Ngao ya Sponji
JF-Expert Member
- Jul 26, 2018
- 341
- 541
Kwa Dunia ilipofikia Sasa Swala la KUPIMA DNA linapaswa liwe ni swala la Lazima Ili Kumlimda Baba, Mama na Mtoto kwa Ujumla.
Usipojua uhalali wa uhusiano wa Damu katika familia Yako inakuweka hatarini kupoteza kizazi Chako na pengine wewe ndio unaweza ukawa Mtu mwa mwisho katika kizazi Chako Kuishi maana utakua huna mtoto wa kuendeleza Damu Yako ya Asili.
Kila mtoto au Kila Mzazi anapswa kuwa na hakika Juu ya Uhalali wa Zao lake au Damu yake katika familia, na Inapaswa kisheria kumchukulia Hatua Kali Kwa yoyote atayepotosha Taarifa za Uzazi na kupelekea Familia kuishi na zao lisilokua la kwao
Ni mara chache sana hutokea Kwa Mwanamke bila kujua/kutofahamu ukweli Juu ya baba halisi wa mtoto na Hivyo kupelekea Naye kuongezwa kwenye kundi hili la waathiriwa wa Tatizo Hili.
Takwimu zinaonyesha Baba na mtoto ndio waathirika wakubwa wa janga hili la kubebeshwa damu zisizo za kwao Huku Mwanamke akiendelea kuinjoy ilihali akijua Hilo ni kosa mbele ya Sheria lakini pia mbele za Mungu.
Kwanini nasema DNA ni lazima?
Kuna Kesi nyingi sana za watoto kubadilishwa mahospitalini, Kwa sababu Moja au nyingine Kwa watu walio na nia ovu, kabla ya Wazazi kuondoka na mtoto wao Nyumbani ni lazima apimwe DNA kuhakikisha uhalali huo.
Lakini pia Kuhakikisha kwamba mtoto huyo ni Mali Halali ya Baba. kila Mtu abebe msalaba wake, Kama Mwanamke alipewa Mimba tofauti na Mwanaume aliyenaye basi Mwanaume huyo ahusike katika kulea mtoto wake, Gharama zote ziwe Juu yake isipokua Kwa MAKUBALIANO MAALUMU TU.
DNA IWE NI LAZIMA ILI KULINDA HESHIMA YA BABA NA FAMILIA KWA UJUMLA.