Sina hakika kama kichwa cha habari kinabeba nachotaka kusema, ndio maana nimeweka kama swali.
Kuna ile unaishi na majirani au ofisini, basi inatokea mtu anakujali kuliko wengine au anajaribu kutengeneza ukaribu kwa makusudi kabisa. Yaani unaona s/he is trying too hard kuwa karibu yako kwa kukuletea vitu au kila saa kukufuata na kuongea hata kama hakuna common interest.
Kama ndio majirani utasikia watoto wameletwa waje wacheze na wa kwako. Kama wakubwa basi wanatumwa kuja kukusaidia sijui nini. Mradi tu someone is all over you.
Na hii ipo pia kwenye shule za wasichana, mtu anakujaali bila sababu ya msingi, unabaki unashangaa anataka nini?
Sasa mie huwa nakuwa very uncomfortable, siamini kuna free lunch duniani kiasi hicho, sijui how to reciprocate kujali huko. Nakuwa naona kama mtu anainunua roho yangu.
Wengine huwa mna deal nayo vipi hii?