Kupima HIV inahitaji moyo

Kupima HIV inahitaji moyo

Hhaaaa kwenye kupima utajiaminije wakati unaemuamini /anaekuamini ndie anaekumbukiza HIV?
Hahaha kwa hali hii hata mimi nimeanza kuogopa kupima Pima , zamani nilikuwa najidungua tu muda wowote with full confidence.
Ila sasa hivi lazima jasho likutoke dadekiiii.
 
Umenikumbusha aisee, wangu alikuwa na hako kamchezo bwana, sasa mwaka jana ile naanza clinik nikamuomba twende akaleta excuses kibao, nikasema ngoja nimkomeshe. Nikaen
da Hospitali, basi kila dk ananipigia anauliza eti vipi majibu!! Nikapima majibu kuja niko poa, basi nikazima sim afu nikapita kwa dadangu nikakaa hadi saa 4 usiku.

Jamaa alipunic ile mbaya! Nikarudi home nikajivisha sura ya huzuniiii! Basi ile kuniona tu na sura ya huzuni akajua kwisha habari yake! Nikaingia room kimya kimya bila hata salamu. Akaniuliza vipi wife mbona ulizima sim?Nikakaa kimya, akaendelea na maswali nikalipuka na kilio eti majibu sio mazuri.

Jamaa alinywea balaa, nikaonajasho linamtoka, kawasha feni mara kajipepea! Katoka nje hajielewi, mara kamwita first born wake, mwanaume kamasi jepesi hiloooo! Mara karudi home kaanza kulia nikamuuliza unalia nini kama ukimwi unao tayari daah! Baadae nikamuonea huruma nikamwambia ni uongo mana nilihisi alikuwa anatafta namna ya ku commit suicide. Wiki nzima mwili wake ulikuwa wa baridi kama mjusi.
haaaaaaaaaaaahaaaaa mbavu zangu kwi kwi kwii
 
we acha tu!hyo siku nusu nijikojolee nikisubiri majibu
 
namba tano ingia! unajua ukimwi ni ugonjwa km magonjwa mengine lakini unahitaji kuchukua tahadhari katika mahusiano ya kimapenzi. zipo njia nyingi za kujikinga na maambukizi mapya ya VVU natumaini unazifahamu.Pia umefanya jambo la msingi sana kuja kupima na kujua hali ya afya yako...(mpaka hapo mtu mimacho imetoka huku huku kwapa zikivuja jasho) then unaambiwa HONGERA UKO SALAMA! Unaweza kudhani unakudanganya kutokana na orodha yako ya ngono zembe. UKIMWI HATARIIIIIII!
 
Hii imo humu
Jana nilienda kupima HIV pale Angaza Mnazi MMoja. Lengo ilikuwa nijijue hali yangu kiafya ili niadhimishe siku ya ukimwi duniani "while I'm informed".

Nimengia hapo angaza saa 2 asubuhi, nikakuta kundi la watu wa kutosha tu. Basi ndio tumewekewa video kwenye TV wakati tukisubiri vipimo (Video ilikuwa na mikwara mingi sana kuhusiana na mambo ya ukimwi). Baadaye kidogo, akaja dada mmoja, ni mrembo, katupa semina na watu wakauliza na kujibu maswali kadha wa kadha.

Angaza sio mchezo! Nilikuwa mtu wa kati katika mfuatano wa kwenda kupima. Waliotangulia, kuna watu walitoka wanacheka, wengine walitoka na nyuso zimebadilika, wengine wanalia, n.k.!

Muda huo, wakati wengine tukisubiria kwenda kupima, wenye roho nyepesi walitoka na kusepa kimojaa. Ukitoka, ilikuwa ni lazima utoke na macho ya watu wote waliokuwepo hapo! Watu wakisikia purukushani kama za mtu kutaka kutoka, hasa kama alikuwa amekaa viti vya nyuma, walikuwa wakigeuka kimyakimya bila kusema chochote na kukupiga macho paa!

Mie nilitoka kwenda kupokea simu nje, walinikata macho, halafu nikasikia wadada fulani wawili wakisema amejibeep huyo! Dah, watu tulikuwa hatuaminiani kabisa! Niliwajibu, kwa taarifa yenu narudi!

