Kupimisha Kiwanja na kupata offer...

Nimeshatumia 1.4 mil bado hakijaeleweka,Ardhi hapana bei kamili mkuu
 
True matapeli ni wengi mimi na wenzangu kama saba hv tulichaga laki nne na nusu ili jamaa apime aweke beacons baada ya hapo tufatilie hati jamaa alipotea mpaka namba yake imeota kutu, muhimu kuwa makini
 
Yaani mpimaji kuja na GPS na kuchukua coordinates kisha kwenda kuangalia kwenye ramani za jiji ndiyo ighalimu laki tatu?
nimepima viwanja vyangu vitatu, sina gari ila usafiri ilinigharimu 50000 kumtoa mtaalamu mpaka site 150000 baada ya hapo anaenda wizarani kupeleka zile coordinates wamtafutie kama zina someka kwenye maeneo yaliyopimwa ....ingawa kitaalamu wanasema gps inapoteza coordinates kuna kifaa kingine wanakikodi (sikikumbuki jina) kukodi tu sh laki tano ambacho hakipotezi coordinate, na gharama zingine, kheri yako we unayejua short cut...
 
Mimi nimenunua kiwanja kimepimwa ila sijapewa namba na alieniuzia kaniambia namba baada ya wiki itatoka je sijapigwa changa hapo.
 
Nimeshatumia 1.4 mil bado hakijaeleweka,Ardhi hapana bei kamili mkuu
ni kweli hapana bei maalum, kutokana na ukubwa wa eneo na mahala eneo lilipo, itambulike kuwa kuna maeneo hayapimiki (hayafai kwa matumizi ya kibadamu) kama mabondeni nk ila ukienda kwa afisa mipango miji asiye mwaminifu atakulia hela ukome, kuna watu wamenunua au wamejenga maeneo ambayo yalipendekezwa kwa shughuli maalum kitaalamu wanaita (planned) au eneo lenye mchoro, pia hii sio rahisi kwani inabidi afisa mipango miji achore eneo lako aliingize kwenye ramani kisha apeleke baraza la ardhi kama watapitisha mchoro huo, kuna watu wamenunua maeneo ambayo hayaja pangwa yaani squatters hii inabidi mjikusanye wananchi kwani huwezi kwenda ardhi ukawambia wakupimie eneo lako peke yako......kwa hiyo cha msingi na muhimu kabla ya kuanza kupima inabidi ujue eneo lako liko wapi?
 
Sawa mkuu. Hongera. Niliuliza tu na sikumaanisha kama najua shortcut. Ila kwa sababu hizi bei siyo rasmi na uwa ni negotiable tukubali kwamba kuna uwezekano wa kupata huduma hiyo hiyo kwa bei ya chini zaidi kutegemea na mpimaji mwenyewe na bargaining strength ya mtaka huduma ukiongezea na options alizonazo za wapimaji.
 
Mk

mkuu mbona lugha humu wametumia ya kiswahili. kama unataka kujua utaratibu wa mchakato endelea kusubiria. kama unataka Title deed uletewe we weka huo mkwanja uone miujiza.
 
Staff mwenzangu kapata hati last year na katumia 1.2m tu....kiwanja chake kipo Goba ...acheni kutisha watu na hizo 3.5m zenu .....mimi nimempa mtu kazi hii nitatoa ushuhuda hapa.....
ukiwa na marejesho ni Bcc mkuu
 
4900 ni square yard = 4047 square meter = acre 1 = hectare 0.4
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…