Yathibitika Wenye mihemko ya kupenda sana ngono wataalamu wabaini si hiyari yao…!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,393
upload_2016-10-6_16-54-27.png


Wataalamu nchini Ufaransa wamesema kwamba, hatimaye wamebaini, sehemu ya ubongo inayowapeleka watu puta wanapompenda mtu kimapenzi na kuwa kama vichaa. Wamesema eneo la ubongo linalofahamika kama amydala, ndilo linalohusika.

Wamebainisha kwamba, kwa kadiri eneo hilo linavyokuwa kubwa ndivyo ambavyo mtu anavutwa kimapenzi haraka na kwa mshawasha mkubwa zaidi. Hii ina maana kwamba, wale wanaosukumwa kupenda haraka na kuwehushwa na kupenda, siyo hiyari yao, bali ni namna tu ubongo wao ulivyotengenezwa.

Eneo hili la ubongo huchokozeka haraka zaidi kuliko eneo lingine, pale mtu anapoingia katika kumpenda mtu. Kabla ya ugunduzi huu, eneo hilo la ubongo lilikuwa likifahamika kwa kazi yake ya kuwafanya wanyama kuvutana kwa lengo la kupandana.

Kwa hiyo hamu au kiwango cha kusukumwa mtu kufanya mapenzi , au kuvutika kimapenzi, kinategemea pia pamoja na mambo mengine, ‘saizi’ ya eneo hilo la ubongo.

Kwa hiyo kwa wale waliokuwa wakishangazwa na baadhi ya wanaume au wanawake wenye tabia ya kupenda sana ngono na kuwa kama vichaa kutokana na kupenda huko naamini sasa wamepata jibu kwamba si kulogwa bali ni tatizo la kwenye ubongo.

Mtuwache maana sasa mmeshajua sababu.....
 
Back
Top Bottom