasa ya vifaa ya kitknolijia ila kia kili tupo vyema ,angalia cabo delgado, Nairobi ,Kampala ,Kigali, Bunjumbura,Comoro ,lilongwe mpaka mogadishu

Achaneni na Tz ,tu si undermine ,kikubwa maboresho kila wakati yafanyike
 
Kigali ndio kinini?
Na Rwanda ndio jamaa gani huyo?
 
Habari yako ipo vizuri ,ila kuna vitu vinavifichwa kuhusu mapinduzi ya Burundi 2015 yalizimwa na vyombo vya ulinzi vya Tanzania(Story zetu vijiweni)
Mapinduzi yalifanyika asubuhi wakati kikao kinaendelea DSM
Waasi walijua tu kikwete atamsaidia Nkurunzinza kurudi Bujumbura.,kweli mpaka mkubwa wenye barabara nzuri wa kobelo ulizungukwa na wanejeshi wakidai ,nkurunziza ana kuja na msafara kutoka mwanza
Ukweli ni kwamba ndege ilienda tupu Bujumbura ikazuiwa kutua ,waasi wakaona wameshashinda mapinduzi, kumbe Nkurunziza alishukia Ngara airstrip usiku wa manane akabitishwa Murusagamba ,akaingia ikulu kiulani kwa msaada wa Tz, Huku ndege ukiangalia kwenye rada za simu janja za waasi ilikuwa ina hangaika kutua mara mwanza, entebe ,kigali,dsm,KIA
inasemekana kulikuwa na mkono wa kigali kwenye hayo mapinduzi yaliyo faili...

(alafu kuna vijana wa hovyo kipindi hicho tulikuwa tunamuitaa Kanali Kikwete ni dhaifu)
Kongole kwake Mzee wa Msoga maana mapinduzi yangefanikiwa diplomasia yetu na majirani ingekuwaje?
 
Kigali ndio kinini?
Na Rwanda ndio jamaa gani huyo?
Kasome historia ya vifo vya Marais Burundi tokea Kagame aanze harakati ndio utaelewa nachosema.

Kuna Rais alipigwa risasi nje ya Ikulu kabisa ndio sembuse huyu wa angani!! Ndio maana Nasema Kigali haikuhusika hapa asingepona huyu.
 
inasemekana kulikuwa na mkono wa kigali kwenye hayo mapinduzi yaliyo faili
Kagame hakuhusika mkuu hizo ni story tu za Nkuruzinza kupata huruma ya waHutu Ili waungane!! Ni kama hii issue ya Maasai ikageuzwa kuwa ni wakenya ndio wamevamia hiyo ardhi!! Hiyo yote ni kuwaunganisha Raia wawe "kitu kimoja" Ili kupambana na "mgeni".

Kagame angehusika hapo Nkuruzinza angeshapotezwa kitambo. Burundi haina Jeshi Wala intelligence yoyote ndio maana mwaka jana kuna wakati hadi waasi waliteka airport kwa masaa kadhaa unabaki unashangaa!! Hii nchi Ina polisi au Jeshi kweli?
 
Sisi levo zetu ni sauzi ,mosaad KGB, na CIA ,huyo kagame yupo hapo kwasababu ya sisi.
Ilikuaje mkapigwa ambush na Kagame both in Darfur na kule Eastern Congo!! Vita ni tactics na timing, unaweza kuwa na inteligensia kama CIA ila wakakuwahi kama September 11.
 
Kwa mambo ambayo hamyajui ..msijifanye kuyajua kwa undani..buyobe Kuna vitu kaandika uongo.
 
Naomba kufahamishwa hapa,aliwezaje kurudi ikulu wakati waliompindua wameshaiteka
 
Ilikuaje mkapigwa ambush na Kagame both in Darfur na kule Eastern Congo!! Vita ni tactics na timing, unaweza kuwa na inteligensia kama CIA ila wakakuwahi kama September 11.
Nilezee kuhusu ambush ya Darfur kaka hutojali
 
Halafu mizunguko yote hiyo waasi hawakushtuka bado. Kitendo cha kukataliwa Entebbe tu kilitosha kumuangamiza
 
Kikwete angemtuliza tu hapo mjengoni.....kwa nini abadirishe katiba na kuwa na uchu wa madaraka??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…