Ikafika zamu yangu kwenda kuchukuliwa damu. Maongezi yangu na Dada mtoa damu yakawa hivi:

Dada: Karibu, kaa kwenye kiti (sikusalimia, maana hapo unasahau mengi), jina lako, taja majina matatu
Mimi: Simplicity. XXXX YYYY
Dada: Umri wako
Mimi: XXX
Dada: Unaishi wapi?
Mimi: Dar, Nimehamia Mbezi Kimara hivi karibuni
Dada: Kiwango chako cha elimu?
Mimi: Nimemaliza chuo, VETA
Dada: Umeoa/una mke?
Mimi: Sijaoa/sina mke
Dada: Unaishi na mwanamke/wanawake?
Mimi: Hapana, naishi mwenyewe
Dada: Namaanisha una mahusiano ya kimapenzi na wanawake?
Mimi: Hapana, nina mahusiano tu ya kawaida
Dada: Una mchumba/girlfriend?
Mimi: Sina mchumba wala girlfriend
Dada: Mara ya mwisho kushiriki ngono ilikuwa lini?
Mimi: Sijawahi kushiriki ngono
Dada: Wewe kaka, acha masihara, umekuja kufanya mzaha eee! Tafadhali umeshiriki ngono lini, mara ya mwisho, na ulitumia condom au haukutumia?
Mimi: Labda zamani, wakati tunacheza michezo ya utotoni, na sidhani hata kama nilimfanya mdada fulani enzi hizo tunacheza michezo ya baba na mama, kondomu sidhani kama zilikwepo enzi hizo. Sikumbuki chochote
Dada: Wewe kaka, naona umekuja kunipotezea muda! Sasa kama hujashiriki ngono unapima nini?
Mimi: Kwani ngoma inaambukizwa kwa kujamiana tu!
Dada: (Kwa hasiri kidogo) Haya leta mkono nichukue damu, na ukutwe unayo sasa!
Mimi: (Nikasema huyu dada hana maana, asije akanibambikizia status, sikumjibu kitu, nikajisemea, la asije akafanya makusudi)
Dada: chukua hiki kikaratasi kina namba yako, subiri nje utaitwa

Nikawa nimetoka zangu nje, ila dah, moyo ukawa unaenda sana mbio, kama mnavyojua, angaza huwezi kujiamini.

Baada ya kama dk 7, nikaitwa kwenda kuchukua majibu.

Dada: Karibu (Dada akawa mpole sana, halafu ananiangalia kwa huruma)
Mimi: A- h sa nte (Maneno yananikwama kooni!)
Dada: Umesema hujawahi kufanya ngono?
Mimi: Samahani dada wewe nipe mie majibu niende zangu
Dada: Kwa hiyo ulikuwa unanitania?
Mimi: Utani gani! Sijawahi kufanya ngono, na kama nimefanya sikumbuki ni lini
Dada: Subiri (katoka nje akamwita dada kutoka chumba kingine, nikasema, dah, majibu sio! Anatafuta ushauri namna ya kunipakulia au? Karibu nisepe alivyotoa huo mwanya lakini nikapiga moyo konde na kuamua kusubiria, baada ya kama dakika 2, Dada akarudi). Wewe kaka umeamua kwa moyo mweupe kabisa kuja kupima?
Mimi: (Nikasema, haya maswali kulikoni, kuna nini?) Ndio
Dada: Uko tayari kupokea majibu?
Mimi: Ndio
Dada: Unatambua kukutwa na maambukizi ya ukimwi sio mwisho wa kuishi?
Mimi: Ndio (Nikasema dah, something detected!)
Dada: Umeshawahi kusikia/kupata ushauri nasaha jinsi ya kuishi na virusi vya ukimwi?
Mimi: Nilishawahi kusikia radioni (Karibu nimnyang'anye daftari ambalo lilikuwa na majibu, najiuliza huyu kwa nini hanipi majibu! Nikazidi kuwa mpole)
Dada: Una watu wowote wanaokutegemea?
Mimi: Dada tafadhali naomba majibu kama unanipa
Dada: Sasa wewe unataka kupewa bila kufuata utaratibu!?
Mimi: Bwana mie nimechoka na maswali hayaishi (Nikamjibu swali lake)
Dada: Iwapo umekutwa na maambukizi ya ukimwi utafanyaje?
Mimi: Hakuna kitu kama hicho (Alicheka wakati mie jasho linanitoka!)
Dada: Wewe kaka una vituko! Hakuna si usingekuja sasa?
Mimi: Siwezi kuwa na uhakika kihivyo, ndio maana nimekuja!
Dada: Nakupa majibu kama utahitaji ushauri au elimu yoyote kuhusiana na ukimwi ofisi zetu ziko wazi Jtatu - Jumamosi, kuanzia saa mbili - saa nane mchana. Tafadhali tumia kondomu wakati wa kukutana kimwili.
Mimi: Naomba majibu (Mood yangu hapo imebadilika kabisa)
Dada: Kwa sasa hivi hauna maambukizi yoyote ya ukimwi, rudi tena kupima baada ya miezi mitatu.

Alivyomaliza tu kuongea sikumwaga, nduki nje, hakuna cha kwa heri wala nini! Kumbe nyuma nimesahau simu. Kidogo mtu ananikimbilia wee kaka umesahu simu yako. Dah huku jasho likiwa linanitoka, watu pale walinipiga macho, na wanaweza kuamini tofauti!

