Kupigwa ngwara kwa ocd wa polisi ni utekelezaji wa mpango wa ccm kumwagaji damu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kupigwa ngwara kwa ocd wa polisi ni utekelezaji wa mpango wa ccm kumwagaji damu.

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Jatropha, Oct 25, 2010.

 1. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Sisi watanzania tumepatiwa malezi mema ya kupendana na kuthamini utu na ubinadamu. Ili kulinda na kutetea hali ya amani na utulivu watanzania tumelelewa na kufunzwa kuviheshimu na kuviamini vyombo vya dola ikiwemo Polisi, JWTZ n.k.

  Hivyo haishangazi katika Tanzania kumkuta askari polisi mwenye mwili na umbo dogo akiwa hana silaha ya aina yeyote amemakamata mshukiwa mwenye mwili wa miraba minne na mshukiwa huyo kuongoza kituoni pasipo ubishi wala rabsha yeyote. Ndio utiifu ambao watanzania tumelelewa na kujengewa.

  Kitendo cha hivi karibuni cha mgombea wa CCM Jimbo la Mwaswa Magharibi Ndg Simon Kisena kumpiga ngwara (mtama) Askari Polisi tena wa cheo cha OCD (Yaani Kamanda wa Polisi wa Wilaya) kimelistua taifa zima na kuthibitisha kuwa tofauti na madai yao ya viongozi wa CCM wakiongozwa na Jakaya Kikwete majukwaani kuwa vyama vya upinzania ndio vitasababisha fujo, vurugu, na kuhatarisha nchi kuingia katika machafuko na damu kumwagika; kitendo hicho kilichofanyika wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndg Yusuph Makamaba akiwa katika Jimbo hilo kinathibitisha kuwa CCM ndio imejipanga kufanya mambo hayo endapo itashindwa katika uchaguzi mkuu wa 2010
  .

  Nini maoni yenu wadau wa amani na utulivu?
   
 2. MTWA

  MTWA JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2010
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 1,024
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Kwa tanzania maana yake ni kunyamaza kimya, hakuna kuhoji hata uonewe ili mradi ni chombo cha dola.

  Hiyo ndo maana yetu sisi bongo, Lakini UKIENDA KINYUME ni lazima uwe mwenzetu, au kuna upande mwingine unaotuhumiwa kwa kosa kama hilo
  basi utakuwa unatafuta amani na utulivu, ila ukienda kinyume na chombo cha dola na siyo mwenzetu IMEKULA KWAKO
   
 3. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2010
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Hii mbaaya!
   
 4. W

  WAMURUBHERE JF-Expert Member

  #4
  Oct 25, 2010
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Askari Polisi tena wa cheo cha OCD (Yaani Kamanda wa Polisi wa Wilaya) kimelistua taifa zima na kuthibitisha kuwa tofauti na madai yao ya viongozi wa CCM wakiongozwa na Jakaya Kikwete majukwaani kuwa vyama vya upinzania ndio vitasababisha fujo, vurugu, na kuhatarisha nchi kuingia katika machafuko na damu kumwagika; kitendo hicho kilichofanyika wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndg Yusuph Makamaba akiwa katika Jimbo hilo kinathibitisha kuwa CCM ndio imejipanga kufanya mambo hayo endapo itashindwa katika uchaguzi mkuu wa 2010

  sahihisho kidogo hapo kwenye bold,OCD ni madaraka na si cheo chake (Officer Commanding District - Mkuu wa Polisi wa Wilaya)
   
 5. g

  glojos88 Member

  #5
  Oct 25, 2010
  Joined: Jul 31, 2010
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo ingetosha kuwa ni disqualification ya kutokuweza kuwa kiongozi anayefaa. Asiyefuata sheria. Kama unaweza kumfanyia fujo polisi mwenye cheo je huko barabarani watu wa kawaida itakuwaje?
   
 6. g

  glojos88 Member

  #6
  Oct 25, 2010
  Joined: Jul 31, 2010
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KUNA MTU ALISHAURI KUWA MAKAMBA NA HUYO MBUNGE WAKAMATWE KWANI NI MUHIMU WAO KUELEZA WANACHOKIJUA.
  Usikute kuna umafia unatumika ili kuonyesha picha kuwa CHADEMA wanataka kumwaga damu.
   
 7. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #7
  Oct 25, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Kibaya hapa ni kwamba ccm hawathamini maisha ya watu,wanawatuma vijana kwenda kufanya fujo wakati wakijua wanaweza kujeruhiwa wakawa vilema au hata kupoteza maisha.Hii ndiyo inaitwa kutumia maiti za watanzania kama ngazi za kupatia uongozi....mbaya sana.
  Mi nawahurumia hao vijana maana uchaguzi utapita na mambo yataendelea kama kawaida,wakifa ndugu zao watapata hasara na hakuna mwingine atakaye wakumbuka.
   
