Kupigwa mnada Ng'ombe toka Kenya: Tanzania na Kenya walishindwa kufikia makubaliano katika mazungumzo ya kidiplomasia

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,929
Waziri wa mambo ya nje nchini Kenya Amina Mohamed ameilalamikia serikali ya Tanzania kufuatia hatua ya taifa hilo kuwapiga mnada zaidi ya ng'ombe 1,300 walioingia nchini humo kinyume na sheria.

Serikali ya Rais John Magufuli ilichukua hatua hiyo baada ya wafugaji kuingia nchini humo na mifugo wao wakitafuta lishe.

Hatua hiyo inajiri siku moja tu baada ya Rais Magufuli kusema kuwa taifa hilo sio shamba la mifugo wa taifa jirani.

Hatua ya kuwapiga mnada ng'ombe hao ilizua hisia kali miongoni mwa wafugaji wa Kenya baada ya wenzao waliokuwa na mifugo hao kukamatwa na kuzuiliwa kwa kuingia nchini humo kinyume na sheria.

Na kufuatia hatua hiyo waziri wa mambo ya nje nchini Kenya Amina Mohammed alidaiwa kuanzisha mazungumzo kati ya serikali hizi mbili kutatua mzozo huo, mazungumzo ambayo yalishindwa kufua dafu.

''Tulidhani kwamba mazungumzo ya kidiplomasia yangetatua mzozo huu, lakini tulishindwa kuafikia makubaliano. Ni wakati huo ambapo tuliamua kuzungumza na balozi wetu nchini humo kuwasilisha barua ya kupinga hatua ya kuwapiga mnada mifugo hao''.

''Historia ambayo tumekuwa nayo na Watanzania ni nzuri sana na kila kunapotokea tatizo tumekuwa tukitatua.Ni kwa sababu hiyo ambapo imekuwa hatua ya kushangaza miongoni mwa wafugaji wa Kenya'', waziri huyo alizungumza katika mkutano na vyombo vya habari.

Bi Mohamed amesema kuwa Kenya imekuwa ikiwavumilia wafugaji wa nchi jirani ambao wamekuwa wakivuka na kuingia katika eneo la Kajiado nchini Kenya kwa wingi.

''Barua yetu ya pingamizi ni kuonyesha wasiwasi wetu kuhusu kisa kilichotokea licha ya kuwepo katika mazungumzo, tunatumai tutasuluhisha tatizo hili'', alisema waziri Mohamed.

Mazungumzo baina ya nchi hizo mbili bado yanaendelea.

CHANZO: BBC
 
Mambo yalishabadilika, aliyepita aliwalea lakini tukasikia tusikia kuna 'Coalition of the willing'willing' huyu wa sasa hivi halei tena vitu kama hivyo. Wawashaur wafugaji wao wapunguze mifugo.
 
Kwenye hili la Kenya Nampa big up sana mhe rais; Wakenya wana dharau sana tena sana; hua namshukuru sana hata mhe Kikwete alipowapigaga mkwara kuhusu ndege zao kutua Dar Airport; kwa ufupi nimefanya kazi na Wakenya, I know them. Mhe rais hivyo hivyo tu. Bado nakumbuka sakata la kiwanda cha maziwa Mara Milk na tenda yao walio ipataga ku supply maziwa kwenye kampuni moja ya kigeni kule Kenya, serikali ilijizungusha kutoa kibali muda mrefu hadi mkataba ule uka expire. Hua nina IMANI na Mkenya aliye kufa tu, Mkenya aliye HAI hua sina IMANI nae kabisa.
 
Ng'ombe hao wameingia nchini kinyume cha sheria,sasa Kenya ilitegemea Tanzania ifanye nini,ichekee watu wanaovunja sheria?No way.Hatua serikali iliyochukua ni sahihi kabisa.Wafugaji,hasa Wamasai, ni jamii korofi sana.Hawaheshimu sheria kabisa,kwa sababu ya hongo wanazotoa.Wamasai ni wahongaji wazuri sana.Adha ya Mifugo ya Wamasai imenikuta,sisimuliwi,I simply don't like the Masais,hawana adabu kabisa.Mimi niseme kwamba hatua serikali iliyochukua itawafanya waogope na wasirudie tena.

Jamani msisimuliwe,Ng'ombe wanaharibu ardhi sana,through hardpan formation,soil erosion and even wind erosion.Tatizo lingine ambalo linasababishwa na mifugo ya Wamasai ni kwamba tunashindwa kabisa kufanya land development,let alone trespassing ambayo inakera kweli kweli.Umekaa na watoto wako, ghafla unaona ming'ombe inapita!I don't like it. I wish JPM would equally be tough on local Masais,wanakera sana.No,it's high time the carrying capacity of every agro-ecosystem is adhered to.Kila kijiji viongozi wake wasimamie jambo hili kikamilifu.They must be forced to do it, kwa kuwa najua wengi hawako intersted,simply because it's a source of their livelihood(hongo).

We as farmers simply don't understand the government,we want something done and quick,Wamasai wanatuonea sana.The government is simply too slow in settling the Masai-Farmer problem once and for all.Wamasai wanaendelea kutamba tu huku vijijini, wakati viongozi wa vijiji,kata,tarafa na Wilaya wapo.No,haikubaliki,na kama nilivyotangulia kusema, hatuilewi serikali,it is too soft on this issue,kuna nini?
 
Ukizingatia juzi juzi vifaranga vilichomwa moto basi watanyooka tu
 
Kwenye hili la Kenya Nampa big up sana mhe rais; Wakenya wana dharau sana tena sana; hua namshukuru sana hata mhe Kikwete alipowapigaga mkwara kuhusu ndege zao kutua Dar Airport; kwa ufupi nimefanya kazi na Wakenya, I know them. Mhe rais hivyo hivyo tu. Bado nakumbuka sakata la kiwanda cha maziwa Mara Milk na tenda yao walio ipataga ku supply maziwa kwenye kampuni moja ya kigeni kule Kenya, serikali ilijizungusha kutoa kibali muda mrefu hadi mkataba ule uka expire. Hua nina IMANI na Mkenya aliye kufa tu, Mkenya aliye HAI hua sina IMANI nae kabisa.
Kweli kabisa mkuu,hata mm nimekaa kenya muda mrefu niliona wanavyomdharau mtz,kwa wale ambao hawawajui wakenya wasingelaumu hiki alichofanya Rais wetu.Kwa mfano,sisi tulio mpakani, tukienda kuuza vitu kwao, wanatufukuza.
 
Dawa ni dikteta kununua ng'ombe wengine kuwafidia hao wafugaji wa ndugu zetu Wakenya period, hizi akili za kijinga jinga za kutaka kupata hela kwa njia zozote hata haramu ni lazima ipigwe vita na kila mwana Afrika Mashariki!
 
Kama bwai na iwe bwai tu. Kila nchi ichunge mifugo yao. Shida ni kwamba. Kila sehemu Kenya ni shamba la MTU sehemu ya kufungia na aina MTU ni TANZANIA. Tena mbuga za wanyama. Kwao wanatunza. Sisi haahaa. Magufuli kaza kwamba wanyooke
 
Tatizo tunaongea tu tunasahau kuwa kuna mikataba ya Africa mashariki ya FREE MOVEMENT OF PEOPLE AND GOODS kila nchi ilisaini na ilikubali ku implement sasa tunategemea nini mgogoro au, hii inaitwa violation, nahitaji kuwaona wanao mshauri rais wawe wanamkumbusha hii mikataba na inafanyaje kazi ili tukubaliane vinginevyo tuvunje mkataba wa africa mashariki
 
Back
Top Bottom