Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kupiga Chafya

Discussion in 'JF Doctor' started by fungamesa, Jun 13, 2012.

 1. f

  fungamesa Senior Member

  #1
  Jun 13, 2012
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 127
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Jamani naomba msaada. Maana huwa napiga chafya sana kila ninapohisi kunusa vumbi, mtu akivuta sigara moshi tu ukipita mbele yangu, pia kama natafuta nguo kabatini, nikipulizia pafyumu n.k. Chafya hiyo huambatana na mafua mepesi. Naomba mwenye kujua dawa yake nifanyaje maana hospitali huwa napewa piliton, chengachenga n.k bila mafanikio.
   
 2. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #2
  Jun 13, 2012
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,580
  Likes Received: 156
  Trophy Points: 160
  Ni dhahiri wewe una allergy na kemikali (allergen) nyingi tu, hilo hutokea kwa watu wengi sana (mimi mmojawapo). Kemikali hizo husababisha mwasho kwenye njia ya hewa na mwili wako kureact kwa kutoa vichocheo (sana sana Histamine) kadhaa ambavyo ndivyo vinavyofanya upate mafua mepesi kama maji!

  Dawa kubwa na ya hakika kwa allergy ni kuepuka hizo allergen zinazokusababishia hali hiyo, lakini hili si rahisi hivyo. Unaweza pia ukatumia dawa za jamii ya Anti-Histamine ambazo zinazuia kichocheo cha Histamine kisifanye kazi na kukusababishia muwasho na mafua, Piriton ni moja ya dawa hizo...except Piriton ina sedating effect hivyo inalaza laza (drowsiness), ni vyema kuitumia usiku kama huna kazi za kufanya. Dawa nzuri ni jamii ya Loratadine (Claritine, Clarityn, Claritin) lakini ni effective ukimeza pindi tu umekuwa exposed kwa hizo allergen, au kabla ya kuanza kazi za ndani ambazo unaexpect utakuna na hizo allergen...Pole!
   
 3. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #3
  Jun 13, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,245
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Pole mkuu, Nichukuwe fursa hii kumshukuru dr.RIWA kwa kueleza kwa uzuri kabisa kuhusu aleji/mzio, ameelezea pia kuhusu histamine na akataja dawa zinazoweza kuidhibiti hiyo histamine (anti-histamine). Kwanza niseme tu anti-histamine ni dawa zenye madhara hasi mengi zaidi mwilini kuliko hata hiyo aleji yenyewe. Kusema ukweli ni vigumu sana kuitibu aleji/mzio kwa sayansi za hospitalini.

  MAJI HUKINGA NA KUPONYA MZIO (Allergy):


  Mzio/allergy, Ni kitendo cha mwili kupungukiwa maji wakati histamini inapozarishwa kupita wastani ili kuhimiza unywaji wa maji na ugawanywaji wa kiasi kidogo cha maji kipatikanacho mwilini.


  Histamini ni kihisio cha kwanza (primary sensor) cha ubongo kinachozarishwa ili kujishughurisha na ugawanywaji wa maji kwa viungo mhimu wakati kunapokuwa na upungufu wa maji mwilini.


  Inajihusisha na kazi ya ugawanywaji wa kiasi kidogo kinachopatikana cha maji (maji ya mgawo) wakati wa upungufu wa maji mwilini (Unintentional chronic dehydration).


  Histamini katika lugha rahisi:


  Histamini ni kemikali ambayo miili yetu huitoa inapohitaji msaada kusawazisha upungufu wa vitu mhimu sana mwilini kama maji, chumvi au potasiamu. Histamini na wasaidizi wake wengine watano (5 buddies) watasaidia kuusawazisha upya mwili ambao upo nje ya usawa.


  Kwa hakika Histamini ni kitu kizuri ambacho huokoa maisha yetu kwa mujibu wa dr. Batmanghelidj. Bonyeza hapa kusoma yote: http://maajabuyamaji.net/maajabu/mzioaleji/
   
Loading...