Angaza sio sehemu ya kufanyia majaribio, nenda kama umeamua kweli na tegemea chochote!

Dah, pamoja na kwamba jasho lilinitoka, lakini baada ya kuambiwa sina maambukizi nilitoka mwepesi kama air force one, huku moyo mweupe! Nilienda sehemu nikanunua grand malt, nikawa nakunywa huku nikipumzika taratibu!

Dah, kutokujua status yako ni zigo la misumiri, lakini kupima nako inahitaji ujivue ufahamu!

Nenda kapime ujue uwe huru.
 
Kazi zaidi ni kupewa uhakika kwamba kweli hakipo!

Uhakika upo

Nenda kamuulize ambae umeamua kwa hiyari yako kumpa mamlaka ya kukupa majibu ya asichokijua na hajawahi hata kukiona anachokiangalia kwenye damu yako na bado unadhani atakupa majibu ya uhakika kwamba unao au huna
 
Ndo raia uko juu ka coment ati ukimwi ishakuwa ugonjwa wa kawaida, labda kama anao la aivyo sikia tu kwa mwenzako
 
Mkuu inaonekana kuna mengi unayajua kuhusu hii ishu, funguka....

HIV haisababishi Ukimwi kwa namna yoyote ile kwasababu hakuna virusi vya aina hiyo,kwa kifupi hakuna aliewahi kuviona

Ukimwi upo lakini hausababishwi na virusi hao wa HIV,bali unasabishwa na mtindo wa maisha tu kama utumiaji wa pombe,madawa ya kulevya n.k

Ukimwi hauambukizwi kwa kujamiiana
 
Sijawahi kuogopa kupima maana nilikuwa lazima tupime ndo ku-do inafuata
Mkuu ina maana kila kabla ya ku do mnapima kwanza/kama ni hivyo demu hakimbii na kukuacga au kukuambia kuwa kwani unataka kumuoa/
BUT hongera...
 
Umenikumbusha last time nilivyopima. Ilikuwa ni lazima kwa waajiriwa wapya kufanyiwa medical checkup ya kila kitu hadi HIV. Hivyo nilitakiwa kwenda kwenye hospital waliyorecommend alafu majibu hospital yenyewe itapeleka.
Mpimaji akaniuliza uko tayari kupima HIV nikamjibu ndio ila majibu msinipe (sababu by then niligundua jamaa yangu alikuwa anachepuka). Baba wa watu akaendeleza ushauri mpaka kikaeleweka. Finaly nikapokea majibu yakiwa mazuri. Ila jasho lilinitoka na uzito ulipungua sababu sikuweza kula na majibu ilikuwa kesho yake
 
Mkuu ina maana kila kabla ya ku do mnapima kwanza/kama ni hivyo demu hakimbii na kukuacga au kukuambia kuwa kwani unataka kumuoa/
BUT hongera...
mkuu hata demu wangu nikishakuwa naye mbali nikirudi tunapima,hao vicheche wengi lazima angaza tukatobolewe kwanza
 
HIV haisababishi Ukimwi kwa namna yoyote ile kwasababu hakuna virusi vya aina hiyo,kwa kifupi hakuna aliewahi kuviona

Ukimwi upo lakini hausababishwi na virusi hao wa HIV,bali unasabishwa na mtindo wa maisha tu kama utumiaji wa pombe,madawa ya kulevya n.k

Ukimwi hauambukizwi kwa kujamiiana

Kwa hiyo watu huugua ninii???
 
mkuu hata demu wangu nikishakuwa naye mbali nikirudi tunapima,hao vicheche wengi lazima angaza tukatobolewe kwanza
Viol wewe ni nomaaaaaa,unajali sana,sipati picha sasa hivi wanakuangalia hapa kuwa ukitaka kuwagegeda unaenda kuwachoma...safi sana,mi nakuunga mkono,BIG UP,Wengine wanaogopa kumwambia kupima eti kamwangaikia muda MMrefu akimwambia kupima mara ya kwanza eti "ndege" atakimbia...
 
Hii tabia ya kupimapima hovyo mkidhani ni sifa iko siku mtu utajiharishia hadharani.fanya kupima pale kwenye umuhimu Tu. Michepuko siyo dili baki njia kuu.
 
Viol wewe ni nomaaaaaa,unajali sana,sipati picha sasa hivi wanakuangalia hapa kuwa ukitaka kuwagegeda unaenda kuwachoma...safi sana,mi nakuunga mkono,BIG UP,Wengine wanaogopa kumwambia kupima eti kamwangaikia muda MMrefu akimwambia kupima mara ya kwanza eti "ndege" atakimbia...
vicheche utawajua,ukiwaambia tukapime leo atakwepa mwishoni humgongi anaanza kukupotezea.
 
Back
Top Bottom