Labda nitoe mfano ulio hai kabisa na current hapa nilipo;sisi tumejikusanya kama watu 5 na tuna jumla ya ekari 14 na Mara baada ya vipimo vya shamba zima Kwa eneo LA ekari hizo 14 tumepata viwanja 22 na mpimaji amesema kila kiwanja kimoja tumpatie laki mbili unusu je ni sahihi kweli au anatupiga huyu jamaa?
Lol!!! Umevamia Treji Kwa Mbele, Inawezekana Wewe Ni Kanjanja Wa Elimu Ona Wenye Taaluma Wanavyokuumbua, Tuambie Hiyo BSC Ya Geomatic Umeipatia Wapi??
Huyu anayekuambia 800000 kupima kiwanja sidhani kama ni surveyor. Kupima kiwanja hadi unapata plani yako ni kuanzia 2000000,chini ya hapo mtazimiana simu. Kama ni nje ya dsm bei hiyo inawezekana. Ni mimi suryeyor nimemaliza 2005 na Bsc in Geomatics
Tuelimishe bwana, mbona wanasema huwezi kupima kiwanja kimoja kimoja mpaka mjiunge wengi! Is this true? If not process ya kuomba kupimiwa ikoje maana no body tells what actually the process is/or seems to know even those in the field. Msaada tueleweshe
Kiwanja kimoja kinapimwa,muhimu kiendane na jinsi ramani ilivyo.
Samahani naomba kueleweshwa hizi law density, medium na high density range zake katika sq. meter zinakwendaje? yaani nikitaka kupima shamba langu zima liwe na viwanja vya low density kwa heka moja nitapata viwanja vingapi?Habari za jioni wana Jf.
Nina Kiwanja kidogo around 1000sqm nataka nipime nipate offer, jirani zangu wao swala lakupima hawataki kuliskia sasa nilitaka kujuaa kwa Kiwanja kidogo kama hicho process zinakua vp na gharama inakua aje?
Huyu anayekuambia 800000 kupima kiwanja sidhani kama ni surveyor. Kupima kiwanja hadi unapata plani yako ni kuanzia 2000000,chini ya hapo mtazimiana simu. Kama ni nje ya dsm bei hiyo inawezekana. Ni mimi suryeyor nimemaliza 2005 na Bsc in Geomatics
Kila mtu ana ushuhuda wake hapa, sasa sijui kama tunaweza kumsaidia ndugu yetu au la but upimaji kwa sasa ni biashara kabisa hivyo tukienda kichwa kichwa tutapigwa ile mbaya. Mimi nimeanza process za kwanza, shamba lipo kibaha ekari 4, umbali wa 12kms kutoka barabarani kuu, jamaa kuja kulipima na kuchora mchoro tu amekula laki 8. Ananiambia mchoro sasa unatakiwa kupelekwa Kisarawe wilayani kwa planner naye anakazi yake ataniambia gharama zake lakini zitakuwa sio chini ya milioni 3. Hapo sijui nimepatwa au ndio hiyo sawa tu?
Samahani naomba kueleweshwa hizi law density, medium na high density range zake katika sq. meter zinakwendaje? yaani nikitaka kupima shamba langu zima liwe na viwanja vya low density kwa heka moja nitapata viwanja vingapi?
Thanks ndugu yangu maana mambo hayo yanahitaji ushauri. Sasa hilo la range za viwanja vya low density ikoje? Nimeuliza hapo juu.Gharama alizokuambia ni sahihi.
Umedanganya hapo.........geomatics haikuwepo 2005....labda kama hukusoma tz
Asante sana. Shamba la heka moja najua lina 4900 sqm., pakitolewa barabara hapo naweza kubaki na 2000sqm.? Hivyo heka 4 nikapata 8,000 sqm.?High density=400-600
Medium density=601-999
Low density=1000-
Pole ndugu yangu, nililiona mwanzo sana hilo, nahisi hakuna jibu la moja kwa moja kuhusu gharama, zinatofautiana kwa mtu na mtu na sehemu uliyopo. Ukipenda kumjaribu huyo jamaa niliyemtumia mimi nitumie ujumbe wa private nikupe namba zake umtafute. But in short changanua katika maongezi hayo yote utapata in avarage ni kiasi gani.Nahisi kuchanganyikiwa hapa, naomba kuelekezwa tena...Kiwanja changu cha 1000sqm kita ni cost bei gani na ipi process ya kuanzia ili nipate hati
Ooooooh!!! thanks nimejifunza kitu hapo thanks again. Kila siku najifariji najua kwamba heka moja ni mita 70 kwa 70 hivyo heka moja ni 4,900 sqm. Thanks kamanda.Ekari moja ni 4047sqm na si 4900