Kupenda si kanuni

KENZY

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
36,634
Reaction score
89,398
Kuna usemi usemao mapenzi ni upofu, kupenda huamuliwa na ubongo na ubongo huohuo hujiundia kanuni kwa yule umtakae lakini mara nyingi hili huwa halitekelezeki.

Watu wengi hujiwekea kanuni katika mapenzi kwamba mimi namtaka msichana au mvulana mweupe, mweusi, mrefu, mfupi n.k lakini hujikuta ameangukia kwa mtu ambae anasifa tatu tu kati ya zile azitakazo.

Mapenzi ni kama ukurasa mweupe ulioandikwa kwa karamu nyeupe hivyo hayatabiriki, penda ya kujisemea ukitakacho si penda iliyopo katika ukurasa mweupe wenye maneno meupe.

Hili litofautishwe na lile la pale ulipopenda ni sahihi au si sahihi. Jihadhari katika ushauri uutoao kwa wale wanaopendana maana kamba zilizowaunga huenda wewe huzijui wala wao pia.

KUPENDA HUAMBATANA NA KURIDHIA mwambie mpenzi wako ya kuwa UNAMPENDA.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Unaenda wapi eti
nimepita tu nilikuwa nakusalimia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…