Nahisi kuchanganyikiwa hapa, naomba kuelekezwa tena...Kiwanja changu cha 1000sqm kita ni cost bei gani na ipi process ya kuanzia ili nipate hati
Huyu anayekuambia 800000 kupima kiwanja sidhani kama ni surveyor. Kupima kiwanja hadi unapata plani yako ni kuanzia 2000000,chini ya hapo mtazimiana simu. Kama ni nje ya dsm bei hiyo inawezekana. Ni mimi suryeyor nimemaliza 2005 na Bsc in Geomatics
Upimaji wa viwanja sekta husika ni ipo? Ardhi au manispaa? Mimi hapa ndipo nachanganyikiwa. Pesa analipwa mtu anayepima au ni pesa ya sekta husiika?? Wengi tuna shida na hii kitu ya kupima viwanja tunashindwa kujua nani ni mhusika halali wa upimaji wa viwanja maana nilishawahi Pima kiwanja na kumlipa pesa mtu wa ardhi lakini kwenda wizarani kulikuwa hakuna hati ya kiwanja wala faili. Matapeli wa viwanja ni mlolongo kuanzia upimaji uuzaji ununuaji umiliki nk Msaada tafadhali mwenye kujua suluhu la jambo hili.
Nakubaliana na wewe,mimi mpaka sasa nimebwagiwa mawe hapa nyumbani huu mwezi wa sita sielewi kinachoendelea. Nchi hii ina vituko sijapata ona.
Ndo madhara ya kukimbilia kuja kuulizia JF! Kuwa mpole! Ulishindwa nini kwenda kuulizia kwa watu ARDHI hapo mjini kwako? Hapa umekumbana na ma-solovea unaona sasa? Wengi wanaokushauri si watumishi Wa halmashauri ni watu waliosoma maswala ya ARDHI lakini wakabaki mitaani, hivyo wamebaki kudandia tu wakisikia MTU anataka kupimiwa kiwanja wanadanganya inawezekana! Ukweli ni kwamba ardhi wanapima kwa kufuata blocks. Hivyo utakavyowaendea kuhusu kupimiwa watakuuliza mko wangapi kwenye block yenu? Mimi huu nakupa maelekezo niliyopewa na Afisa ARDHI!!
Stesheni 2005 kulikuwa hakuna Bsc in Geomatics Bali Land Surveying. Wakati huo tuliwaita LS mi nilikuwa LMV.
Gharama za upimaji zina tegemea mambo makuu mawili
1. Kama Eneo lako lipo kwenye ramani ya mipango miji
2. Ukubwa wa eneo lako
Kama eneo ambapo kiwanja kipo Hakuna city plan Au ramani ya mipango miji basi ujue gharama itakuwa si chini ya 3M, sababu itabidi ulipie mchoro wa mipango miji uchorwe na kupitishwa ardhi. Gharama za kuchora huo mchoro ni 4M Sababu inabidi uhonge. Kama eneo lina city plan then Hiyo gharama unakuwa umeiepuka
Ukishapata mchoro ndio zoezi la kugawa eneo lako na kuweka mawe linafuata, hili zoezi hufanywa na surveyor yoyote na bei yake inategemea na ukubwa wa eneo lako. Kama eneo lako Ni kubwa litatoa viwanja vingi bei inakuwa ndongo kwa kila Kiwanja Lakini kama eneo dogo basi bei kwa kiwanja inakuwa kubwa. Kwa kawaida bei ina tofautiana kati ya surveyor na surveyor
NB: Hizo estimate za bei ni kwa dar kwahiyo mikoani zinaweza kuwa tofauti.
Mimi naomba kuuliza ma surveyor. Kuna eneo langu nilitaka kulipima na nimwashajenga. Ila baada ya kuchukua vipimo linaonyesha lipo kwenye OPEN SPACE. Niliongea na surveyor akanambia kuliondoa kwenye open space inawezekana ila ni gharama kubwa. Je ilo swala linawezekana?
Mimi naomba kuuliza ma surveyor. Kuna eneo langu nilitaka kulipima na nimwashajenga. Ila baada ya kuchukua vipimo linaonyesha lipo kwenye OPEN SPACE. Niliongea na surveyor akanambia kuliondoa kwenye open space inawezekana ila ni gharama kubwa. Je ilo swala linawezekana?
Pole ndugu hilo swali halihitaji surveyor kujibu.Open space lazima iwepo eneo husika, wakitoa kwako watapata wapi kwingine pakueka open space? Maanake wamnyanganye mwingine kiwanja.Subiri kulipwa fidia ya nyumba yako.Kama nyumba haijaisha sitisha process za kujenga.
Umemkamata vibaya!!.Ha ha ha aaah!!
Mimi nilimaliza 2005 B Arch! Geomatics ilikuwa bado!
Nimekuambia sibishani kitoto,mimi ni surveyor nafanya kazi serikalini,ofisa ardh hausiki na gharama za upimaji,bali anahusika na garama za umilikishaji ambazo ni ndogo sana,unapoongea ujinga wakati watu wanataka kujua inaonesha how iliterate you are. Kupima kiwanja bei ya serikali kwa hapa dar ni 2000@sqm. Kama umemuuliza huyo kishoka wako mbona hutuelezi wanafanyaje.
Umemkamata vibaya!!.Ha ha ha aaah!!
Mimi nilimaliza 2005 B Arch! Geomatics ilikuwa bado!
Kama kiwanja kiko kwenye surveyed area, gharama zinazobaki ni zipi?