beautifulonyinye
JF-Expert Member
- Mar 16, 2015
- 728
- 481
Habarini za asubuhi wakuu, natumai ni wazima sana. Leo nina swali kwa wanandoa au wenye mahusiano ya mbali, mimi mume wangu siyo kwamba anafanya kazi nje ya mkoa ila amesafiri kikazi kwa muda tu ana kama karibia miezi 2.
Ila mwenzangu huyu hapigi simu ni ujumbe tu, sasa mimi hicho kitendo kinaniudhi sana na akipiga kidogo utasikia dk. zimeisha, sasa najiuliza dk. zimeisha anaongea na kina nani?
Sasa swali langu kwa wanandoa hasa wenye upendo na wake/waume/wapenzi wao, wanaweza kaa hata siku 3 bila kumpigia simu mwenza wake, yaani ni kawaida au kuna shida pahala?
Naomba maoni yenu hasa kwa wanaume waliokuwa makini na wake/wapenzi wao, namaanisha wenye upendo wa Agape.