Jatropha
JF-Expert Member
- Apr 9, 2009
- 1,151
- 199
Sisi watanzania tumepatiwa malezi mema ya kupendana na kuthamini utu na ubinadamu. Ili kulinda na kutetea hali ya amani na utulivu watanzania tumelelewa na kufunzwa kuviheshimu na kuviamini vyombo vya dola ikiwemo Polisi, JWTZ n.k.
Hivyo haishangazi katika Tanzania kumkuta askari polisi mwenye mwili na umbo dogo akiwa hana silaha ya aina yeyote amemakamata mshukiwa mwenye mwili wa miraba minne na mshukiwa huyo kuongoza kituoni pasipo ubishi wala rabsha yeyote. Ndio utiifu ambao watanzania tumelelewa na kujengewa.
Kitendo cha hivi karibuni cha mgombea wa CCM Jimbo la Mwaswa Magharibi Ndg Simon Kisena kumpiga ngwara (mtama) Askari Polisi tena wa cheo cha OCD (Yaani Kamanda wa Polisi wa Wilaya) kimelistua taifa zima na kuthibitisha kuwa tofauti na madai yao ya viongozi wa CCM wakiongozwa na Jakaya Kikwete majukwaani kuwa vyama vya upinzania ndio vitasababisha fujo, vurugu, na kuhatarisha nchi kuingia katika machafuko na damu kumwagika; kitendo hicho kilichofanyika wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndg Yusuph Makamaba akiwa katika Jimbo hilo kinathibitisha kuwa CCM ndio imejipanga kufanya mambo hayo endapo itashindwa katika uchaguzi mkuu wa 2010.
Nini maoni yenu wadau wa amani na utulivu?