 8. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #8
  Oct 25, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Me ninge penda mtu atupe Scenario ya mambo yalivyokuwa mpaka kumfika mauti huyu mwana CCM,

  Je walikuwa wanaenda wapi hawa wana CCM?
  Walikuwa wanajua eneo fulani kuna mwendeleo wa Kampeni za chama fulani?

  Maana vyama vingine hulalamika sana kuwa panapo kuwa na kampeni za vyama vyao wanachama wa CCM na magari yao ya matangazo hupita pita mara kwa mara na sasa sijui hiyo ni kuashiria nini?

  Nadhani njia huwa ziko nyingi sana za kupita kuepusha shari au kusumbua mkutano wa mwenzio.

  Sasa haya ni ya kuchunguza ni nani manager kampeni? aliye waruhusu au aliye ruhusu msafara wa wana CCM kupita eneo la wanachama wengine CHADEMA huku walisha jua matatizo mengi yalisha tokea maeneo mengine kwani wao wasiepushe shari na wana enda kuanzisha shari?

  Kifo cha mwana CCM kweli kimeniuma sana na CCM walioongoza huo msafala lawama zangu kwao kwanini umwambie dereva apite huko?? Mlifuuta nini jamani. na Mbaya zaidi ni kuwa wewe mgombea ubunge CCM ulifikaje police na kumchota ngwala OCD hii yote sio asila bali ni kuashiria ulikuwa umejipanga kuanzisha mapambano kwa wana CHADEMA kama watu wameshikwa wewe ulitakiwa ufuatilie sheria inasemaje ili uwaweke hao ndani sasa matokeo yake wewe ndio umenda mpiga police kituoni umepoteza jimbo kwa wana CCM tayari khaaa
   
 9. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #9
  Oct 25, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nauliza: Hivi kosa la kumpiga polisi adhabu yake ni nini mtu akipatikana na hatia chini ya Kanani ya Adhabu? Sina hakika mimi, lakini nadhani ni kifungo tu bila ya faini. Kama ni hivyo, unless kina Makamba/Manumba/ridhwani watamuokoa, huyo mgombea wa CCM sasa ni finished politically.

  Labda compromise moja tu inaweza kumuokoa huyu, kwamba wote wawili -- yeye na Shibuda waachiliwe mara moja. In fact kosa la Shibuda silioni, hakuwepo eneo la tukio, labda wa-prove kwamba aliwatuma wafuasi wake wakamwuue huyo dereva.
   
 10. Gerad2008

  Gerad2008 JF-Expert Member

  #10
  Oct 25, 2010
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 489
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Kitendo cha Mgombea wa CCM jimbo la Maswa kumpiga ngwara OCD na kuelezwa kuwa ni jambo la Kawaida ni kutaka tu kumbeba ili shibuda abebe mzigo wote wa tukio la Mauaji. Ukweli ni kwamba kumshambulia askari aliyevaa sare tena akiwa kazini si kawaida kuvumilika na hawa jamaa kwani huwa wanahakikisha ukitoka hapo hutakaa uzae tena.

  Hii ya Maswa imekaa kuvumilia maumivu kutokana na kwamba CCM inataka ionekana katika hili ni Malaika. OCD aliyekuwa Arusha ambaye sasa ni RPC kagera ndg Henry Salewi aliwahi sogelewa tu kwa kutishiwa na mfanya biashara wa kizungu hapa na ikawa kabla ya kumfikia alipigwa kipigo cha mbwa mwizi na kupakiwa kwenye pickup ya polisi akiwa kazirai na kuzindukia hospitalini. Hii ya OCD kupigwa mtama halafu akapiga kimya ni mbinu za CCM ila najua yeye OCD mpaka sasa ana HASIRA. HII NI SAWA NA KUPIGWA NA MTOTO WA BOSI WAKO UNAYEMTEGEMEA KWA KILA KITU.
   
 11. kiraia

  kiraia JF Gold Member

  #11
  Oct 25, 2010
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 1,614
  Likes Received: 268
  Trophy Points: 180
  Kweli huyu OCD kapigwa na mtoto wa bosi wake na hatathubu kulalamika wala kuchukua hatua yoyote, angekuwa ni mgombea wa chadema tayari angeshapandishwa kizimbani na asingepewa dhamana hadi uchaguzi umalizike.
   
 12. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #12
  Oct 25, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  kwa hakika ndg simon kisena hafai kuwa kiongozi kutokana na kitendo chake cha kumshambulia ofisa wa polisi tena wa ngazi ya juu sana. Kama ndg simon kisena ameweza kuwa na ujasiri wa huo nini kitkufika wewe mwanachji wa maswa magaharibi utakapokwenda kudai ndg kisena ahdi zake kama vile maji, elimu, afaya n.k. Je mwanachi utatoka salama?.

  Kwa heshima ya ndg shibuda chadema iendeleze kampeni katika jimbo hilo ikieleza wazi wazi kuwa ndg simon kisena ni mhuni asiyefaa kuwachaguliwa. Ni mtu wa kuogopwa kama ukoma!!!!!!!!!
  !
   
Loading...